KERO Wananchi wa Pasiansi jijini Mwanza hatuna maji wiki mbili sasa na hakuna taarifa yoyote imetolewa

KERO Wananchi wa Pasiansi jijini Mwanza hatuna maji wiki mbili sasa na hakuna taarifa yoyote imetolewa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi wa eneo la Pasiansi jijini Mwanza wamekumbwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa takribani wiki mbili sasa, hali inayosababisha usumbufu mkubwa katika shughuli zao za kila siku.

Kinachozua malalamiko zaidi ni kwamba mamlaka husika hazikutoa taarifa yoyote kwa wananchi kabla ya huduma hiyo kukatika. Aidha, wananchi wanaofika ofisini kutafuta ufafanuzi kuhusu tatizo hilo wamekuwa wakikosa majibu ya kuridhisha kuhusu chanzo cha tatizo na lini huduma itarejea.

Tunaiomba mamlaka husika kutoa taarifa rasmi kwa wananchi kuhusu sababu za kukosekana kwa maji na hatua zinazochukuliwa kurejesha huduma hiyo kwa haraka.
 
Na mpo karibu na ziwa Victoria hakika aliyeiloga hii nchi alituweza, nawaza kama Tanzania ingekuwa jangwani kama nchi za kiarabu tungeshakufa kwa dhiki na kiu, mamlaka za maji ni mzigo kwa walipa kodi na zimefeli pakubwa
 
Back
Top Bottom