Wananzengo tuingie "field" kuusaka ugomvi binafsi kati ya Rais Magufuli na Benard Membe

Tumewapeni historia ya kufukuzwa/ kujitoa kwa wanachama wenye nyazifa kubwa ndani ya ccm. Haya fuatilia;
1. Abdul Jumbe
2. Maalim Seif
3.Augustino Mrema
4. Edward Ngoyai Lowassa
5. Frederick Sumaye
Bado chama hakikupata hata mafua, sembuse Membe wayiiiiiiiiiiiiii akwende bana
 
Jk anaweza yule master mind achana kile kichwa ww unafanya masihara nini yule mtu hatari sana yule...Jk aseme ajitoe amunge mkono membe uwezo wa kuitoa madarakani jk anao tena kweupe unakumbuka alivyowavuruga ukawa....
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwani hao waliwateta wenyeviti kwenye simu? Au walihujumu chama?

Kesi ya kinana, makamba na membe ni personal attack linked directly to someone
 
Wana CCM mlioko CCM mnajifunza nini ktk kutenda haki, Membe leo amekuwa dhalili wakati alijiona yy ndo CCM wa milele, aliitetea tume ipo huru lkn sasa hawezi kusema ni tume huru, aliipinga katiba ya Warioba lkn sasa anaitamani.
Huwaga wanajipa ukichwa ngumu... hawawezi sema walichojifunza... wanayoyaongeaga wakia madarakani au ndani ya CCM huwa wanakuja kuyajutia, INGAWA HUWAGA KIMOYOMOYO... kumbuka kauli kama goli la mkono au KAULI YA BUNGE LIVE.. etc
 
Unaijuwa nguvu iliyotumika wakati wa LOWASA....??
 
Ahh kumbe !!.

Africa bhuaana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika CCM kuna dhulma, mauaji, ukatili na ubabe. Kunukuu Maandiko Matakatifu kwa chaka mamba hii ni kashfa
 
Hakuna cha mambo makubwa wala nini. Magufuli anaogopa Membe kuwa kwenye chama kwasababu wakati wa uteuzi wa mgombea wa urais kwa tiketi ya ccm Membe angejitokeza kugombea hivyo Magufuli akaogopa akijua kwamba. Kwenye kura za maoni anaweza kuondolewa kutokana na jinsi anavyoendesha nchi na chama cha ccm. Ni uoga wa urais tu. Kwasasa hakuna atakeyeweza kuthubutu kuchukua fomu au hata kutia nia. Na Magufuli akipata urais tena Watanzania tutakuwa na hali mbaya zaidi. Magufuli hatakubali kutoka madarakani kwasababu ataogopa kufungwa. Magufuli amejijengea maadui wengi sana wakubwa kwa wadogo, wafanyabiashara, wafanyakazi na wasiokuwa na kazi. Magufuli anatuletea vita watanzania tutauwana wenyewe kwa wenyewe.
 
Ukute wanagombania vimada tu au umesahau wanaume wa Afrika?
Hili nalikubali kabisa kinawezekana baba yangu alipoteza kazi nilipokuja kuchunguza binafsi kwa undani nikagundua kisa kilianzia kwa kimada na yeye hakukubali alihakikisha kamfukuzisha kazi mwenzie wanawake ni ni shiiida!
 
Ninachojiuliza.
kama mtu amefanya mengi na anapendwa na wengi kwanini awe muoga kiasi hiko?

Shetani alivyozingua Mungu hakumuua japo uwezo alikuwa nao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana CCM mlioko CCM mnajifunza nini ktk kutenda haki, Membe leo amekuwa dhalili wakati alijiona yy ndo CCM wa milele, aliitetea tume ipo huru lkn sasa hawezi kusema ni tume huru, aliipinga katiba ya Warioba lkn sasa anaitamani.
Uzuri waliopanda miba njiani wote imewachoma nape,makambas,membe,kinana wafatao jk na mkapa,chama ni mali binafsi mwenye chama ndie anaeamua
 
Mbona waliofanya the same mistake hawajafukuzwa
 
Africa buana roho mbaya ndo mpango mzima hakuna kuwaza kesho yako, unatenda leo leo.....huku huna hata robo ya unachokijua juu ya kesho yako......leo yako wewe ni kesho ya mwenzio ni keshokutwa ya mwengine......ila mambo yanatokea siku zote kwa sababu mbalimbali nyingine ikiwa ni kujifunza na kuweka rekodi ya vizazi vijavyo ktk nchi, taifa au jamii
 
Kosa lake alionyesha makucha mapema angetumia staili ya kumchinja kobe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…