wanandoa badilikeni

wanandoa badilikeni

ndoa nyingi sana zinamatatizo na visababishi ni wanaume,hivi inakuwaje mwanaume anajua fika huyu ni mke wa mtu na wewe unamtokea?wewe unajua una mke iweje umtokee msichana tena kabinti kadogo? iweje wewe unagirl friend wako na bado unawatokea wengine? mimi bwana tatizo kubwa ni kina baba,hata wasichana wanao jiuuza,wanajiuza kwa sababu wanaume wapo wanao nunua
Lakini nani wa kusema HAPANA? Yaani wewe ukitokewa huwezi kukataa?
 
Suruali zilizobana, min skirt za kuachia mapaja nje, 80% ya manyonyo kuwa nje, Mikao yenye kuleta mihemko kwa mwanamme sasa tutegemee nini hapo????????????:nono:
 
chek kwenye trafiki jam;
ukiona mwanume na mwanamke wamekaa tu kwenye gari bibi macho mbele bwana bize na mskan basi ujue ao wanandoa
ukiona wanaongea ongea vicheeeko vingi basi ujue kampa lift kimada wake labda apo wanapongezana jinsi walivyopododoa jana
ukiona stor nying bar mkono wa eva umeshikwa na adam mara kamlalia bega mara kamshka ndevu bas ujue ao wachumba au mtu na hawara yake
ukiona bibie macho mbele bwana kashika gazet bar maongez mpk muhudumu aje that vp utaongeza basi ujue ao ni mtu na mume wake
ukiona kwenye meza poch yake bwana kaishika ,miguu imewekwa juu ya mapaja ya bwana ujue uyu ana mke uyu ana mme bt wamemisi kufanya ayo manjonjo so wanafarijiana (ni wahanga wa mapenz mfu uko kwenye uhusiano wao)
NI WACHACHE SANA WANAENDELEZA VICHEKO NA SHAMRA SHAMRA MAHABA AFTA MARRIAGE...............eeeh mola nsaidie mie manake dahhhhhh hatari!!!!!!


Good work shostito
 
ndoa ni tamu sana only if umeolewa na mtu unaempenda na anakupenda
 
:crying:weekend hii niliamua kuzungukia viwanja mbalimbali kwa ajili yakuona yanayojiri mjini hapa lakini katika mambo yaliyonivuta ni jinsi watu niliwaona wametoka vijana ambao hawajaoa au ambao walikuwa wametoka kama groups walinifurahisha sana sasa ukija kwa wale waliokuwa mke na mume mara mume yuko busy na simu kageukia upande mwingine au wako kama wanasikiliza mahubiri hivi huwa mkiwa pamoja ndo kuweka heshima au kunakuwa hamna habari za kuelezana hembu nisaidieni kwa hili naamini kuna ambao wameshaona hili au wao wenyewe ndo wahanga

Majibu ni kwamba, usiku wote, watu wawili mumeongea mpaka asubuhi;Stori nyingi huzunguzwa masaa hayo( Kwa lugha nyingine " Pillow Talk"), Hao unaowaona wakishikina mikono na kupigana mabegwa, STORI ZITAISHA BAADAE!!!!
 
[COLOR=darkslateblue said:
Mwasu;1175204]hapa umesema kweli kabisa rose sijui kwnin watu wakishaowana mapenzi yanapungua jamani me mpaka sometime naogopa hii kitu
.[/COLOR]

Si lazima muwe mnacheka barax2ni ndo muonekane mnapendana. Kuna maongezi ya hapa na pale munaweza kuwa mnaongea safari inaendelea. Kama mlikuwa mumelala usiku mzima mnapiga story zenu na mipango ya maisha ikawa imewekwa sawa si lazima muwe mnaongea wee kama hakuna story iliyojitokeza mkaanza kuidiscuss.

Mwasu Ndoa ni nzuri zaidi hata kipindi cha G/F na B/F kama umempata Umpendaye na Anakupenda Pia. Kwenye G/F na B/F bado kwanza mnasomana tabia, kwa hiyo kama mmelidhiana mkakubali kukaa pamoja kama life partner inamaana mmeamuwa kujitowa kwa kila mmoja wenu. Mnaweza kuifanya ndoa yenu yenye raha au yenye machungu kwa kadili nyie wenyewe mlivyojitowa. Zaidi muwe wazi kwa kila mmoja wenu na kuzungumza tofauti zenu ili kila moja ajuwe mwenzake anapenda nini na anachukia kitu gani. Hayo yote yanawezekana kama mkimshirikisha Mungu na siyo kwa Nguvu zenu. Mfanyane kuwa marafiki na kuchukuliana. Ujuwe mahitaji ya mwenzi wako na kuheshiana. Kwa mwanaume ujuwe kujali mke wako na Kumpenda. Kwa mdada muheshimu mumeo na ajuwe unamuheshimu. Msali pamoja munapoenda kulala na kuamkapo. Mungu akiwa kati yenu utasikia wengine wanalalamika ''wanaume watoto wa baba mmoja'' wewe unapeta tu na kumshukuru Mungu na kukemea kimoyo moyo kuwa siyo maneno ya kweli kwa huyu niliyepewa na Bwana. Kwa akina kaka utasikia ''wanawake wa siku hizi wako material zaidi hawajatulia huko maofisini'' Unasema kimoyo moyo siyo kweli kwa huyu niliyepewa na Bwana.

Karibuni kwenye Chama cha Wachache Rose 1980 na Mwasu na wengine wote. Mungu akawape kile kinachowafanana





 
uzoefu unaonyesha kwamba kuzoeana kwingi kunapunguza mahusiano. badilika kwa kudumisha mapenzi, ndoa haizeeki
 
Back
Top Bottom