Uchaguzi 2020 Wananchi wamkataa Diwani na Mbunge mbele ya Rais Magufuli kata ya kiloleni Busega

Uchaguzi 2020 Wananchi wamkataa Diwani na Mbunge mbele ya Rais Magufuli kata ya kiloleni Busega

JPM Nimeona kachukia kwelikweli mpaka akaanza kuwatisha kuwa sileti barabara!
Kampeni za kishamba hizo. Unapangia watu kiongozi wao halafu unatishia kuwa huleti barabara hiyo si sawaa. Akiambiwa dikteta uchwara anakamata watu..
 
Hao wananchi lazima wakamatwe wawekwe ndani.
 
Wajumbe tunaendelea kuwakataa wote Waliopita kimazaBe
Nalog off
 
Hapa ndipo rais anapokosa busara. Barabara si hisani.. kwamba yeye anatoa zawadi. Ni jukum lake.
Hii mambo ya kufanya huduma ni za hisani wkt watoa kodi ni watanzania. Ni upumbavu
Tatizo siyo JPM. Ni katiba yetu ndiyo inayompa kiburi hivyo. Nyerere alisema kuwa kwa katiba hii tutakuja kupata rais dictator.
 
Bado usishangae mwisho wa siku ukasikia huyo aliyezomewa akitangazwa kushinda kwa kishindo!!
Japo kwa sasa tunaona na kitu cha kawaida, lkn amini, wahusika hukosa FURAHA na Amani ktk maisha yao japo hujisifia wakifanikisha
 
Mkuu mbona sentesi yako imekataa tamaa na INA hisia za kulipiza? Sio vizuri. Tupunguze hisia mbaya kwa wenzetu. Tuwe pamoja
Chegeni na Masele wanamhujumu Magufuli.Anyway subiri uchaguzi uishe kitaeleweka
 
Hajawatisha amewaeleza ukweli!
Mkuu acha utani, kuna kutishwa zaidi ya kule tulipo ona leo. Kama mnadanganyana huko kwenu sawa. Muulize Mzee Mgaya atakufahamisha vizuri. Leo mbona hujaweka kile kibwagizio chetu "Maendeleo hayana chama". Ni wazi JPM ni mzee wa alinacha na inasikitisha kusema ni mwongo pia kwenye hili.
 
Maendeleo hayana vyama bwashee!
 
Rais Magufuli akiwa anaelekea Mwanza amewashawishi wananchi wamchague diwani wa ccm na Mbunge wa ccm lakini wananchi hao wamezomea na kukataa mbele ya Rais Magufuli

Wananchi hao wa kata ya kiloleni jimbo la Busega ambalo mgombea wao pendwa Bwana chegeni amekatwa jina lake wakati aliongoza kura za maoni wamekasirika mbele ya Rais kwa kuzomea

Mwananchi mmoja ameomba kuelezea tatizo ,Mwananchi huyo wa ccm amesema mbunge na diwani wa ccm bwana Magoti hawafai

Rais amesisituza wakichagua mgombea mungine watajuta

Akitumia kilugha ambacho mimi sikuelewa ni lugha gani akiweka msisitizo,Aidha lugha hiyo ya utamaduni bado haikusaidia zomea zomea hiyo

Muda huu yupo live TBC saa tano

Wananchi wameweka ngumu na Rais anasema hatapeleka lami

Wananchi wanamjibu hatumtaki wala hatumchagui Bwana Magoti diwani

Kazi kazi kweli kweli
Kumbe sehemu ambazo hawachagui chama tawala hawapati maendeleo
nilidhani serikali ipo kwa ajili ya wananchi wote
 
Aisee comrade fanyeni kikao cha dharura mumpange upya Mzee Pombe maana tangu mkutano Shinyanga ametoka nje ya mstari amekua ni mtu wa jabza na vitisho kwa wapiga kura 🤣🤣🤣
Na badooooo! Ngoja aende kule kwenye koro-show! Naamini kesho atakuwa kwa Nshomile wakamhoji kuhusu tetemeko! Mwaka huu mpaka apasuke! Ila niwatahadharishe Watanzania wenzangu, tufanye kila linalowezekana kumzuia huyu mzee kwenda Ikulu tena maana ukatili atakaotutendea hauna mfano tukizingatia kwamba uchaguzi ujao wa 2025 hana cha kupoteza!
 
Hivi mnafikiri Magufuli akipita 2025 kuna uchaguzi na hao akina Ndugai wake? Katiba itahaririwa ovyoovyo, haitokuwa na tofauti na gazeti la tanzanite.

Mwaka rasmi wa mabadiliko ni huu, tukifeli hakuna rangi tutaacha kuiona kwa miaka kibao tu, si mitano tu!
 
maendeleo hayana vyama, hapohapo mkichagua upinzani sileti lami.
Nchi ya Amani huku analeta Jeshi la Akiba.Mzee amejaa gas,anatema moto.Hizi ndiyo Sera mlizotuahidi?
Kosa lingine kubwa walilofanya ni kuchapa ilani(Volume), kama vile vitabu vidogo(Booklets)walishindwa kuzisoma na kuzielewa,itakuwaje kwa hiyo ya sasa?Kweli CCM Mpya imepoteza dira na mwelekeo.Mara shida ya barabara,huku Maji,Kule umeme na watumishi wanaulizia mishahara.Wataacha kuchanganyikiwa?Wanadhani maisha yanasimama kupisha reli,Stigler's ama flyovers?
 
Back
Top Bottom