Mimi ni mmoja niliyevutiwa na falsafa ya 4R alizoziasisi Rais Samia. Na kwa vyama vya siasa, viongozi wa dini, mashirika ya nchi za nje, mabalozi na wananchi walianza kumwelewa na kuamini kuwa safari nchi itaonja nuru ya uchaguzi ulio huru na haki ili wananchi wachague wanachokitaka.
Baada ya kuruhusiwa mikutano watu wakaamini zaidi kwenye ajenda hii ya 4R ambayo ninahisi ni sifa muhimu iliyomuwezesha Rais kupewa digrii za heshima nyingi duniani kote. Hali imeanza kubadilika kidogo kidogo kuelekea uchaguzi kuna dalili uchaguzi huu wa 2024/25 ukachukua sura na mkondo kama wa mwaka 2019/2020. Hii itakuwa mbaya sana, ACT wamekwisha onja adha ya maovu ya uchaguzi mdogo maeneo mbalimbali. Na wametoa angalizo.
Swali fikirishi, je itakuwaje iwapo hali ya mwaka 2019/2020 ya uchafuzi itajirudia kwenye uchaguzi huu! Kuenguliwa mawakala kunyanyaswa, na kutangazwa matokeo tofauti. Wananchi tutaipokeaje hiyo hali. Nashauri Rais atoe hotuba ya msisitizo wa kufuata sheria kwa vyombo vyote vya dola vya kiuchaguzi, na watendaji walio chini yake ifuatiwa na Waraka wa Tume ya uchaguzi au wa kiutumishi kutoka Ikulu, pia Wakatoliki, Bakwata, CCT nk wawaelekeze wafuasi wao.
Vinginevyo ikiachwa hali itokee kama wakati ule, Tanzania itaingia kwenye giza nene la demokrasia. Tujadili.