kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Uwindaji wa Kitalii Wanufaisha Nchi, Billioni 9.6 zatolewa Kwa Halmashauri na Vijiji Pembezoni mwa Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu - Kamishna Mabula
Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi Nyanda amesema shughuli za Uwindaji wa Kitalii zinazofanywa katika Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu yanayosimamiwa na TAWA Nchini, zina manufaa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Nchi na mwananchi mmoja mmoja hususan wale waishio pembezoni mwa Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu.
Kamishna Mabula amesema Serikali kupitia TAWA Tshs. Billioni 9.6 Kwa Halmashauri na Vijiji wanufaika wanaoishi pembezoni mwa Mapori ya Akiba na Mapori Tengefu Nchini ikiwa ni fedha zitokanazo na asilimia 25 ya ada ya Wanyamapori waliowindwa pamoja na Utalii wa picha katika kipindi cha kuanzia Aprili 2022 Mpaka Desemba 2022.