Wananchi wapinga sheria kibali cha sherehe Moshi

Wananchi wapinga sheria kibali cha sherehe Moshi

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Kufuatia Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kutoa tangazo la kulipia matukio ya sherehe na kisha tangazo hilo kusitishwa kwa muda, mjadala umekuwa mkubwa baada ya wananchi nao kupinga sheria hiyo wanayodai ni kandamizi.

Akizungumza na Jambo TV Frank Maro mkazi wa Moshi ameeleza kuwa sheria hiyo ni kandamizi kutokana na wamiliki wa kumbi za sherehe,washereheshaji na wadau wengine waliotajwa katika sheria hiyo wanalipa kodi stahiki.

"Hiyo sheria ndogo iliyoanzishwa ya utozaji wa fedha za vibali vya kufanya sherehe katika kumbi ambazo zina leseni za halmashauri, zina usajili @BasataTanzania na zinalipa kodi ya mapato Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni ajabu kwani mwananchi anayeenda kutumia huduma ya mfanyabiashara mwenye leseni ya halmashauri na amekidhi matakwa ya sheria kutakiwa kuwa na kibali ili apate huduma yake ni chanzo kilichobuniwa lakini kinapoteza sifa ya usawa na ukandamizaji" Maro

Kwa upande wake mshereheshaji wa shughuli mbalimbali ambaye hakutaka kutaja jina lake ameeleza kuwa sheria hiyo inakandamiza upatikanaji wa ajira kwa makundi mengine na kufanya utegemezi uzidi kuwepo.

"Kwakuwa kumbi za sherehe zina kibali na washereheshaji wanatambulika hiyo sheria iondolewe inatangeneza chuki kwa wananchi hao madiwani wawaze sheria nyingine ili kulinda ajira za watu waliojiajiri ili kuepuka kuwa tegemezi,ukiona sherehe ya mtu imekamilika ufahamu watu wengi wamepata ajira hapo" alisema

Kupitia kikao cha madiwani wa halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro, limesimamisha kwa muda utozwaji wa kodi katika shughuli za sherehe mpaka hapo wananchi watakapopewa elimu ya kutosha ili kuondoa malalamiko.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Morris Makoi ambapo alisema kuwa wamelazimika kusimamisha sheria ndogo hiyo namba 39 ya mwaka 2024 baada ya kusikiliza maoni ya wananchi kuwa jambo hilo ni geni kwao.
 
Back
Top Bottom