Nelson...
Ukweli haukataliki muhimu ni kuwa uwe kweli ni ukweli.
Lakini ni muhimu ujue kuwa kuna propaganda nyingi katika historia ya utumwa.
Unazungumza utumwa Zanzibar lakini umekuwa kimya kuhusu Transatlantic Slave Trade.
Yawezekana huna ujuzi wala maarifa ya historia hii.
Ninapokusoma jinsi unavyoandika na hata pale ninapokuongoza katika kanuni za uandishi unakuwa mkaidi na kurejea katika makosa yale yale basi najua kuwa hapa hakuna kitu.
Sultan kaondoka Zanzibar hana damu katika vidole vyake.
Jela za mateso na mauaji ziliingia Zanzibar baada ya mapinduzi.
Historia ya jela hizi Wazanzibari wote wangependa kusahau.
Wazanzibari wameukataa utawala ulioko madarakani toka 1964 kwenye sanduku la kura mara sita kuanzia 1995.
Nakupa yote haya kwa ushahidi na jambo la kusikitisha maraisi wote hao wameshindwa na mgombea yule yule mmoja.
Kilele cha fedheha hii ni pale baada ya kushindwa wa 2015.
Uchaguzi ule ukafutwa.
Kila uchaguzi damu ya Wazanzibari inamwagika.
Wewe unakuja na lugha "Wabantu hatusahau."
Wajue kwanza Wazanzibari ni nani.
Ndipo nikakuuliza nini tafsiri ya CCM kushindwa kila uchaguzi?
Wazanzibari wanayakataa mapinduzi?
Huenda hadi hapa tulipo hujanijua labda ungenijua ungechukua tahadhari lau kidogo.
Nimeshiriki katika uandishi wa historia ya mapinduzi nikiwa Mtafiti Msaidizi wa Dr. Harith Ghassany.
Mradi huu ulichukua miaka saba kukamilika.
Kitabu kutokana na utafiti huu kipo mtandaoni bure, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru."
Dr. Ghassany haitaji kuelezwa.
Nimealikwa Zanzibar mara nne kufanya mihadhara ya wazi kuhusu historia ya Zanzibar:
Zanzibar State University, Mwinyi Baraka Foundation, na mara mbili na Zanzibar Institute of Research and Public Policy (ZIRPP) kufanya pitio kwa vitabu viwili kuhusu historia ya mapinduzi.
Nimezungumza kuhusu kitabu cha Hashir Seif Hashir: "Mimi Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar," na kitabu cha Khamis Abdulla Ameir, "Maisha Yangu."