Marry Mdaki
Member
- Aug 26, 2022
- 25
- 23
Utangulizi
Utayari ni hali ya kuafiki au kukubali jambo fulani. Hivi sasa kumekuwa na mikanganyiko ya aina mbalimbali baina ya nchi na watu wake, huku ikionekana kuwapo kwa upinzani kutoka kwa wananchi juu ya masuala mbalimbali yahusuyo uendeshaji wa nchi kwa ujumla.
Mpaka sasa ni dhahiri kuwa kuna baadhi ya sekta ambazo zimepokea upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wake huku ikionekana kuwa kila mmoja yuko sahihi kwa upande wake juu ya imani na mtazamo wake juu ya masuala hayo.
Kabla sijaelezea dhamira ya uzi huu, ningependa tujikumbushe kwa kifupi tu kuhusiana na baadhi ya mambo kadha wa kadha ambayo ni dhahiri kuwa yameacha fumbo kwa wananchi hata kwa mamlaka husika pia.
Kwa kuanza na suala linalohusu tozo ni dhahiri kuwa limepokea ukinzani wa hali ya juu kutoka kwa wananchi ambapo wengi wametoa malamiko mbalimbali juu ya suala hilo huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kuona kuwa wanaonewa na kukandamizwa.
Picha; kutoka mtandaoni ikionesha baadhi ya mapendekezo juu ya tozo za miala ya kibenki.
Pia, siku za nyuma kulizuka baadhi ya mgongano baina ya sekta ya nishati nchini dhidi ya wananchi wake juu ya masuala mbalimbali kuhusu ongezeko la gharama ya upatikanaji wa nishati ya umeme pamoja na nishati ya gesi kutoka gharama zilizotumika awali.
Sambamba na yote kumekuwapo kwa migogoro baina ya mamlaka inayohusika udhibiti wa upatikanaji wa bidhaa mbalimbali nchini dhidi ya wananchi wake huku wengi wakionesha kutokuwepo kwa sababu za msingi juu ya upandaji wa gharama hizo. Rejea malalamiko ya wananchi juu ya mfumuko wa bei za mafuta, vyakula kama vile nafaka, sukari n.k
Suala lingine ni kuhusiana na uzinduzi wa kaulimbiu thabiti ya filamu ya utalii iliyoongozwa na raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Samia Hassani iliyojulikana kama "Royal tour". Jambo hili lilipokelewa tofauti na baadhi ya wananchi huku wengi wao wakiamini kuwa imekwenda kuleta hasara zaidi kuliko faida itakayopatikana.
Haya ni baadhi ya masuala kati ya masuala mengi yaliyoleta mikanganyiko kwa wananchi dhidi ya mamlaka husika huku ikionekana kukosekana kwa taarifa muhimu juu ya masuala hayo.
Je! Ni kweli kuwa wananchi hawako tayari juu ya masuala mbalimbali yatolewayo na mamlaka mbalimbali?
Ukweli ni kuwa si kila mtu anayepinga jambo fulani ni dhahiri kuwa halipendi jambo hilo la hasha bali wengi wao hupinga ili wapate sababu au waelewe kiundani juu ya jambo hilo. Yapo masuala mbalimbali ambayo yaliwahi kupokea upinzani kutoka kwa wananchi lakini mwishowe yalikuja kuonekana na kupendwa zaidi na wananchi.
Mfano dhahiri unaweza kuonekana hata kipindi miradi kama vile reli ya kisasa (standard gage), mradi wa bwawa kubwa kwa ajili ya nishati ya umeme. Miradi hii ilipoanzishwa ni dhahiri kuwa ilipokea upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya watu mbalimbali huku wengi wakidai kuwa inatumia pesa nyingi hivyo itaingiza nchi katika madeni makubwa na miradi mingine mingi iliyoanzishwa kipindi hicho, lakini kutokana na ufafanuzi wa kina juu ya manufaa ambayo yangeweza kupatikana baada ya kukamilika kwa miradi hiyo kiasi kwamba wengi wao waliokuwa wakipinga waliishia kuafikiana sambamba na usimamizi thabiti uliokuwa ukifanyika ulivuta imani ya watu wengi na kuwafanya waamini manufaa hayo ya baadaye.
Je! Ni kipi kifanyike zaidi?
Ipo haja au umuhimu wa kuwepo kwa jukwaa la kitaifa litakalotoa elimu pamoja na mrejesho juu ya shughuli zinazoanzishwa na mamlaka mbalimbali. Ni wakati thabiti wa serikali kuimarisha taarifa kwa wananchi wake kabla hakijafika kipindi ambacho kutakuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Ni dhahiri kuwa endapo wananchi watapewa taarifa kamili na maelezo juu ya uanzishwaji wa shughuli fulani ambayo itahusisha wananchi moja kwa moja basi ni dhahiri kuwa itaweza kufungua fikra za watu na kupunguza baadhi ya maswali ambayo baadhi yao ndio yamekuwa silaha kuu katika upinzani.
Pia serikali kupitia mamlaka zake husika ingeongeza jopo la wataalamu watakaohusika kufanya uchakataji wa mawazo mbalimbali yenye kuleta manufaa kwa wananchi juu ya uanzishwaji wa shughuli mbalimbali. Hivyo basi ni wakati thabiti wa serikali kuhusisha watu wenye ubobevu juu ya masuala mbalimbali kama vile watu waliobobea katika masuala ya uchumi, siasa n.k. hii itasaidia katika kuweka uwiano wa watu wanaotumikia idara husika. Mfano huwezi mtumia mtu aliyebobea katika mambo ya afya katika idara ya mauzo na manunuzi ya nchi kwani ni taaluma mbili tofauti.
Pia, ni wakati sahihi wa serikali kupitia mamlaka zake husika kuongeza jitihada katika usimamizi wa miradi mbalimbali inayoanzishwa ili kutia chachu kwa wananchi kwa kuwapa hamasa katika kushiriki vema katika mipango mingine itakayoweza kutokea baadae.
Sambamba na yote pia serikali iongeze mkazo katika kuwawajibisha viongozi ambao watashindwa kusimamia mipango thabiti kwa wananchi kwani wanaibebesha serikali mzigo wa lawama kwa watu wake na kutoona umuhimu wowote juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali kwa watu wake.
Jaribu kutafakari juu ya suala la tozo za miamala, je! Wananchi wangepokea vipi jambo hili endapo wangepewa muongozo thabiti juu ya hali halisi ya nchi ilivyo?
Je! Kuna mwanachi ambaye angetia vita ya maneno juu ya uanzishwaji wa ziara ya "Royal tour" endapo angeelezwa kwa kina lengo na dhumuni ya jambo hilo?
La hasha, ni ukweli usiopingika kuwa wananchi wote wapo tayari kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali ziletazo maendeleo katika taifa kwa ujumla endapo tu kutakuwa na njia thabiti ya ufikishwaji wa masuala hayo. Ambapo elimu yakinifu na mrejesho wa shughuli hizo ndio nguzo kuu katika kuinua imani ya wananchi dhidi ya mipango mbalimbali ya taifa zima kwa ujumla.

Upvote
11