Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kila mmoja ameshuhudia jinsi uchaguzi wa Serikali za mitaa ulivyoharibiwa na taasisi za usimamizi.
Ni dhahiri kulifanyika maandalizi ya kutosha toka mwanzo kuuharibu uchaguzi huu, ndiyo maana kuliwekwa mpaka kanuni za kuwalinda watakaoharibu uchaguzi.
Wananchi wana haki ya kuwakataa na kutowapa ushirikiano wowote viongozi ambao hawakuwachagua, hiyo nayo ni sehemu ya demokrasia. Hivyo sehemu yoyote ile ambako wananchi wamefanyiwa maovu ili kulazimishwa watawaliwe na kiongozi ambaye hawakumchagua, hata baada ya kutangazwa, wamkatae, na wasimpe ushirikiano wa namna yoyote ile, na mtu huyo atengwe na kuwekewa vikwazo vya kijamii.
Kushirikiana na kiongozi ambaye hamkumchagua, ameletwa kwa njia ya uovu, ni kuubariki uovu uliotendeka, itakuwa ni kukubali kuwa sehemu ya uovu.
Maendeleo ya Demokrasia yana gharama zake, lazima tukubali kuzibeba gharama hizo, lakini kamwe tusibariki uovu.
Hata kama hatua hizi haziwezi kuwashitua walioupanga uovu huu, lakini hao viongozi waliowatengeneza wapokee adhanu kutoka jamii yenye hasira dhidi ya uovu uliobuniwa na kusimamiwa na TAMISEMI