Wananiwangia nawasikia, niwafanyaje hawa?

Wananiwangia nawasikia, niwafanyaje hawa?

Generetaion Z

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2022
Posts
343
Reaction score
874
Wakuu

Nimekuja hapa nina andika kwa ghadhabu kidogo 🙁

Kuna watu wanasema Uchawi haupo ila upo na unakera haswa hatukatazi watu kufanya mambo yao ila si mambo ya kuchezeana miili ni jambo linalokera sana.

Kuna mambo unafanyiwa usiku ya ajabu ajabu sawa unaamka ila unakuta mwili wako unafanyiwa mambo ya ajabu ajabu yasio kichwa wala miguu.

Niende kwenye point:

Kunakipindi nilisafiri nikaenda mkoani kitovuni kwangu uko kumamoto kaskazini.

Wakati nipo uko siku zote nilikuwa naenjoy maisha ya pale ila mauzauza yalianza pale nilipoanza kutembeatembea na kuchangamana na watu ktk vilabu, makanisani n.k

Wakati wa usiku hakuna rangi sijaiona mpka nikawa naona usiku mrefu

Kwanza ilikuwa nikilala nitaota ndoto za ajabu ajabu hazina kichwa wala miguu, alafu nikiamka asubuh nimezisahahu zote sikumbuki hata moja.

Nikamweleza mwenyeji wangu mzazi wangu akanambia uwe unasali usiku,binafsi ninasali ila juu juu tu

Nikafuata ushauri wake nikawa nasali sana, sasa usiku nikiwa nimelala usiku mzito usingiz unakata ilanakuwa nimefumba tu macho.

Sasa nikiwa nini imejiegesha naanza kusiia kama kuna kitu sicha kawaida kinanisogelea mi nakisikilizia tu, huku nasali kimya kimya.

Kinavyonisogelea. Moyo unaanza kwenda spid sana kwa ghafla, na joto kupanda zaidi.

Hatua ya kwanzab kinakuja puani na mdomoni nasikia kabisa kitu chenye joto kinaingia puani mpaka sinus za pua zina tanuka wakati kinafanya hivo mi ninasali tu kimoyo moyo.

Wakati kinaingia puani na mdomoni moyo unazidi spid zaid na pumz inakuwa nzito kuhema, joto la mwili linakuwa juu, kikishatoka puani na mdomoni apo mdomo unakuwa upo wazi, kinarudi tena najihisi tena kama kinanibana mbavu kinazunguka nami hadi miguuni.

Hapo hapo nahisi kama kitu kinaingizwa mdomoni tumbo linaanza kusokota ,kikimaliza kinakuja kiunoni kina . Ninabana kiuno sana mpaka najihisi kama haja.

Hapo hapo naanza kuhisi kama kuna kitu kinavutwa kwenye korodani zangu,kinahangaika haswa mi hapo nasali tu, kinatoka kinarudi tena.

Yani nakisikia kabisaa hapa kimeondoka hapa kimerudi tena yani. Kule ni baridi ila jasho linanivuja.

Sasa asubuh nikamwelezea mzaz akanisisitza kusali.

Ila wakati naenda kujisaidia haja haitoki. Kabisa na sikua na iyo shida

Hali ikawa inaendelea nikazidisha maombi kule nikaamua kusepa maana usiku ulikuwa mrefu mno,kuanzia hapo ninatatizo la kusahau sahau. Skip those days njoo leo usiku.

Nipo zangu nimelala huwa nachelewa kulala nalala saa saba usiku muda mwingi nakuwa online,

Nimezama kitandani leo nimelala mwenyewe nyumba nzima tangu ijumaa ,siogopi maana najua Yesu yu pamoja nami nikimwomba.

Nikalala vyema hadi saa tisa hivi usingizi ukakata nipo nimejifunika tu, gafla nje nasikia mbwa wana bweka sana mfululizo sehemu ninayoishi nyumba nyingi zina mbwa ila wapo getini, mbwa wakawa wanabweka sana kuashiria kuna kitu wameona.

