Wananchi wajitolea kukarabati Barabara inayounganisha Kata ya Kandawale na Njinjo wilayani Kilwa

Wananchi wajitolea kukarabati Barabara inayounganisha Kata ya Kandawale na Njinjo wilayani Kilwa

Kilwa94

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
2,747
Reaction score
3,183
Hii ni barabara inayounganisha Kata ya Kandawale na Njinjo na kuelekea Kilwa-masoko(wilayani).

Barabara hii inahudumiwa na TARURA lakini kwenye uhalisia haipati huduma ya kuboreshwa miaka 10's sasa mbali na mchango mkubwa wa mapato tunaochangia wananchi wa kata hii kupitia mazao tunayolima kama vile ufuta, nazi, korosho.. n. K

Kitendo cha kutoboreshwa kwa barabara hii inafanya tupate wakati mgumu hasa katika kipindi hichi cha mavuno tunashindwa kabisa kuleta magari ya kusafirisha mazao na kupeleka sokoni.

Hali hiyo imetusukuma tutumie njia asilia kukarabati kwa kutumia nyenzo asilia: Majembe, sururu, koleo na mapanga.

Mara kadhaa tumejaribu kulisema hili tatizo la miundombinu lakini cha ajabu hakuna hatua inayochukuliwa. Mbunge anayemaliza muda wake Fransis Ndulane(kilwa kask) mara kadhaa naye tumemfikishia kero hii ila cha ajabu aliishia kutuaminisha tu kwamba itajengwa huku akiambatanisha na nakala za bajeti iliyotengwa kwaajili ya barabara hii Kwa bajeti za miaka 3 mfululizo ameishia kufanya hivyo lakini hakuna mabaresho yoyote yaliyofanyika.

Hali hii imetufanya sasa tutumie nguvu kazi tuliyonayo kukarabati barabara hii ili gari iweze kufika, kuchukua mazao ambayo tunanuia kuyafikisha ghalani(sokoni).

Rai:
Tunaomba sana serikali ione umuhimu wa kuboresha barabara hii kwani mbali na kutumika kwa shughuli za kibiashara, pia ni njia tunayopita kwenda kupata huduma za afya, utawala, polisi n. K, huko Kilwa-Masoko(wilayani).

mode2 Moderator naomba mutupazie sauti kwani hii ni kero kubwa kwetu raia wa maeneo haya. Aidha naomba nisaidieni kuhariri kichwa cha habari.

IMG-20250630-WA0112.jpg
 
Mkuu umenikumbusha 2022 Niliwahi kupita hiyo barabara na bodaboda sitasahau kiatu changu kilizama mtoni ulikuwa msimu wa mvua nikavivua ili nivuke mto kwanza na pikipiki tuliibeba.. Itoshe kusema hilo ni pori siyo barabara.. Wakati wa kurudi nilikula boda kutokea darajani Nasaya mpaka njia nne...
 
Back
Top Bottom