Wakuu Hii ni kwamba Wananchi wamefanyishwa sherehe ya kukamilika ujenzi wa kituo cha afya, wananchi ni kama wamepewa maelekezo ni cha kusema. Hii ni sehemu ya ajenda ya kumpigia kampeni ya mitano tena hakuna la maana.
=======
Wananchi wa Kata ya Mtipa, mkoani Singida, wamefanya sherehe kubwa kushukuru kukamilika kwa ujenzi wa Kituo cha Afya kilichojengwa na Serikali.
Katika kusherehekea hatua hiyo, wananchi hao wametoa zawadi ya mbuzi kwa Rais Samia kama ishara ya shukrani kwa juhudi zake za kuboresha huduma za afya, hatua inayotajwa kumaliza changamoto ya muda mrefu katika eneo hilo.
Kituo hicho kinatarajiwa kupunguza adha ya wakazi wa Mtipa na vitongoji vyake waliokuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu, hivyo kuongeza unafuu na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya vijijini.