MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa wananchi wengi hawakubaliani na serikali kwenye suala la chanjo za korona.
Huhitaji kufanya utafiti wa kina kujua ukweli wake kwa sababu utapata maoni ya wananchi kwenye video za YouTube katika channel kama Millard Ayo ambazo hazifungamani kisiasa katika kutoa habari.
Kama ukitaka kujua mawazo ya wananchi wengi angalia sehemu ya maoni hasa kama wachangiaji wamekuwa zaidi ya 800.
Wabunge waliochangia maazimio ya Kamati ya bunge ambao waliwashambulia Askofu Gwajima na Jerry Silaa wameshambulia sana na wananchi kwenye sehemu ya maoni.
Kwa taasisi yenye watu mwenye akili timamu na ambao wanatumia fikra timamu katika kuchambua maswala mbali mbali watayachukua maoni ya wananchi kama picha na kiakisi kwa yale wanayofanya kama bunge na serikali.
Mfano ni hii video ya YouTube ambayo baadhi ya wabunge walikuwa wanawashambulia kina Askofu Gwajima na Jerry Silaa ambayo imepata wachangiaji zaidi ya 1000. Soma maoni ya wachangiaji utagundua kinachoendelea katika fikra za watanzania wengi.
VIDEO:
Kwa maoni haya ya wananchi ni lazima Bunge na Serikali wajitathimini kwa yale wanayoyafanya kwa sababu inaonekana hayana maslahi kwa wananchi wengi!
Bunge na serikali wanatakiwa wajue Askofu Gwajima na Jerry Silaa ni sauti ya watanzania wengi walioko “nyikani”.
Serikali na bunge waache “kushupaza shingo” kama hawataki kuvunjika kwa sababu kwenye siasa hakuna watu wajinga na wasio wajinga bali kuna watu wanakubaliana na serikali au hawakubaliani na serikali.
Mmarekani aitwaye George Carlin aliwahi kusema, “Never underestimate the power of stupid people in large groups.”
Muda ni mwalimu wa kweli!