Wananzengo tuingie "field" kuusaka ugomvi binafsi kati ya Rais Magufuli na Benard Membe


Endelea kujidanganya
 
Wana CCM mlioko CCM mnajifunza nini ktk kutenda haki, Membe leo amekuwa dhalili wakati alijiona yy ndo CCM wa milele, aliitetea tume ipo huru lkn sasa hawezi kusema ni tume huru, aliipinga katiba ya Warioba lkn sasa anaitamani.
Hawawezi kujifunza chochote kwa sababu wanasiasa huwa na kawaida ya kusimamia kile kinachowapa maslahi. Unafikiri walikuwa hawayajui haya? Mtu kama Membe alikuwa amejihakikishia kushika urais na akaona katiba iliyokuwepo ingempa fursa nzuri ya kutawala. Lowassa hali kadhalika.
 
Chadema mmeshapata mgombea, mchukueni

Sent using Jamii Forums mobile app

Nani sisi hatuhitaji majeruhi wa ubatizo wa moto
1. Nape
2.kinana

Walijitapa ccm yakwao, eti wao hata bao la mkono.... kweli wakamshindisha bila sabuni

3. Makamba senior
4. Makamba junior

Eti wao wanaijuwa ccm ni wanafamilia, wakatabilia wenzao UBATIZO WA MOTO

5. LOWASA
6.SUMAYE

sasa wapo wengi kwelikweli kwenye kundi la akina Lugola, andengenye nk.

Moto unawaka Lumumba, ubatizo unaendelea..... Mungu atusaidie ubatizo ufike tena na kukamilika kwa mwigulu, Makonda, sabaya bila kusahau wakuu mikoa ya Iringa na Arusha.

Amina
 
Wana CCM mlioko CCM mnajifunza nini ktk kutenda haki, Membe leo amekuwa dhalili wakati alijiona yy ndo CCM wa milele, aliitetea tume ipo huru lkn sasa hawezi kusema ni tume huru, aliipinga katiba ya Warioba lkn sasa anaitamani.
Tatizo Bwana Maembe alitaka kuuaminisha umma kua yeye ni zaidi ya taasisi CCM ! Aliwavimbia viongozi kwa kauli za kejeli kama niguse ninuke, sasa sijui wameanza kunuka ? Walianza kusema oooh eti mzee Mangula kachoka hamuwezi bwana yule...subiri tuone
 
Inasemekana ,ila si za uhakika,Membe ndie aliepanga mpango wa kumpoisoni Magufili Dodoma na huko ziarani Lindi na Mtwara
 
Halafu hao wanao mvua uanachama hawaja wahi hata kuwa mabalozi wa nyumba kumi. Walijaribu ku beep simu ikagoma kukatika, wakaokota embe dodo chini ya mti wa mpera.
Hawajui siasa na hawataki kujua. Sias azaidi ya kupenda masifa.. Hicho ndicho chama kikongwe Africa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chanzo ni Ukatibuu Mkuu wa Commonwelath 2016

JK alisha seti Mitambo yote Msaliti Benard Membe apewe Cheo hiki, Kumbuka Jk ni fundi sana wa Lobbing, aliwez kwa Balozi Muya muya kuwa Katibu wa Nchi za Maziwa Makuu na kuna Mama Mwingine alimpigania akawa Katibu mkuu wa Sadec akitoka kwny Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Africa Masharik chini ya Mzee Sitta (nmemsahau jina)


Sasa Mkuu wa Dola mpya akatangaza Nchi kujitoa kwny kiny'anganyiro kile kumkomesha Membe kwa kuwa Membe anajiona Yeye anajua sana

Bifu likaanzia hapo ila akasahau kuwa Rais hata awe dhaifu vipi bado ana nguvu kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachoendelea ni watoto wamekusanyika kuwasuta Wazee wao. Enzi za kifimbo cheza angewaambia wamepitwa na usemi " Usitukane fukunaga wakati uzazi ungalipo"
 
Walioshiriki kindaki ndaki kuidhoofisha CHADEMA sasa wote wamedhoofishwa hawana mahali pa kukimbilia(Nape, Lugola, Makamba, Membe, n.k) Wapo wale waliohama vyama tutawaangalia baada ya uchaguzi mkuu kupita. Mliopo bado madarakani jaribuni sana kuona demokrasia inastawi, ongleeni juu ya katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, mgombea binafsi n.k. Acheni woga.
 
Mnatengeneza vihadithi vya vya kusukumia siku kuelekea Oktoba 2020.

Jiandaeni jamani, kuna gharika linawajia.
 
Ninachojua CCM haimuhitaji Membe ili iendelee kuwepo.
Ninachojua taasisi ya urais haimuhitaji Membe ili iendelee kuwepo.
Wanaomuhitaji Membe ni familia yake hata nao wanaweza kuishi bila Membe.
Na Membe anaihitaji CCM ila CCM haimuhitaji atulie tu Maisha yataenda tu.
Kama unapanga mipango dhidi ya taasisi yako Lazima taasisi ikurudi.
Mwaka 2014 ulionywa ukasimamishwa mwaka mmoja na wakati huo mwenyekiti Alikua JK je alikuonea?
Mwaka 2020 umerudia yaleyale umefukuzwa uanachama na mwenyekiti Akiwa Magu na sababu ni toka 2014 hujajirekebisha umeendeleza tabia zilezile.
Kwanini unaeonewa niwewe tu na kwanini kila mwenyekiti akuonee wewe? Punguza kiburi na ujuaji na kuhisi unaumuhimu kuliko wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…