Uchaguzi 2020 Wananchi wamkataa Diwani na Mbunge mbele ya Rais Magufuli kata ya kiloleni Busega

JPM Nimeona kachukia kwelikweli mpaka akaanza kuwatisha kuwa sileti barabara!
Sisi ndio waajiri wake,kila kinachofanyika sio msaada wala ombi ni jambo la lazima,wanakata kodi kila kitu,kwenye mishahara ndio usiseme.Halafu unatishi upeleki barabara badala ya kulitafutia utatuzi (hapo amefail sana).Shida Tz hakuna vyama vya siasa vya upinzani vyenye misimamo,wamejaa "wasaka tonge" wacha sisiemu waendelee kuongoza.
 
Chegeni na Masele wanamhujumu Magufuli.Anyway subiri uchaguzi uishe kitaeleweka
 
Mwache asomweshwe namba na yeye,ahahaha
 
Leo hii ahadi ya kujengewa barabara ndio imekuwa silaha ya kutisha wananchi waipe kura CCM kwa lazima!
Hizo ni akili za kiuwendawazimu kwa 100%.

Kweli Magufuli amechoka na kuchokwa vibaya.
 
Mzee wa maendeleo ya vitu siyo watu anaanguka vibaya, barabara ndo Nini? Watu wanataka unafuu wa maisha,

Huku dar es.. city center Kuna barabara nyingi hazijajengwa Ni vumbi tu. Sembuse huko mikoani wilayani
 
Hawajapotezwa hao wananchi?? JPM hana uvumilivu wa kisiasa,,ukitofautiana kimtazamo,anafunga kisasi/uadui. Hiyo kamata kamata inayokuja hapoo, kuna viumbe watapotea pasipojulikana
 
Watu mtaani hawaongei sana,,hasa watumishi wakiwemo polisi/jeshi...hasa maeneo waliyopitishwa CCM bila ushindani. Kampeni za lissu zinafuatiliwa kwenye mitandao,tena kwa siri. Nimewakuta vijana sehemu wanafuatilia nyomi la jana....lissu mbeya,,wakimwona mgeni wanaondoka... CCM hali si shwari,tena huko ndani kwao
 
JPM Nimeona kachukia kwelikweli mpaka akaanza kuwatisha kuwa sileti barabara!
Wananchi wamemcheka tu kwa kuwa hata Yeye atakuwa Raia wa Kawaida tu kuanzia 28th October
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…