Bandiko lako namba moja lina ukweli kwa asilimia kubwa mno, lakini kuna sehemu hauko sawa. Ni hivi, hakuna mwanaccm yoyote alithubutu kumpinga Magufuli. Watu pekee walioweza kumpinga Magufuli ndani na nje ya bunge ni wapinzani, na viongozi wachache sana wa kidini tena wanahesabika. Hawa akina Slaa, Tibaijuka, Shivji nk walikuwa wameufyata, sio kwasababu waliona Magufuli yuko sahihi, ila walitaka waendelee kubaki hai kumsubiri rais mwingine wa kumkosoa, lakini sio Magufuli.
Wakati wa Magufuli hakukuwa na chombo chochote rasmi cha habari kilichothubutu kuandaa press, au mdahalo wa kujadili asichopenda Magufuli. Na baadhi ya online media au baadhi ya media chache zilizothubutu kuruhusu ukosoaji kwa Magufuli, zilifungiwa au kupewa adhabu kali, ikiwemo na kudhalilishwa na ushahidi upo wazi. Hao wanaosema kuwa kipindi cha Magufuli hakukosolewa kwa kiwango kikubwa wako sahihi, japo sio kuwa hakukosolewa kwa kuwa alikuwa sahihi, bali lile kundi lake la watu wasiojulikana lilifanya kazi yake vizuri ya kunyamazisha wakosoaji. Hata Magufuli kuanza kununua wapinzani kwenye ile siasa yake chafu ya kuunga mkono juhudi, ilikuwa ni kupunguza kukosolewa, na funga kazi ilikuwa ni kunajisi uchaguzi wa 2020 ili kuua rasmi ukosoaji kwenye bunge. Mitandao ya kijamii ndio pekee iliyofanikiwa kubaki kumkosoa Magufuli kwa kutumia fake ID bila kuumizwa. Lakini yoyote hasa wapinzani waliomkosoa waliuliwa, kutekwa, kuharibiwa sehemu zao za kuwaingizia vipato, kubambikiwa kesi na ukatili mwingine wa wazi kabisa.