Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WANANCHI WANAOZUNGUKA UWANJA WA NDEGE WA KIA WATAKIWA KUWA NA SUBIRA YA MALIPO YAO
Serikali imewataka wananchi wanaozunguka uwanja wa ndege wa KIA kuwa na subra wakati wanasubiri malipo ya fidia ya maeneo yao kwani tayari imeshafanya tathmini na uthamini kwasasa wapo katika hatua za mwisho za utekelezaji wa adhima hiyo.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete kufuatia swali la Kimkakati la Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Elinikyo Mafuwe June 20, 2023 bungeni jijini Dodoma la kutaka kujua lini zoezi la kulipa fidia kwa wananchi wanaozunguka uwanja huo litaanza ambapo ameuliza kuwa
“Wananchi wanaozunguka uwanja wa Ndege wa KIA wamekwisha kufanyiwa tathmini baadhi ya maeneo ambayo yanapaswa kupisha uwanja huo Je? ni lini Serikali itaanza kulipa wananchi hawa fidia?” Mhe. Mafuwe
“Serikali imeshafanya tathmini na uthamini, kinachoendelea sasa tumeshapeleka daftari kwa mthamini Mkuu wa serikali tayari kwaajili ya malipo na kwenda kulipeleka hazina hivyo niwaombe wananchi wawe watulivu wakati wanasubiri malipo yao” Mhe. Mwakibete