Viongozi tunaowasema humu ni ndugu zetu, wajomba zetu, shangazi zetu nk, wakija kwenye vikao vyetu vya harusi na misiba wakitoa vitita vya hela tunashangilia na kupiga vigelegele huku tukijua hizo hela ni mali za watanzania masikini....tuanze kuwakataa huku kwenye ngazi ya familia tuje kwenye ngazi ya vitongoji, wilaya na mikoa..
Unakuta kiongozi anayesifika kwa uchafu na ujinga woote huko kwao ndio anapewa uchifu na kutukuzwa na jamii yake nakuitwa mtemi...halafu leo hii tunawalaumu hao hao viongozi...
kila mtu atimize majukumu yake, popote alipo apinge ujinga, kwa kukemea, hata kuuondoa na mikono yake....tusitoe rushwa, tuwapige mawe wakija vijijini na mijini kwetu, tuwapuuze, tusiwakaribishe kwenye nyumba zetu za ibada na jamii zetu...huko makanisani na misikitini watu hawa hawa tunaowaita wezi ndio tunapokea michango yao na kuwa wafadhili wetu...na wengine tunawapokea kwenye vyama vyetu na kuwaita makamanda.....