Wananchi wote wasifiwe kwa kujilinda na korona, Mungu ashukuriwe inaisha.

Wananchi wote wasifiwe kwa kujilinda na korona, Mungu ashukuriwe inaisha.

Masi Lambo

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2020
Posts
532
Reaction score
360
Sasa naamini Mungu anailinda Tanzania na korona, lakini pia sababu sisi ni wasafi sana kuhusu pua na mdomo, tunakinyaa cha vyote kutoka puani na mdomoni.

Yaani dunia nzima inavyoogopa korona na bado kuipata kwa wingi zaidi, pamoja na lockdown zao kali za hata kuuwa wananchi wasiofuata sheria zake, lakini sisi tupo tunakita kama vile korona haipo tena. Tupo mpirani na barabarani bila hofu.

Kama nilivyosema mwanzoni, kutokana na umakini wetu asilia wa makamasi na mate, tunaweza kuwa nchi yenye wagonjwa wachache zaidi Afrika mashariki.

Pambano halijaisha ila Mungu lazima asifiwe, Magufuli apewe pongezi kwa kututoa hofu na kuendeleza uchumi, waziri wa Afya asifiwe kwa kazi yake nzito aliyofanya bila kulala. Wananci wote wasifiwe kwa kujilinda na kutoa hofu, walioko Ulaya na Marekani wanashangaa na kutoamini.

Asante mwenyezi Mungu wa waislamu na wakristo wote hata marastafarian.

Amin.
 
Corona ipo usijidanganye
Ndugu yetu dereva wa Lori za dangote kaondoka juzi tu na familia yake ikawekwa karantini.
Sijasema imeisha, ila huwezi kufananisha na nchi nyingine hata za jirani pamoja na lockdown zao. Jaribu kufananisha na UK yenye lockdown kali mpaka leo, au hata Kenya inayoua raia sababu ya lockdown.
 
Pigo linalokuja kwa kasi ni la walevi na waasherati.corona goodbye
 
Corona ipo usijidanganye
Ndugu yetu dereva wa Lori za dangote kaondoka juzi tu na familia yake ikawekwa karantini.
Mimi pia ndugu yangu dereva wa roli juzi tu kapata ajali amekufa.
 
Back
Top Bottom