[
G Sam CCM ni taasisi, nakushauri ondoa fikra potofu kichwani mwako kusema eti Mh. Magufuli kamfukuza Mh. Membe uanachama, hapana kabisa.
Taasisi ya CCM imepiga imemkuta anamakosa, anakiburi na ujuaji kama vile yeye ndiye CCM wakati kumbuka kila mtanzania alikuwa kachoshwa na wanaojifanya wana hati miliki ya chama.
Ukitaka kujua kuwa CCM ni taasisi angalia tu ni watu wangapi imewatosa lakini bado ipo imara. Mh. Membe huko aliko atakuwa anahangaika ku draft barua za kuomba msamaha, maana sasa ameondoshwa kwenye mafua kwa sababu kakulia CCM kalelewa CCM sasa maisha ya nje atayaweza?
Yaani kama Mzee Kingunge mpaka siku akiwa kalazwa alisema yeye ni CCM damu damu, sembuse huyu Mh. Membe? ambaye hata ushawishi hana kabisa, labda kama ataungwa mkono na JK, yaani JK ajitoe CCM, atangaze kumuunga mkono Membe, then watafute chama wakibake ili Membe agombee urais, then JK apite nchi nzima kumpigia kampeni.
Kwa ninavyofahamu JK hawezi kufanya hivyo kwa sababu anafahamu kuwa CCM ni taasisi, yaani hawezi kujipa taabu kwa miaka yake aliyobakiza hapa duniani kuanza kushindana na taasisi uliyoiasisi na kuiishi ila baadaye ujiwekee mazingira ikudharirishe
Endelea kujidanganya