Wanaochukia mapinduzi matukufu ya Zanzibar 1964 wana ajenda gani nyuma ya pazia?

Basi nimekulewa nitakujibu kaka ila tusitoke nje ya mada
Sawa toa jibu na references itapendeza zaidi ukifanya hivyo, ni lini ulimsikia Hayati Karume akimsifu Okello kua ni shujaa wa Mapinduzi ya Zanzibar? Au kwa wepesi ni lini uliwasikia wananchi wa Zanzibar wakimsifu Okello kua yeye ndie shujaa wa Mapinduzi ya Zanzibar? Au kwa urahisi inapofika siku ya kumbukizi ya Mapinduzi ya Zanzibar umewahi kusikia popote Okello akitajwa km yeye ndie shujaa wa Mapinduzi?
 
Usijali nitakujibu mzee mwenzangu!!!Kua na amani tupo pamoja
 
Tatizo ni moja mzee wangu unajikweza sana na muoga wa maoni kinzani!!!Huukubali ukweli unaopingana na maoni na mapokeo yako ya kisiasa na kidini sasa wasomi hawapo hivyo!!!!Huo ndio udhaifu wako mzee wangu
Nelson...
Kama wewe unaona hivyo sawa.
Kuwa mimi muoga hilo nakataa.

Nimeandika kitabu "...the Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism," Nyerere yu hai.

Hutaki kusoma historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kuandika historia ya Waislam kwako ni udhaifu.
 
Ila darasa naliandaa usisahau miadi yetu na wewe umenihaidi utakua mwanafunzi mzee wangu
 
Nelson...
Ualimu unahitaji uwe na elimu.
Elimu ipo ondoa shaka!!!Na kikubwa zaidi nina elimu ya kibantu ambayo ni asili yetu wabantu mbali na elimu hizi zilizokuja africa kutoka mabara mengine!!!Kwahiyo kua na amani kakangu Said
 
Kuna watu hapa Afrika Mashariki wanabeza sana mapinduzi ya Zanzibar yaliyoongozwa na Mh Okello na kufanya miadhara kuyaponda!

Wana ajenda gani nyuma ya pazia?

Huyo okello kama nikweli alishiriki basi kwa Mwenyezi Mungu atakipata akitakacho, na anaeshadadia upumbavu uliofanywa na washirika wake maana yake yupo tayari hata kumkill mama/baba/ndugu yake.

Muogopeni Mwenyezi Mungu enyi wakristo/wapagani n.k, japo sio wakristo wote.
Hao ni mabaki ya sultani,wanaitwa waarabu koko,

Waite hata waarabu ugali ila ndio hivyoo waarabu/waislamu wamestaarabika, wana imani na wakarimu kuliko jamii yoyote ulimwenguni, si ajabu hata wazazi wako na mababu zako waliopita walielimika kutoka kwa waislamu/waarabu. God bless arabian people and all Muslims around the world.
Hawa ni maadui wakubwa kabisa, walitaka Mzee Karume afanyeje? atuache chini ya utawala dhalimu wa Usultani?

Wewe na wenzio ndio maadui wakubwa wa waarabu na waislamu, ila hulijui hilo ama kujitoa ufahamu.
 
Asante sana kwa maoni yako ndugu yangu na karibu ASP na TANU tujenge nchi yetu pendwa ya Tanzania pamoja!!!
 
Asante sana kwa maoni yako ndugu yangu na karibu ASP na TANU tujenge nchi yetu pendwa ya Tanzania pamoja!!!

Nchi haijengwi kwa ukatili, nguvu,dhulma na mauwaji, nchi inajengwa kupitia haki.

Waliofanya ukatili huo leo hii hatunao kwa maana wameshakufa, kama ni yule kafiri wa uganda hatunae, kama ni yule wa butiama hatunae, kama ni abeid karume nae hatunae, wote hawa na others siku ya Qiyamah hukmu yao itatolewa.

Mwenyezi Mungu awarehemu waarabu/waislamu wote waliokufa katika mauwaji hayo.
 
Mkuu mimi ni Muislam.

Ila kigezo cha wapumbavu wachache kutumia dini kuwanyanyasa watu kisa rangi zao sikubaliani nao na hakuna hadith wala aya ya Quran tukufu inayopongeza hilo

Kama unadhani uislam ni kumwacha Sultan na washenzi wenzie kutawala Zanzibar huku wenyeji wengi waishi kama wako utumwani fikiria tena

Uislam umeweka bayana sheria za kutawala ardhi
 

Kwanini useme "mimi ni muislamu"!!! Kwanini usitoe hoja bila kujiita hivyo!! Na nitaamini vipi kama wewe ni ndugu yangu katika imani? Kuwa serious! Na inavyoonekana unasapoti huo upumbavu na ukatili uliofanywa na ndugu zako. Allah akuongoze mkuu
 
Ebu nisaidie kuwaelezea ndugu yangu Capone!!
 
Upo sahii kwa maoni yako mzee wangu kuhusu mapinduzi matukufu ya 1964 pale tawala za kidhalimu na tawala za kiimla zilipoondolewa zanzbar na watu wa matabaka yote kupata uhuru wa kweli bila kujali rangi zao na dini zao na asili zao!!
 

Ahsante sheikh wangu, Allah akulipe na akuongoze inshaallah
 
Una fact za uhakika brother kama msomi
 
Kwanini useme "mimi ni muislamu"!!! Kwanini usitoe hoja bila kujiita hivyo!! Na nitaamini vipi kama wewe ni ndugu yangu katika imani? Kuwa serious! Na inavyoonekana unasapoti huo upumbavu na ukatili uliofanywa na ndugu zako. Allah akuongoze mkuu
Mkuu mimi ni muislamu na silazimiki kujieleza kwanini nimeamua niseme na silazimiki kukuaminisha kivyovyote

Uislam wangu si kwaajili yako wewe Sol de Mayo , Uislamu wangu ni kwaajili ya Mungu yeye ndiye mwenye kujua kweli ya nafsi zetu mkuu ni yeye atakaenilipa kwa mema yangu atakaesamehe mabaya yangu na kama ataamua ataniadhibu

Wewe Sol de Mayo
Hunifai chochote mimi wala mimi sikufai kitu hivyo sijielezi walq kukuaminisha chochote kile


Ninasapoti Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliyong’oa tawala dhalimu ya sultan mkuu

Je watu wasio na hatia waliuawawa?
Of course waliuwawa

Ninahisi huzuni juu yao!?
Absolutely,

Sultan aliwaonea wtu wasio na hatia?
Absolutely aliwaonea

Karume na wenzie walifanya kitu sahihi mbali na mauaji ya wasio na hatia?
Absolutely walifanya jambo sahihi sana mbali na vifo vya wasio na hatia

Kuna kiongozi yoyote kafanya ya maana bila kuua watu?
No, hayupo hata mmoja

Unajua haya mambo kama hujui uongozi na hujui uhalisia wa ulimwengu utamchukia kila kiongozi

Allah atuongoze sote mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…