G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,505
- 40,002
Tuingie field kwa kigezo kimoja tu "Urais ni taasisi" "Urais wa nchi ni jambo linalomuhusu kila mwananchi"
Hawa watu abadan wana ugomvi binafsi tena unafukuta kwelikweli. Kila mmoja hana amani na mwenzie. Facts ni hizi hapa.
1. Magufuli alipopata ridhaa ya kuongoza CCM kuwania urais wa JMT, Membe alijitokeza hadharani na kuahidi kustaafu siasa za majukwaani. Jana Membe ananukuliwa kuwa amefukuzwa CCM kutokana na tatizo la urais (2020?) na kuwa ndoto yake iko pale pale. Si alisema amestaafu siasa za majukwaani? Nasema ni 2020 kwa sababu kama ingekuwa ni 2025 basi ni nafasi ya kila mwana CCM mwenye sifa ilimradi akubalike hivyo kusingekuwa na haja ya kumfukuza.
Ni kwanini Membe ajipambaue wazi wazi kumpinga na kumvaa Magufuli kwenye urais? Ni kawaida? Ni kwanini Magufuli ahamaki na kumfukuza CCM haraka haraka hivyo hasa ikizingatiwa kuwa kutokana na nguvu ya kimamlaka aliyo nayo ndani ya CCM, anaogopa nini? Nguvu ya Membe inamtisha? Kwanini? Yupo na kina nani wanaotisha hivi?
Rais Magufuli alipoenda kusini kwenye ziara yake 2019 hakuonana kamwe na Membe, pia alipofika jimbo la Mtama akadiriki kupiga vijembe waziwazi kuwa kuna mtu alichelewesha maendeleo ya Mtama eti akayapeleka kwingine. Yani mbunge apeleke maendeleo kwingine, nje ya jimbo analoliongoza?
Pia, jambo ambalo si la kawaida kwa mkuu wa nchi ni kuwa alipofika Lindi kuendelea na ziara yake hatimaye aliamua kuondoka kimya kimya bila ya taarifa wala watu kujua alipitia njia ipi kurudi Dar! Kamwe hili si jambo la kawaida. Nini kilitokea? Nani mafia huyo aliyehusika? Lipo jambo!
Kumekuwepo na mtu anayeitwa Hamisi Khagasheki ambaye amejipambanua kama rafiki wa karibu wa Membe. Huyu naye haikutegemewa ila hajawahi kuwa karibu na Rais Magufuli na amekuwa mara kwa mara akirusha vijembe kule Twitter kwa mkuu huyo wa nchi. Watu wote waliokuwa marafiki wa Membe ilibidi wajikane sana ndipo waingie kwenye himaya ya Magufuli kitu ambacho kilikuwa tofauti na wale waliokuwa karibu na Lowassa.
Membe pamoja na kufungua kesi mahakamani kuhusu mtu anayeitwa Cyprian Musiba kumchafua, bado anaonekana ndiye mkosaji mbele ya mhimili wa utawala. Yani kwa huu utawala kupambana na Membe basi wewe ni Yes haijalishi kuwa unamtukana, kumzushia ama vipi (Rejea kina Makamba na Kinana waliandika mpaka barua za malalamiko, hazikujibiwa popote kwenye vikao vya chama badala yake leo wameadhibiwa wao). Kwa hili pia kunadhihirisha hali si shwari kabisa kwa wawili hawa. Leo wale wote waliolalamika kuhusu Musiba wamenyonyolewa na kuonywa! Hakuna aliyepata hata nusu ya ushindi kisa tu wanaonekana kuwa kwenye mkondo wa Membe.
Wananzengo tuzame porini kuusaka ugomvi huu mkubwa kati ya wawili hawa. Huenda yapo mambo mengi makubwa tunayohitaji kuyajua kuhusu wakubwa hawa hasa miongoni mwao akiwemo mkuu wa nchi!