Binadamu tunashindwa kuelewa kuwa WATOTO NI RIKIZI KUTOKA KWA MUNGU.
Kama ilivyo katika riziki nyingine, kufanya kazi kila siku hakuwezi kumfanya kila mmoja wetu awe tajiri, vivyohivyo kufanya sana mapenzi na mwanamke hakukupi uhakika kuwa utapata watoto wengi maishani.
Kikubwa inatakiwa tusiwe na presha kwa mambo tusiyo na uwezo nao. Kuna ambao wamepewa zaidi watoto zaidi ya kumi kuna wengine wana wawili, wengine mmoja na wengine hawana kabisa.
Nabii Ibrahim alikaa kwenye ndoa yake na Sarah kwa zaidi ya miaka 80 bila ya kupata mtoto...alikuja kupata mtoto uzeeni kabisa.