mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Katika hali ya kawaida, ungetegemea wananchi kutokuunga mkono mapinduzi dhidi ya viongozi wao waliowachagua wenyewe!! Tatizo ni kwamba baada ya kuchaguliwa viongozi huamua kuwa vibaraka wa mabeberu wa nchi za magharibi na kuwasahau wananchi waliowaweka madarakani! Sasa Rais aliyepinduliwa badala ya kutetewa na wananchi wake, anatetewa na mabeberu wa magharibi!! Ni aibu!!
Endeleeni kuwaabudu mabeberu wa KiarabuMapinduzi sahihi na bora Afrika ni yale mapinduzi matukufu ya ZANZIBAR....
Baada ya mapinduzi hayo tukaasisi chama kiitwacho "MAPINDUZI"....
Hiki ndicho chama bora ambacho hakitoi upenyo wa MAPINDUZI YA KIJESHI.....
LIDUMU TAIFA LA JMT ,amen[emoji120]
Umri wako hauja kusaidia kitu maana sujaona gadafi gapo pia unafananisha mapinduzi yaliofanywa na uneducated na haya ya Sasa yanayofanywa na educated person? Unafananisha enzi Dunia IPO gizani na Sasa ambapo baada ya mapinduzi unaweza Kodi mpaka consultant wa kiulinzi achilia mbali wa kiuchumi lohNina umri wa kutosha kuelewa kuwa 90% ya mapinduzi ya kijeshi huwa hayaleti maendeleo yoyote. Mengi huwa yana nguvu ya soda tu na baadaye huharibu nchi zao kwa kuondoa misingi ya utawala bora.
(1) Amin alipopindua Uganda, wanafunzi wa Makerere na umma mkubwa wa Kampala walifurahi na kuandamana kwa furaha kwa vile walimchukia Obote. Baada ya mwaka mmoja wakaanza kulia.
(2) Baada ya kuuwawa kwa Rais Shermake wa Somalia kwa sababu za kikabila kulitokea vurugu na hadi Siad Bare akaingilia kati kijeshi kuchukua madaraka. Matokeo yake Somalia imekuwa ni lawless state kwa zaidi ya miaka 50 sasa. Ni nchi ambayo watu wake ndio wakimbizi wengi duniani.
(3)Baada ya njaa ya Ethiopia ya mwaka 1974 ambapo mfalme Haile Selassie alikuwa akiishi maisha ya kifahari, jeshi lilimpindua na watu wengi walifurahi. Hata hivyo utawala wa kijeshi wa ethiopia uliirudisha nyuma sana ethipoia kiasi kuwa mpaka leo unajua jinsi waethiopia huwa wanashikwa wakikimbilia nchi nyinghine. Ni miaka ya hivi karibuni tu baada ya utawala wa kiraia kurudi ndipo Ethiopia imeanza kuimarika.
(4) Nigeria walilimpindua na kumwua aliyekuwa Waziri Mkuu Tafawa Balewa pamoja na wasaidizi wake Ahmadu Belo, Samuel Ankintola, Festos Okotie-Oboh. Kuna raia walifurahia mapinduzi hayo na kuna walioyapinga. Matokeo yake Nigeria ilivurumisha na vita ya wenyewe kwa wenyewe huko Biafra na kugeuka nchi yenye rushwa kwa muda mrefu sana hadi miaka ya hivi karibuni tu ndipo wameanza kustabilize na kurudia utawala wa kiraia.
(5) Chad
(6) Sudan
(7) Central African Republic
(7) Equatorial Guinea
Mifano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi ipo mingi sana; labda uondoe yale ya Nasser, ingawa alifariki baada ya muda mfupi na hatujui nchi ingeendeleaje iwapo angekaa madarakani muda mrefu. Mtu mwingine labda ni Ghadaffi ingawa alikuwa anawapa raia wake vitu vya bure, hakujenga taifa imara kwa maana ya kuwa na one man rule. Baada ya kupinduliwa na yeye tunaijua Libya ikoje kwa vile watu wake wengi walikuwa hawakuandaliwa mabadiliko ya uongozi. Thomas Sankara alikuwa ameleta matumaini lakini naye alipinduliwa na kuuwawa baada bya muda mfupi na mwanajeshi mwenzie; matokeo yake tunaijua Burkina Faso ikoje hadi leo.
Laana tupu kwa viongozi.Katika hali ya kawaida, ungetegemea wananchi kutokuunga mkono mapinduzi dhidi ya viongozi wao waliowachagua wenyewe.
Tatizo ni kwamba baada ya kuchaguliwa viongozi huamua kuwa vibaraka wa mabeberu wa nchi za magharibi na kuwasahau wananchi waliowaweka madarakani.
Sasa Rais aliyepinduliwa badala ya kutetewa na wananchi wake, anatetewa na mabeberu wa magharibi.
Ni aibu!!
