Wanaochukia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 wana ajenda gani nyuma ya pazia?

Wanaochukia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 wana ajenda gani nyuma ya pazia?

Kwa ubaguzi wa wazi unaooneshwa na wazanzibar dhidi ya watanganyika, sitaona ajabu watu kuyaponda hayo mapinduzi.

Ni muhimu kujua mapinduzi sio kuondoa rangi fulani ya watu na kuweka rangi nyingine bali ni mapinduzi ya kifkra...jambo ambalo kwa wazanzibar wa sasa bado sana.
Upo sahii kaka
 
Shida ndo hapo , historia imepindishwa waweke mambo wazi mbona haitaleta shida yeyote
Mkuu historia haijapindishwa mambo yako straight

WaOman walivamia visiwa vile miaka mingi tu, waliabaka na kuwanyanyasa wazee wetu, waliwadhalilisha na kuwafanya watumwa, waliwaua na kuwatumikisha kama wanyama, waliwapokonya ardhi yenye rutuba, ikafika hatua waafrika tukachoka, wakaja n Compromise ya uhuru wa mchongo mwaka ‘63

Karume, Okello na wazalendo wengine wakaingia kazini kufurusha masalia ya utawala batili na ndio hapo tukapata Zanzibar inayotawaliwa na walio wengi

Mambo yako straight, hao wanakumbuka na kuhusudu nyakati za Jamshid na wenzie ni wale walionufaika na mfumo ule kandamizi.
 
Back
Top Bottom