Wananchi wilaya ya Kasulu wanarejeshewa fomu zao za NIDA

Dusabimana

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2019
Posts
278
Reaction score
248
Huku TCRA wakiendelea kufungia Watu Line zao katika Wilaya ya kasulu NIDA wanawarejeshea Wananchi fomu zao ili wakahojiwe upya!

Mwezi January mwaka huu walianza kutoa namba kwa baadhi ya watu wachache huku Watu wengi wakiwa bado hawajapata ! Ghafla tena J'pili ya February 2 tangazo likasikika "wote ambao hawajapata namba za NIDA wafike kwenye ofisi za Mitaa yao watarejeshewa fomu zao na kuhojiwa upya"Hali ambayo imewakasirisha wengi wakilinganisha na usumbufu walio upata Mwaka juzi kwa kupanga foleni wakisubiri kusajiliwa! Watu wengi wamesikika wakisema kuwa hawatoenda kupiga kura October mwaka huu na baadhi yao wakiapa kutomchagua Magu tena kwa unyanyasaji anao wafanyia!
 
Kwani mbona kumtambua mtu ambae sio raia ni rahisi sana mnashindwa nini huko kigoma na ngara mbona sisi tuko mpakani lakini watu kibao tayari wamekwisha patiwa namba za vitambulisho nahisi tatizo ni ubishi wenu nyie waha
 
Sasa wataishije jamani hawa watanzania wenzetu halafu kwa nini wanashindwa kusikilizwa wakati wako kwenye vijiji vyao kabisa vya kuzaliwa mbona tunaanza kutengeneza matabaka
 
Kurejeshewa fomu kuna maana kuwa fomu zilijazwa kimakosa wazirekebishe !! Halafubwarudi ofc za NIDA KWA KUKAMILISHA TARATIBU ZILIZOBAKI

Mfano fomu haina sahihi ya mwenye kiti wa mtaa , haina muhuribwa mtendaji wa kata

Haina sahihi ya afisa wa uhamiaji maama yake haijakamilika ili mtu apte number kuna hatua km 4 fomu inapitia baada ya kupigwa pichwa ndio number inatoka

Msipende kupotosha umma

sent from toyota Allex
 
Inawezekana ni mapungufu ya sahihi za viongozi lakini kuhusu uraia jamaa wanatambuana vizuri Hadi kwenye mapori ya Kumtundu na Kumkambati. Shida iko mpakani kule Muyama maana wengine wameoana kimataifa.
 
Napendekeza viwepo vitambulisho mbadala kwa watu wa pembezoni huko ili kutowanyima fursa kama ajira na passport kwa kisingizio cha utata wa uraia wao
 
Kwani mbona kumtambua mtu ambae sio raia ni rahisi sana mnashindwa nini huko kigoma na ngara mbona sisi tuko mpakani lakini watu kibao tayari wamekwisha patiwa namba za vitambulisho nahisi tatizo ni ubishi wenu nyie waha
Hata huko Dar Uhamiaji hawako makini Warundi ni wengi sana! Mfano kuna Jamaa ambaye ni Murundi na anafahamika ni artist kwa uchoraji anapatikana pale Mwenge .Ni Murundi na bado ndiye kapewa ushindi mchoraji bora kitaifa! japo Mama yake ndo Mzaliwa wa Kasulu. huyo Jamaa alikuja kutoka huko kwao Burundi 2016 kisha kuondoka kwenda Dar! Na wengine wengi wanafahamika sana, kama Uhamiaji wangekuwa makini wangetoa chochote kwa Mabaharia wawaelekeze wageni ni akina nani. Wahamiaji haramu wangepungua. Kuliko kuwataabisha Watanzania na kuwacheleweshea haki zao za msingi!
 
Kwenye uchaguzi hawakagui RAIA au muahamiaji haramu Ila kwenye huu upumbavu wa NIDa ndiyo utasikia mambo ya kijinga ya hivyo...kama MTU ni mkimbizi kwa nini usimrudishe kwao kuliko usumbufu wa kipambavu,ifikie wakati watu wa mkoa wa kigoma kudai haki\uhuru maana wanaonea sana......kuna watu kibao wageni wanapata passpoti,Kitambulisho cha NIDa,cha mpiga kura kiulani kuliko hata RAIA huu kama siyo ujinga ni nini?

Kuna watu mababu zao walikuwa wanachama wa TANU wa mwanzo kabisa wamempokea nyerere kwenye harakati za kudai Uhuru mkoani kigoma hadi leo familia zao wanavithibitisho....lakini unakuta afisa wa uhamiaji ambaye babu YAKE hakuchangia chochote kwenye harakati za kujikomboa toka kwa mkoloni alikuwa maporini anachunga ng'ombe eti anakuhoji uraia anakwambia ni mkimbizi ...kweli hii nchi ni ya hovyo sana.
Wazee wetu walikuwa na passpoti za kwanza kabisa za Tanganyika lakini bado utaambiwa ni mkimbizi kwa kuwa unatoka kigoma...kama vipi acheni tuwe koloni la mmarekani.
 
Ila tatizo lenu nyie waha ni wabishi sana badala ya kutoa ushirikiano kwa maafisa wa uhamiaji nyie mnabishana nao mwisho wa siku fomu zenu zinapigwa alama maalum
 
Hamna ubishi wowote hao maafisa wenu wanakuja na dhana ya ukimbizi vichwani mwao ndiyo maana wanaleta usumbufu.....MTU umekamilisha nyaraka zote umehojiwa umepigwa picha...wakatoa majina watu kama wamekosea wakahakiki wabadilishe majina yako sawa...leo unamrudishia fomu mtu akahojiwe tena,huo usumbufu unawafanyia watu wasiyojielewa...mbona mikoa mingine hawafanyi hivyo na ilikuwa kama hujakamilisha taarifa hawapokei fomu sasa leo wanakuja na upumbavu tena..utasema watu ni wabishi,isitoshe kuna watu walijiandikisha wakakamilisha taratibu zote wakaondoka,je utawapa nauli ya kwenda kuhojiwa tena?
 
Na wanasema hata ukipewa vitambulisho kina life span ya maiaka 10 tu kwahiyo zoezi la mahojiano ni zoezi endelevu
 
Back
Top Bottom