Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Wananchi wa Mkoani Njombe wamepata hati miliki za makazi kupitia Ardhi Kliniki, kwa kutumia mfumo wa kidigitali wa e-Ardhi ambapo zoezi hilo limefanyika Mtaa wa Idundilanga kwa ushirikiano wa Ofisi ya Ardhi Njombe, na Halmashauri ya Mji Njombe ikiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma za ardhi.
Wananchi wamepongeza huduma hiyo kwa kuwa imerahisisha na kuharakisha upatikanaji wa hati miliki, ambapo baadhi yao waliwasilisha maombi na kupata hati zao siku hiyo hiyo. Wamesema Ardhi Kliniki na mfumo wa e-Ardhi ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za ardhi kwa wananchi.