Mpepetaji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 346
- 213
Wananchi wa Kata ya Katesh, wilayani Hanang, mkoani Manyara, wamelalamikia kutoshirikishwa katika kuibua na kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ya elimu na afya hivyo kushindwa kusimamia uwajibikaji na kulinda miundombinu ya miradi hiyo inayogharimu mamilioni ya fedha za umma. Wananchi hao wametoa malalamiko yao katika mkutano wa wananchi na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.