Kama dk mbili hivi nikaanza hisi kunakitu si cha kawaida kinanisogelea, mbwa kule wakawa wapo kimya sasa awabweki tena. Iko kitu sàsa kama kawaida kikaanza mapicha picha kama niliyoelezea hapo juu.

Nikawa nakemea sana kinatoka kinarudi tena kinatoka kinarudi nakisikia ,joto linapanda moyo unaenda kasi mnoo kikitoka unapoa, kikirudi unaanza upya.

Mi nakemea tu mara kikasepa kama dk mbili nikasikia mbwa wanabweka tena kikarudi nikahisi mwili unatetemeka mara mkono mara mguuni yani kama kilikuwa kinapambana kuniinua ila mi nikawa mbishi.

Kikasepa tena mbwa wakawa wanabweka mfululizo tena nikajuwa kimeondoka mazima kumbe bado kikaja tena nahisi sasa muda ule kilikuja na nia ya kunifuta kumbukumbu, nikahisi hewa ya joto puani na mdomoni alafu kichwa kikawa kama kina stimulate nikasonya kikaacha, kikarudia tena nikafumbua macho, kikaacha kikasepa mbwa wakabweka tena, mara kunguru wanapita kwa kikundi wanageuza kama mara tatu hivi.

Wapuuzi sana hawa watu wa gizani, nilikuwa naweza kuamka ila niliamua tu kulala nn isije nikakutana na mtu namjua mwisho wa siku nile visu asubuhi watu waseme kajiua maana nipo mwenyewe na nimejifungia.

Yani nahisi ndo mambo yao kila siku wamechukuwa ufahamu wangu, napoteza kumbukumbu,nadharaulika, sijiamini tena, nipo kama nimevalishwa uhusika usio wa kwangu, wameharibu mfumo wa chakula wananilisha vitu vya ajabu, they hunt my potential m&fk.

Washenzi sana sitaki kumjua anaeniwangia ila sitaki aniwangie, shusheni mbinu za kuwazibiti ambazo ni za kawaida.
 
Hapo ulipo upo katikati ya kushinda na kushindwa. Lakin nasema hakuna mchawi mwenye nguvu kukushinda wewe na mchawi wako ni wewe mwenyewe na hapo umewapa access yako. Km utataka ushauri zaidi nicheck.
 
Haya mambo yapo aisee...Kama Mimi tangu usiku wa juzi tunakesha.Mwanangu anapiga kelele tangu juzi usiku kucha anaona kuku na mbwa!sisi hatuwaoni.Na haumwi, kukicha Yuko vizuri tu.Ila naona tofauti kwake tangu hiyo juzi anakuwa mnyonge na hataki kucheza na watoto wenzie,muda wote anataka awe na Mimi au mama yake,Basi.Sijui ngoja tuone usiku wa leo.
 
Haya mambo yapo aisee...Kama Mimi tangu usiku wa juzi tunakesha.Mwanangu anapiga kelele tangu juzi usiku kucha anaona kuku na mbwa!sisi hatuwaoni.Na haumwi, kukicha Yuko vizuri tu.Ila naona tofauti kwake tangu hiyo juzi anakuwa mnyonge na hataki kucheza na watoto wenzie,muda wote anataka awe na Mimi au mama yake,Basi.Sijui ngoja tuone usiku wa leo.
Unasubiri tena yatokee yale yale na utayaona. Chukua hatua iliyo kinyume na kama dogo anajua kusali mfundishe asli akiona upuuzi na mazingaombwe hayo. Tambua NURU na giza havikai sehemu moja na siku zote giza hukimbia.

Msali kwa imani na sio kusubiri kuona huo upuuzi wa wachawi
 
Imeshawahi nikuta hiyo hali,zidisha maombi hasa kila unapohisi hiyo hali inakujia,amka na uombe na kukemea kwa jina la Yesu, fanya hivyo kila unapohisi inakujia, pia usiwe unalala usiku bila ya kufanya sala,fanya maombi ya usiku hasa huo muda unapotaka kulala.

