Wananchi wa Niger waunga mkono mapinduzi ya kijeshi. Wanasisa wa Kiafrika wanakuwa vibaraka wa mabeberu na kuwasahau wananchi

Usipokunywa chang'aa una point nzuri,Leo nimekuelewa[emoji13]
 
Ahsante Mkuu....
Tujiulize who engineered all those coups?
Vipi kwa Nchi ambazo hazijaexperience mapinduzi, zina utofauti wowote na hizi zilizopitia tawala za Kijeshi?
Ukikaa vizuri utaona Kuwa nchi haziendelei sio kwa sababu ya Mapinduzi, ila kuna factor zingine pia.
 
NAKAZIA
 
Kawaida fisadi hutetewa na fisadi mwenzie😂
 
Watawala wa kiafrika bila kuwa na mfumo au kitu Cha kuwalazimisha wawatumikie wananchi wanajisahau sana, uchaguzi umeshindwa kwa sababu ni kitu Cha miaka mingi hivyo wakishaingia madarakani hawana hofu na uchaguzi Wanajua wataiba tu kura.
 
Niger kuunga au kutokuunga mkono inategemea ni kabila gani linaloshika madaraka.

Hakuna utaifa kuna ukabila.
 
Jeshi ni mali ya wananchi na always lipo sahihi.
Jeshi umtii raisi aliyepo madarakani lakin rais aliyepo madarakani asipowatii wananchi ni haki yake kupinduliwa
 
Mtaandika mpaka herufi zote ziishe.... Mtaandika magazeti na mavitabu msipoangalia na kujitafuta ndio kitawakuta hichi .... Endeleeni tu kujipakulia minyama ...si mnakula asali...wenzenu huko wanakula mnafu na mchunga .....
 
Kiongozi yeyeto asiyejali maslai ya wananchi, mapinduzi ndio jibu sahihi kwake
 
Kwa nini wananchi washangilie kipinduliwa kwake badala ya kuwa naye bega Kwa bega... !!? Waliyemchagua DOMOcratically??!
Vi vil rais anakuwa madarakani halafu anafanya vibaya kama alivyokuwa jiwe lakini utaratibu wa kumuondoa kwa kura unakuwa pale pale sio kupinduliwa
 
Huyo Rais kama wanamuona mzuri Macron amkabidhi kiti chake awaongoze pale paris
 
Mbona haujataji misri
Siku zote mifano mibaya ndo mnaitoa kuwatisha watu
 
Majirani msijisahau sana. Msijiamini sana .Maana mambo hubadilika muda wowote.
 
Kumbuka rais aliyepinduliwa aliekwa madarakani na demokrasia, sio kidikteta
Lakini baada ya kuwekwa madarakani akawageuka wananchi na kuamua kuwafurahisha mabeberu!!! Hao hao wananchi waliomchagua ndio wanafurahia yeye kupinduliwa!!! Demokrasia ni kukubaliana na matakwa ya wengi!!
 
Vi vil rais anakuwa madarakani halafu anafanya vibaya kama alivyokuwa jiwe lakini utaratibu wa kumuondoa kwa kura unakuwa pale pale sio kupinduliwa

Wewe unaamini matokeo ya uchaguzi wa kupiga kura barani Africa??

Ingekua kuna chaguzi huru na za haki basi wanajeshi wasingekua na haja za kupindua nchi.


Afrika hakuna uchaguzi huru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…