Tulijengewa tenki la maji na sehemu za mabomba ambayo maji ya kutoka kwenye tenki hilo yatakuwa yanatoka. Tenki hilo lililopo kwenye jiwe kubwa lilitupa matumaini makubwa ya kupata maji ya bomba ambayo tuliambiwa yangevutwa kutoka Mwankoko.
Hadi leo hii Desemba 2024, hatujaona maji tunaishia kunywa maji ya Kisima tu, mbaya zaidi mabomba hayo mengi yameibwa kwasababu yalionekana hayana kazi.
Mh. Mussa Sima, Mbunge wetu tunaomba uone aibu kidogo katika hili, unatusahau sana sisi huku Vijijini ambao ndio tunaoteseka zaidi na hii adha ya maji.
Majibu ya Mamlaka ~ SUWASA yafafanua hoja ya Mdau kuhusu uhaba wa maji Kata za Unyianga na Mtamaa Mkoani Singida