Kwa vile unasoma na mindest fulani huwezi kuelewa mambo kwani kama hata kuweza kusoma Ghadafi kweny post hiyo ni dhahiri hujui unachosma au unachofikiria. Kuhusu kuelimika, elewa kuwa hilo ni jamo relative sana na linategemea jamii husika. Tulipoata uhuru watu wenye digrii walikuwa hawachache sana, na baraza la mawaziri la nyerere halikuwa na graduate yeyote ispokuwa yeye mwenyewe; wengine wote walikuwa ni darasa la 12. 14 na diploma lakini waliongoza vizuri.Umri wako hauja kusaidia kitu maana sujaona gadafi gapo pia unafananisha mapinduzi yaliofanywa na uneducated na haya ya Sasa yanayofanywa na educated person? Unafananisha enzi Dunia IPO gizani na Sasa ambapo baada ya mapinduzi unaweza Kodi mpaka consultant wa kiulinzi achilia mbali wa kiuchumi loh
Ukiona wananchi wanaunga mkono mapinduzi ya kijeshi ujue serikali ilishawatelekeza siku nyingi!! Watawala walishakuwa vibaraka wa mabeberu wa nchi za magharibi!! Watawala wanapokea rushwa halafu wanauza raslimali kwa bei ya kutupa!! Mabeberu hawana aibu, wako tayari kumpigania kibaraka wao kinyume na matakwa ya raia walio wengi, kwao hiyo ndiyo demokrasia wanayodai!! Najua MK254 wewe ni mshabiki wa mabeberu na hufumbia macho maovu yao yote!!Ni kosa kuunga mikono uongozi wa kijeshi, na watajilaumu sana baadaye, uongozi wa kijeshi huwa haukosolewi, sio kama hapo Bongo leo mnamsema mama Samia kwa issue ya bandari, mna uhuru wa kumkatalia, ingekua jeshi hamngesema chochote, jeshi lingewapa Waarabu bandari zote kibabe tu bila kukosolewa.
Na wala haitachukua muda kabla huyo kiongozi wa kijeshi hajaingizwa mkenge na wanaoiba raslimali za nchi, na siku akianza kuwaskliza, hakuna mwananchi atamkosoa.
Halafu nchi za magharibi ni wanafiki sana!! Hudai kutetea demokrasia sasa wanaona kabisa matakwa ya wananchi walio wengi lakini bado wanaamua kumpambania kibaraka wao. Demokrasia ni kufuata matakwa ya walio wengi, lakini hapo hilo watalifumbia macho!!Laana tupu kwa viongozi.
Mtu anawaza kuiba mali za umma kwa ulafi kisha anataka aungwe mkono na wale wenzangu wa pangu pakavu tia mchuzi.
Kuna mataifa ya kiafrika mengine serikali na viongozi wao wamegeuka mbwa mwitu, yaani wao ni kutapanya mali, kodi za kikoloni, kuuza raslimali za umma kwa bei ya chenji, kutetea wezi wenzao, kutekeleza mipango miovu ya usitawi wa jamii ikiwemo utoaji wa elimu duni kwa wananchi wa kawaida.
Viongozi wanawabebesha wananchi mzigo mzito usiobebeka wa kulipia madeni ya vitu ambavyo havikufanyika au vimefanyika chini ya kiwango, mikataba ya hovyo et al.
Vp hapa jirani Rwanda kwa kagame?Nina umri wa kutosha kuelewa kuwa 90% ya mapinduzi ya kijeshi huwa hayaleti maendeleo yoyote. Mengi huwa yana nguvu ya soda tu na baadaye huharibu nchi zao kwa kuondoa misingi ya utawala bora.
(1) Amin alipopindua Uganda, wanafunzi wa Makerere na umma mkubwa wa Kampala walifurahi na kuandamana kwa furaha kwa vile walimchukia Obote. Baada ya mwaka mmoja wakaanza kulia.
(2) Baada ya kuuwawa kwa Rais Shermake wa Somalia kwa sababu za kikabila kulitokea vurugu na hadi Siad Bare akaingilia kati kijeshi kuchukua madaraka. Matokeo yake Somalia imekuwa ni lawless state kwa zaidi ya miaka 50 sasa. Ni nchi ambayo watu wake ndio wakimbizi wengi duniani.
(3)Baada ya njaa ya Ethiopia ya mwaka 1974 ambapo mfalme Haile Selassie alikuwa akiishi maisha ya kifahari, jeshi lilimpindua na watu wengi walifurahi. Hata hivyo utawala wa kijeshi wa ethiopia uliirudisha nyuma sana ethipoia kiasi kuwa mpaka leo unajua jinsi waethiopia huwa wanashikwa wakikimbilia nchi nyinghine. Ni miaka ya hivi karibuni tu baada ya utawala wa kiraia kurudi ndipo Ethiopia imeanza kuimarika.
(4) Nigeria walilimpindua na kumwua aliyekuwa Waziri Mkuu Tafawa Balewa pamoja na wasaidizi wake Ahmadu Belo, Samuel Ankintola, Festos Okotie-Oboh. Kuna raia walifurahia mapinduzi hayo na kuna walioyapinga. Matokeo yake Nigeria ilivurumisha na vita ya wenyewe kwa wenyewe huko Biafra na kugeuka nchi yenye rushwa kwa muda mrefu sana hadi miaka ya hivi karibuni tu ndipo wameanza kustabilize na kurudia utawala wa kiraia.
