Wananchi, Wanafunzi na Zimamoto washirikiana kuzima moto Mlima Kilimanjaro

Wananchi, Wanafunzi na Zimamoto washirikiana kuzima moto Mlima Kilimanjaro

Moto unazimwa na wataalamu sio wanafunzi kati ya ajali mbaya za Moto ni pamoja na Moto wa msituni msipojua kitu mtazungukwa na kuteketea moto wa California wiki iliyopita uliwazunguka fire fighter kadhaa mlima unaingiza pesa nyingi kuweni na vifaa thabiti vya kuzimia Moto wa maporini na mlimani acheni ujanja ujanja kwenye Mambo ya msingi, watu wa Moto mkoa KLM na Arusha wahusike kuzima Moto sio hao wanafunzi.
Kusaidia kuzima nafikiri kuna kazi nyingi ,kuwachotea,maji,kuwapa chakula ,watu fire,ndo maana wakati wa Vita na Uganda ,mpaka bend zilienda ,japokua hawakupigana,wao ilikua kutoa burudani,kuwapa moyo wanajeshi
 
Watu wengi tuliokua tunafanya kazi za Moto hasa wa meli,oil lig au majumbani wataalamu walitusihi kwenda kuzima Moto wa msituni ni hatari kuliko maelezo inatakiwa upate Elimu ya kuanzisha Moto ili ubadili uelekeo na jinsi upepo ilivyo sio umewashinda hamuwezi hata hii mbinu ndogo sema huku wanachukulia poa tuu kila kitu tunawaangalia maana maamuzi ya kitaalamu yanategemea wanasiasa..
Wao wanadhani kuzima huo moto unabeba maji kwenye beseni na kwenda kuumwaga tu.

Kuzima moto ni taaluma sio kila mtu anaiweza.
 
Moto unazimwa na wataalamu sio wanafunzi kati ya ajali mbaya za Moto ni pamoja na Moto wa msituni msipojua kitu mtazungukwa na kuteketea moto wa California wiki iliyopita uliwazunguka fire fighter kadhaa mlima unaingiza pesa nyingi kuweni na vifaa thabiti vya kuzimia Moto wa maporini na mlimani acheni ujanja ujanja kwenye Mambo ya msingi, watu wa Moto mkoa KLM na Arusha wahusike kuzima Moto sio hao wanafunzi.
Nakumbuka nilipokuwa nasoma Dakawa High School tulikuwa tunaenda kuzima moto kwenye mapori yaliyomo DADECE!
 
1602504356988.png

Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) imesema inaendelea kuchunguza chanzo cha kuzuka kwa moto katika Mlima Kilimanjaro huku jitihada za kudhibiti moto huo zikiendelea.

Moto huo ulizuka Jumapili Oktoba 11, 2020 katika eneo la Whona ambacho ni kituo cha kupumzikia wageni wanaotumia njia ya Mandara na Horombo kupanda mlima huo mrefu kuliko yote Afrika.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete katika taarifa yake amesema moto huo unaendelea kudhibitiwa na vikosi vinavyoshiriki zoezi hilo.

Vikosi vinavyoshiriki kuzima moto huo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shelutete Oktoba 12, 2020, vinajumuisha wananchi, wanafunzi kwa vitendo na wale wa Mweka (Chuo cha wanyamapori) na Kikosi cha Zimamoto.

“Taarifa zaidi kuhusu chanzo zinaendelea kufanyiwa kazi,” amesema Shelutete.

Hata hivyo, Tanapa imesema inachukua tahadhari zote ili kuhakikisha usalama wa wageni na vifaa vyao unaimarika bila kuathiri shughuli za utalii ambazo zinaendelea kama kawaida hususan njia ya Marangu iliyoathirika na moto husika.

Mlima huo wenye urefu wa mita 5,895 (futi 19,340) ni sehemu ya hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. Hifadhi hiyo ina ukubwa wa kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini.

Mlima huo unaopatikana katika mkoa wa Kilimanjaro ni moja kati ya milima ambayo kilele chake hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka kila pande za dunia.

Mamlaka zinaeleza kuwa wastani wa watu 50,000 hupanda mlima huo kila mwaka.
 
Wa Tanzania zaidi ya million 60, Ninaamini Kuna wenye mamlaka wenye uwezo wa kushauri namna ya kuudhibiti moto huu.

Kuna namna tunaweza omba msaada/ushauri kwa wazoefu wa janga kama hili.

Ninajua Sina uzoefu. Lakini kama helkopta za kawaida zipo.

Weka pipa la maji ya kuzimia moto. Weka na water pump, then zitumike hata namna hiyo.

Nimeongea locally, najua Kuna namna wana deal nao, utazima tu

Kuudhiti ni muhimu, kama sio lazima.

Kwa maoni yako mdau, unadhani wapi tumekwama?
Na ni nini kifanyike?
 
Ni aibu sana na dunia nzima inatushangaa.

Mlima Kilimanjaro ni kitovu cha utalii ktk nchi yetu, lkn limetokea janga la moto mlimnani hapo kuuzima imekuwa ni full vituko na vioja.

Nimeona wazima moto wakitumia fimbo na chupa za maji ili kuuzima moto unapendelea kwa kasi kuharibu uoto wa asili wa mlima huu mrefu zaidi barani Afrika.

View attachment 1599205
Leo ni siku ya tano hakuna la maana linalofanyika. Serikali kupitia waziri wake wa utalii ilichokifanya kikubwa zaidi ni ku-tweet tu.
 
Waziri mstaafu wa mambo ya ndani alitaka kununua vifaa vya kisasa vya kuzimia moto ...mr mjuaji akamtumbua akidai ni ufisadi na vichwa maji wakaona mr haambiliki ni shujaa kwerikweri
 
Sipati picha nyoka na viumbe wengine wakiwa wanajihami kwa kukimbia mbele zaidi kutoka eneo la tukio la Moto...wale wazimaji sijui itakuaje
 
Back
Top Bottom