Wananchi wa tabaka la chini wazidi kuonewa na umasikini uliokithiri, huku Viongozi wakiendelea kuishi kihafahari kupitia kodi za walala hoi

Bila kichapo kutembea V8 zikawa hazipandiki hatuwezi heshimiana.


[emoji23][emoji23][emoji23] yani kinatakiwa kinuke mwanzo mwisho barabara ziwe hazipitiki ni kipigo tu. Uone kama hawajakaa kamati ya maridhiano
Na hapo ndio litakua suluhisho la kudumu
Hawatakuja kujisahau tena
 
Hakika mkuu, mimi nakula nashiba lakini naumia napoona wenzangu wana njaa najikuta machozi yanatoka lakini nashangaa aina ya viongozi wetu mbona hawana huruma, wanaendesha maV8 ikiwa watu hawana maji, chakula, vitu havishikiki wapo tu kama mazuzu.
Na wala hawajali kuhusu hilo ni ufala mno
 
Mkuu hata wewe ukiwa kiongozi huwezi kuyatimiza hayo.
Mifumo ya duniani imewekwa na watu na imewapangia watu madaraja.
Kila mtu yupo kwenye daraja lake, kulihama unatakiwa ujitume.
Mifumo tumeirithi na wala hatuielewi inavyofanta kazi.
Viongozi wengi na watu wengi wa Africa hawana uwezo wa kuyatimiza hayo unayoyalalamikia hivyo jali bisiness zako.
Kumbuka kuna watu hizo hali wanaona ni halali kwao hata ukimpa milion 10 leo kesho unamkuta vile vile.
Maana ya maisha ni tofauti kwa kila mtu, kwa hio usijitie huzuni kwa jambo ambalo huwezi kamwe kulitatua, kama unataka kutatua anza kuwasaidia hao wanaokuzungika uone impact yake.
 
mkuu toka tupate uharo 1961 hakuna unafuu we umeona leo
 
Well said bro [emoji122][emoji122][emoji122]
 
Usifananishe ulaya, marekani na Tanzania. Wenzetu rule of law inafanya kazi kwelikweli haichagui huyu ni waziri au mbunge
Na wana taasisi imara ambazo zipo fair kwa kila mtu na sio km Tanzania raisi ndie anaeamua keki ya taifa apewe nani. na wote ni mashuhuda jinsi teuzi zinavyofanyika tanzania ni full kupeana vyeo

Leo hii unaweza kuwa na nia ya kuanzisha biashara fulani hpa Tanzania na ukashindwa kufanikisha kwa sababu tu huna connection na watu wazito wa nchi

Kaka yangu alishangahangaikia kibali cha kufungua bureau de change bot kwa miaka mitatu na hakufanikiwa .hii scenerio ingekuwa tofauti km angekuwa mtoto wa kigogo.
 
Hao wanaitwa elite class ni watu wasiozidi elfu hamsini na ndio wafaidika wakuu wa keki ya taifa

Wameshika nyanja zote za uchumi na kitovu chake kikuu ni kamati kuu ya chama cha mapinduzi.

Wote hawa hawana njaa na hakuna mtoto anaetoka kwenye hii class akasoma kayumba school au akakosa ajira akimaliza chuo na huwezi kukuta wanakaa sehemu ambazo umeme na maji ni changamoto

Na wameweka vikwazo kibao kwa watu wasiotoka kwenye class yao kujikwamua kiuchumi, ndio maana ukianzisha kabiashara kadogo unakutana na lundo la tozo za vibali.

Ndio maana wengine wameamua kuwa chawa tu ilimradi waingie kwenye hiyo class, mfano halisi ni bashite amejipenyeza penyeza mpaka kaingia ndani ya system na leo inamfaidisha kwa kumlinda kwa madudu aliyofanya
 
Ukitaka kujua tabia ya mtu mpe vitu vitatu;
1.Mpe pesa
2.Mpe madaraka
3..Mpe uhuru
#Gombea uraisi kama sifa ,zina kuruhusu
 

Brother, hiyo Ulaya na America zilikuwa shit kama unavyoona au zaidi ya ilivyo Tanzania...hayo unayoyasema ni kwa sasa wamestaarabika baada ya big struggle na watu wengi kuumia na kufa...

Primitive stage wameziishi sana huko nyuma... Tanzania kwa sasa ndio iko kwenye hizo stage za uprimitive, kifupi woote tu bado ni primitive na tunaishi kigangaganga tu...

Kutoka hapa lazima upitie stages kadhaa za mateso na maumivu makali..
 
Viongozi tunaowasema humu ni ndugu zetu, wajomba zetu, shangazi zetu nk, wakija kwenye vikao vyetu vya harusi na misiba wakitoa vitita vya hela tunashangilia na kupiga vigelegele huku tukijua hizo hela ni mali za watanzania masikini....tuanze kuwakataa huku kwenye ngazi ya familia tuje kwenye ngazi ya vitongoji, wilaya na mikoa..

Unakuta kiongozi anayesifika kwa uchafu na ujinga woote huko kwao ndio anapewa uchifu na kutukuzwa na jamii yake nakuitwa mtemi...halafu leo hii tunawalaumu hao hao viongozi...

kila mtu atimize majukumu yake, popote alipo apinge ujinga, kwa kukemea, hata kuuondoa na mikono yake....tusitoe rushwa, tuwapige mawe wakija vijijini na mijini kwetu, tuwapuuze, tusiwakaribishe kwenye nyumba zetu za ibada na jamii zetu...huko makanisani na misikitini watu hawa hawa tunaowaita wezi ndio tunapokea michango yao na kuwa wafadhili wetu...na wengine tunawapokea kwenye vyama vyetu na kuwaita makamanda.....
 
Viongozi wetu naona wanazidi kungaa tu na kuongezeka mashavu

Huku sisi tukizidi kupauka.
 
System haina mwenyewe. Hata hao wakubwa walikuwa chawa tu kabla ya wao pia kushikwa mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…