Wananchi waitilia shaka kesi kuhusu ngorongoro huko Arusha-wadai ina harufu ya kimchongomchongo

Wananchi waitilia shaka kesi kuhusu ngorongoro huko Arusha-wadai ina harufu ya kimchongomchongo

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Baada ya joto kuhusu ngorongoro kupanda, ghafla eti tunasikia eti kulikuwa na kesi mahakama kuu kule Arusha na eti mahakama hiyo imetoa hukumu kupinga amri ya serikali kufuta vijiji.

Mijadala inayoendelea ktk duru mbalimbali za wananchi, imeonyesha wananchi kuitilia shaka kesi hiyo. Wanatoa sababu zifuatazo.

1. Serikali huenda ina mpango wa kujifanya kukata rufaa mahakama ya rufaa

Wananchi wanadai kuwa huenda kesi hiyo imesukwa kimkakati na serikali yenyewe kisha hukumu kutolewa ili baadae serikali hiyohiyo ikate rufaa mahakama ya rufaa. Baada ya hapo iwakate watu kilimilimi kuwa mahakama imeamua kwa hiyo watu waheshimu amri ya mahakama.

ifahamike siyo mara ya kwanza serikali kukata rufaa ktk mahakama ya rufaa "kimkakati" na kuzuia madai ya nsingi ya wananchi ikiwemo ile kesi maarufu ya mtikila ya "mgombea binafsi"

2. Kutaka kuzuia movements na kulizungumzia hili jambo kwa hoja kuwa liko mahakamani

Wadau wanadai ni mpango wa serikali baadae kujifanya kukata rufaa mahakama ya rufaa ili ikiwa huko basi serikali ikiulizwa iseme haiwezi kuongea chochote jwa sababu kesi iko mahakamani

3. Mitandaoni wanahoji iweje kesi hiyo muhimu ya namna ile ifunguliwe gizani?
Hata wanaharakati wa kimasai wanaozungimza katika mtandao wa clubhouse wanashangaa hiyo kesi ilifunguliwaje wakati wao wako aware na kila kitu kuhusu struggle zao. Wameikataa hiyo kesi, na wanasema mtu inayedaiwa kuifungua hiyo kesi wala hana taarifa nayo.

N.B
Serikali kwenye hii ishu ya Ngorongoro imegusa pabaya. Isipokuwa makini itakuja kusababisha madhara makubwa na itajikuta watakaohusika na uonevu huo wanafikishwa kwenye mahakama za uhalifu dhidi ya binadamu. Wawe makini sana.

Inavyoonekana Wamasai hawataki kuondoka katika ardhi yao kupitia utaratibu wa mabavu ambao serikali inataka kutumia. Na wanasema wako tayari kufia ktk ardhi yao
 
Huo ndiyo ukweli.

Kesi iliwezaje kufunguliwa na mtu ambaye anakataa kuwa hakuwahi kufungua kesi? Wamasai ni vema wakaendelea kupambania haki yao kwa njia zenye kuleta tija ya kweli.
 
Huo ndiyo ukweli.

Kesi iliwezaje kufunguliwa na mtu ambaye anakataa kuwa hakuwahi kufungua kesi? Wamasai ni vema wakaendelea kupambania haki yao kwa njia zenye kuleta tija ya kweli.

Mchezo wao umestukiwa.

Wanataka kufanya delay tactic kupitia kufungua shauri mahakama ya rufaa ili kupoza joto then waitumie mahakama kuhalalisha maamuuzi yao yaliyokinyume cha sheria.

Umma umewastukia!
 
Huo ndiyo ukweli.

Kesi iliwezaje kufunguliwa na mtu ambaye anakataa kuwa hakuwahi kufungua kesi? Wamasai ni vema wakaendelea kupambania haki yao kwa njia zenye kuleta tija ya kweli.
Kesi inafunguliwa ndani ya masaa 12, inasikilizwa na hukumu inatoka ndani ya muda huo huo!
 
Kwa suala LA Ngorongoro, Wamasai watatoka tyuu watake wasitakee.
Hii nchi ina wenyewee, Lol
 
Back
Top Bottom