Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Wananchi wa Fumba, Zanzibar, wamemuomba Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha ACT - Wazalendo, Profesa Omar Fakih Hamad kuishawishi Serikali kuangalia upya mpango wa kukikodisha Kisiwa cha Kwale kwa mwekezaji, wakieleza kuwa eneo hilo ni tegemeo lao muhimu la kujipatia kipato.
Kisiwa cha Kwale ni miongoni mwa visiwa 15 ambavyo Serikali imevikodisha kwa wawekezaji.
Wananchi hao wametoa ombi hilo jana Jumatano Oktoba 14, 2026, wakati Profesa Omar alipofanya ziara katika eneo hilo akiwa ameambatana na Mwakilishi wa Ole, Seif Hamad Suleiman.
Wamesema kisiwa hicho kinatumika kwa shughuli za uvuvi na utalii, ambazo zinawapatia kipato cha kuendesha maisha na kuhudumia familia zao.
Baadhi ya wananchi hao wamedai kuwa hawajapewa taarifa wala kushirikishwa katika makubaliano yoyote kuhusu mpango wa kukikabidhi kisiwa hicho kwa mwekezaji.
Mkazi wa Fumba, Hassan Othman Hassan amesema wananchi wana wasiwasi kutokana na taarifa za kukikodisha Kisiwa cha Kwale kwa mwekezaji, akieleza kuwa eneo hilo ni miongoni mwa vyanzo vyao muhimu vya kipato.
Chanzo: Mwananchi