Wananchi walia na ujenzi wa Daraja Kijiji cha Komdudu (Tanga), wadai wanateseka kwa muda wa miaka miwili

Wananchi walia na ujenzi wa Daraja Kijiji cha Komdudu (Tanga), wadai wanateseka kwa muda wa miaka miwili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Wananchi wa Kijiji cha Komdudu Wilayani Handeni Mkoani Tanga wamelalamikia kukumbana na changamoto ya kuvuka kwenye daraja lililopo kijijini hapo kwa muda wa miaka miwili tangu lilipoharibika.

Daraja hilo halijatengenezwa bali limeweka la muda hali ambayo imekuwa ikiwapa changamoto Wananchi wengi ambao wanalazimia kupita chini ya daraja pindi wanapokuwa na mizigo mizito huku vyombo vya usafiri navyo vikishindwa kupita katika njia hiyo.

Wananchi wameomba Serikali ichukuwe taadhari kabla ya Mvua kubwa El Nino azijaanza,

Daraja hilo muhimu kwa wakazi wa Handeni linalounganisha Wananchi wa maeneo ya Kabuku, Kwadkwazu, Sindeni na maeneo mengine lina zaidi ya Mwaka mmoja na nusu toka liharibike na TARURA kuchukuwa hatua ya kujenga Daraja la Mpito ambalo kwa kiasi kikubwa upitisha watu wanaotembea kwa miguu, kwa kiasi kikubwa Wananchi wanaotegemea daraja hilo kupitisha wagonja au Mazao kwa gari ni ngumu, mawasiliano yamekatika baina ya Vijiji Kwa vijiji.
 
Ona tulivyo mazuzu. Eti wanaomba. Ni kuitaka serikali iwape huduma hiyo!
 
Back
Top Bottom