KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Tume ya maboresho ya mfumo wa haki jinai ikiwa imemaliza kazi yake na ripoti yake kuwasilishwa Kwa Mhe. Rais Kwa hakika mapendekezo yake kama yakifanyiwa kazi, mfumo wa upatikanaji wa haki Tanzania utaboreka na kuimarika. Na niseme kwamba maboresho hayo ni sawa na kuifumua katiba iliyopo na pengine hakutakuwa na haja tena ya kuwepo Kwa mchakato mpya KATIBA MPYA Kwa sasa. Mchakato wa katiba MPYA utakuwa umemalizika bila uwepo wa gharama kubwa Kwa serikali.
Mbali na yote yaliyotolewa kama mapendekezo na tume, Kuna baadhi ya mapendekezo yatakuwa ni hatari Kwa usalama na amani Kwa Taifa.
Pendekezo la kufutwa Kwa adhabu ya kifo litakuwa na athari kubwa sana Kwa baadaye maana litatumiwa Kwa nia ovu. Kwa Sasa, utulivu na amani iliyopo Kwa kiasi kikubwa inachochewa Kwa uwepo wa adhabu hii hata kama utekelezaji wa adhabu hii ni mgumu.
Tuchukulie Kwa upande wa uhaini, ugaidi na majaribio ya kupindua serikali, Kwa hakika ni matendo hatari Kwa usalama wa Taifa. Leo hii, wanaowaza kufanya mambo hayo wanahofia uwepo wa adhabu ya kifo na kufanya kushindwa kutekeleza mipango yao. Amani inaendelea kutamalaki.
Kwa mtazamo wangu, kubadilisha adhabu ya kifo kwenda kifungo Cha maisha au kuondoa adhabu ya kifo ni jambo linalotakiwa kuangaliwa Kwa upana mkubwa Kwa amani na usalama wa Taifa. Mtu akiona akifanya uhaini, ugaidi au jaribio la kupindua serikali atafungwa tu hilo litampa ujasiri mkubwa sana wa kutekeleza jambo hilo bila hofu.
Haya ndio ninayofikiria juu ya pendekezo hilo la tume ya maboresho hayo ya mfumo wa haki jinai na ni utangulizi wa mada yangu.
Wakati akipokea ripoti ya tume hiyo, Mhe.Rais alitoa agizo lifuatalo, nanukuu ' Itungwe sheria kwa viongozi wanaoingia kwenye maeneo ambayo sio yao washughulikiwe'. Niseme ni agizo lenye nia njema lakini Kwa mtazamo wangu Sheria tu haitoshi bali nani atakuwa ni mtekelezaji na mfuatiliaji mkuu wa Sheria hiyo ndio jambo la msingi.
Kwa kuwa ripoti hiyo imewataja viongozi wa kisiasa Kwa kuingilia majukumu yasiyo yao, nina mapendekezo yafuatayo katika kukazia agizo alilotoa Mhe.Rais:
Kwa kuwa viongozi wa kisiasa, wengi wao wanatokana na maamuzi ya wananchi Kwa maana wanachaguliwa na wananchi basi itoshe kusema wananchi ndio wahusishwe kwenye utekelezaji wa Sheria hiyo.
Mwananchi yeyote ambaye ametimiza umri wa kupiga kura, Kwa Sheria hiyo itakayoundwa apewe mamlaka ya kufungua mashtaka mahakamani pale anapoona kiongozi ameingilia majukumu yasiyo yake.
Mwananchi yeyote atakayeona kiongozi katumia Sheria vibaya apewe mamlaka ya kumshtaki kiongozi huyo bila kujalisha cheo, wadhifa au mamlaka yake. Hapa nazungumzia maRC na maDC ambao ndio wanaonekana kutumia vibaya Sheria ya kuweka ndani watu masaa 48, aliyewekwa ndani aweze kumshtaki kiongozi husika kama akiona hakutendewa haki.
Mwananchi anapomfungulia mashtaka kiongozi na mahakama ikathibitisha ni mashtaka ya kisheria kweli na yanatakiwa kujibiwa na mhusika basi Sheria iseme kwamba kuanzia Muda huo mshtakiwa Kwa mamlaka ya Sheria atakuwa kiongozi Tena. Hapa Sheria itoe mamlaka ya waliovunja sheria kushtakiwa kama wahalifu na sio kama viongozi.
Lengo kuu la kutaka mwananchi kuwa ndie mtekelezaji wa sheria hiyo ni Kwa sababu maamuzi mengi ya viongozi yanawagharimu wao Moja Kwa Moja hivyo wakiwa watekelezaji wa sheria Moja Kwa Moja itapendeza sana.
Pia, itafanya viongozi kuwaheshimu wananchi na wananchi kupewa nafasi ya juu ya maamuzi. Na hii itasaidia utekelezaji wa Sheria kuwa wa ufanisi zaidi.