(5) Chad
(6) Sudan
(7) Central African Republic
(7) Equatorial Guinea
Mifano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi ipo mingi sana; labda uondoe yale ya Nasser, ingawa alifariki baada ya muda mfupi na hatujui nchi ingeendeleaje iwapo angekaa madarakani muda mrefu. Mtu mwingine labda ni Ghadaffi ingawa alikuwa anawapa raia wake vitu vya bure, hakujenga taifa imara kwa maana ya kuwa na one man rule. Baada ya kupinduliwa na yeye tunaijua Libya ikoje kwa vile watu wake wengi walikuwa hawakuandaliwa mabadiliko ya uongozi. Thomas Sankara alikuwa ameleta matumaini lakini naye alipinduliwa na kuuwawa baada bya muda mfupi na mwanajeshi mwenzie; matokeo yake tunaijua Burkina Faso ikoje hadi leo.
Ukiona wananchi wanaunga mkono mapinduzi ya kijeshi ujue serikali ilishawatelekeza siku nyingi!! Watawala walishakuwa vibaraka wa mabeberu wa nchi za magharibi!! Watawala wanapokea rushwa halafu wanauza raslimali kwa bei ya kutupa!! Mabeberu hawana aibu, wako tayari kumpigania kibaraka wao kinyume na matakwa ya raia walio wengi, kwao hiyo ndiyo demokrasia wanayodai!! Najua MK254 wewe ni mshabiki wa mabeberu na hufumbia macho maovu yao yote!!
Mi nadhani ni kwasababu jumuia za kimataifa huzitenga nchi zilizopinduliwa kijeshi.Nina umri wa kutosha kuelewa kuwa 90% ya mapinduzi ya kijeshi huwa hayaleti maendeleo yoyote. Mengi huwa yana nguvu ya soda tu na baadaye huharibu nchi zao kwa kuondoa misingi ya utawala bora.
(1) Amin alipopindua Uganda, wanafunzi wa Makerere na umma mkubwa wa Kampala walifurahi na kuandamana kwa furaha kwa vile walimchukia Obote. Baada ya mwaka mmoja wakaanza kulia.
(2) Baada ya kuuwawa kwa Rais Shermake wa Somalia kwa sababu za kikabila kulitokea vurugu na hadi Siad Bare akaingilia kati kijeshi kuchukua madaraka. Matokeo yake Somalia imekuwa ni lawless state kwa zaidi ya miaka 50 sasa. Ni nchi ambayo watu wake ndio wakimbizi wengi duniani.
(3)Baada ya njaa ya Ethiopia ya mwaka 1974 ambapo mfalme Haile Selassie alikuwa akiishi maisha ya kifahari, jeshi lilimpindua na watu wengi walifurahi. Hata hivyo utawala wa kijeshi wa ethiopia uliirudisha nyuma sana ethipoia kiasi kuwa mpaka leo unajua jinsi waethiopia huwa wanashikwa wakikimbilia nchi nyinghine. Ni miaka ya hivi karibuni tu baada ya utawala wa kiraia kurudi ndipo Ethiopia imeanza kuimarika.
(4) Nigeria walilimpindua na kumwua aliyekuwa Waziri Mkuu Tafawa Balewa pamoja na wasaidizi wake Ahmadu Belo, Samuel Ankintola, Festos Okotie-Oboh. Kuna raia walifurahia mapinduzi hayo na kuna walioyapinga. Matokeo yake Nigeria ilivurumisha na vita ya wenyewe kwa wenyewe huko Biafra na kugeuka nchi yenye rushwa kwa muda mrefu sana hadi miaka ya hivi karibuni tu ndipo wameanza kustabilize na kurudia utawala wa kiraia.
(5) Chad
(6) Sudan
(7) Central African Republic
(7) Equatorial Guinea
Mifano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi ipo mingi sana; labda uondoe yale ya Nasser, ingawa alifariki baada ya muda mfupi na hatujui nchi ingeendeleaje iwapo angekaa madarakani muda mrefu. Mtu mwingine labda ni Ghadaffi ingawa alikuwa anawapa raia wake vitu vya bure, hakujenga taifa imara kwa maana ya kuwa na one man rule. Baada ya kupinduliwa na yeye tunaijua Libya ikoje kwa vile watu wake wengi walikuwa hawakuandaliwa mabadiliko ya uongozi. Thomas Sankara alikuwa ameleta matumaini lakini naye alipinduliwa na kuuwawa baada bya muda mfupi na mwanajeshi mwenzie; matokeo yake tunaijua Burkina Faso ikoje hadi leo.
Kuna sehemu nimeona bendera ya urusi.aisee maisha yanaenda Kasi mno.wananchi wanaunga mkono mapinduzi ya kijeshi kwenye nchi yao.
.
Kumbuka rais aliyepinduliwa aliekwa madarakani na demokrasia, sio kidiktetaKatika hali ya kawaida, ungetegemea wananchi kutokuunga mkono mapinduzi dhidi ya viongozi wao waliowachagua wenyewe.