Pia maombi bila kuishi katika usafi ni kupoteza muda,kwani maombi ya mwenye dhambi ni kelele mbele za Mungu.

Hizo ni nguvu za giza zinakufuatilia, inaweza kuwa ni wachawi au hilo eneo lina mauzauza,wakishaona una msimamo na Mungu watakimbia na hutaona tena hizo hali,nowadays am sleeping like a baby...
 
Haya mambo yapo aisee...Kama Mimi tangu usiku wa juzi tunakesha.Mwanangu anapiga kelele tangu juzi usiku kucha anaona kuku na mbwa!sisi hatuwaoni.Na haumwi, kukicha Yuko vizuri tu.Ila naona tofauti kwake tangu hiyo juzi anakuwa mnyonge na hataki kucheza na watoto wenzie,muda wote anataka awe na Mimi au mama yake,Basi.Sijui ngoja tuone usiku wa leo.
Wahi kwa wataalam,hao wasenge walitaka mchukua mwanangu
 
Hahahha... pole sana. Subir nkupe kisa changu.
Miaka kama 5 hv niliwah kufanya kazi eneo moja kijijini. Nlipokua nakaa n kama nyumba za ofisi ziko ndani ya fence af nje ya fence ndo wanakijiji wanaishi. Nakumbuka tulikua staff wawili tu ndani ya hilo eneo kila mtu na nyumba yake.

Mapicha picha yakaanza, yaan ukiwa umelala usiku unaskia kama mtu anakuja anamwaga toroli la kokoto kwenye bati, yaan vurugu kwelikweli. Sometimes kama mtu anarusha jiwe juu ya bati n.k ilimradi kero. Mwanzon nkawaza labda ni ndege, lakn akili ikacheza kwakua ndege pekee wa uaiku ni bundi sasa inakuaje bundi wengi hivyo au wanakuja kupigana juu ya bati?

Anyway, siku moja tumekaa na staff wengine ambao wanakaa mtaani nkawauliza hyo ishu, wakacheka sana. Wakaniambia hapo kuna wanga wanakuja kucheza na system usiku. Na wakasema huyo mwanga lazma asubuh ajitahd kuja kukupa salam na kukuuliza umeamkaje n.k. nkatafakari nkashindwa kujua ni nan maana kila siku nakutana na watu wengi asubuh.

Hapo ndo nkaja na psychological solution, nkangoja wateja wakiwa wengi nkaanzisha hyo mada kwa staff wenzangu, kisha nkawaambia kwetu kuna dawa ambayo ukiwa nayo mwanga akija anastuck anashindwa kuondoka mpka uongee neno lolote ndo anafanikiwa.

Nkawaambia naenda kuchukua hyo dawa, na nkija nkimkamata ntamchapa viboko hadi kukuche then akipita mtu namwita kwa ishara, akishakuja akamuona pia then ndo naongea chochote ili huyo mwanga afanikiwe kusepa lakn akijua kbsa ushahidi upo wa yeye kuniwangia.

Tena nkawaambia kuna mwalim walikua wanamchezea akaenda kwao akaja na mtungi, akawa anawakamata usiku anawatia viboko af anawapeleka shambani kwake wanalima hadi asubuh ndo anawaachia.

Turns out hyo sehem wanaogopa wasukuma because ya ishu ya misukule. Mimi sio msukuma lakn kwakua natokea mwanza wakawa wanahisi mimi n msukuma pia. The next day nkasepa nkaenda kujilia mbususu kwa manzi yangu nkarud kama 5 days later.

Tangu nlivorud sikuwahi kuskia chochote mpaka naondoka hilo eneo.

So smtyms inasaidia kama n mwanga, kama n mchawi siez kujua maana mimi siamini mambo ya ulozi, na Noah nakula like every week na ndum pia niliwahi kua mdau.

Kila la kheri mkuu.
 
Back
Top Bottom