Wananchi wa Jimbo la Sengerema kata ya KISHINDA Kijiji cha TUNYENYE wamekaidi agizo la Mheshimiwa Mbunge wao Ndugu Hamis Tabasamu Mwagao kubomoa Nyumba zao kwa hiari.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa,kuna upanuzi wa barabara inayoendelezwa na (TANROADS)ambayo ilikuwa chini ya TARURA. Hivyo Mbunge alifika kijinini hapo mnamo tarehe 31-12-2023, na kuanza kuweka alama ya ( x ) kwenye majengo na baadhi ya Fremu za biashara kijijini hapo. Jambo ambalo lilileta taharuki miongoni mwa wananchi ambao ni wamiliki wa majengo hayo.
Kwa upande wa wananchi wao wanachodai ni kulipwa fidia ilimradi wapishe mradi huo na wala si kupinga maendeleo kwani wanaona juhudi Za Rais Samia Katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Mbunge huyo akiwa Katika ziara ya kikazi alipita kijijini hapo,ndipo mwenyekiti wa Kijiji hicho alipata nafasi ya kumuuliza kuhusu taharuki hiyo na Mheshimiwa Mbunge alinukuliwa akisema kuwa "Wananchi hamtalipwa fidia kwani hii ni miradi ya Maendeleo,hivyo mnatakiwa mbomoe Nyumba zenu kwa hiari tofauti na hivyo tutabomoa kwa kutumia Greda/Skaveta na gharama juu.