Wananchi wafunga barabara Morogoro

Tuko

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
11,180
Reaction score
7,346
Wananchi wa Mayanga, kata ya Lubungo mpakani na kata ya Lukobe wamefunga barabara inayopita maeneo hayo leo tarehe 12 mwezi wa nane 2024 kuanzia saa mbili asubuhi. Hadi kufikia saa sita mchana hamna kiongozi aliyefika hali inayosababisha mkwamo wa vyombo mbalimbali vya usafiri....

Sababu ya kufunga barabara ni uharibifu mkubwa wa barabara unaosababishwa na kupita malori ya vifusi, barabara inachimbika, inajaa vumbi, inakuwa kero kubwa na hatarishi kwa wakazi wa maeneo hayo, huku wakipuuza maombi ya wananchi kutaka barabara hizo zitengenezwe.

Ikumbukwe kwamba malori yanayopita yanaenda kubeba kifusi kijijini humo kwa ajili ya kwenda kujengea barabara za mjini, huku maeneo hayo yakiachwa na hali mbaya
 
Inasikitisha sana yaani 2024 barabara kubwa bado ina kiwango cha kokoto.
 
Umekurupuka kuandika habari, sababu ya kufunga ni ipi
 
Andika jambo la kieleweka sio unaandika kama unawanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…