Wanaodai Rais Magufuli hakuwa anapingwa ni waongo wakubwa

Toka hii serikali iitwe ni awamu ya sita ilikuwa ni dhahiri nia ya kujionesha ni serikali mpya si ile ya JPM. Tanzania awamu zinabadilika kwa uchaguzi tu! Ila propaganda ikashinda na wote tunaimba awamu ya sita!

Kwa yanayoendelea bora walijitenga na awamu ya tano. Shimo walilochimba wanadumbukia kama vipofu [emoji1787]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwanini nyie walipa kodi muamue leo mbona utawala uliopita ulikuwa "worse" zaidi na hamkuamua? Ila pia mkubaliane kuwa na tunaomuunga mkono Rais samia tupo nae mpaka kieleweke.
 
Ile awamu ya 5 ilikua na laana.
 
Hawa uliowataja ndio hao watu wachache sana waliothubutu kumkosoa Magufuli kwa gharama kubwa. Ila hawa watetezi wa Samia sasa,wanashangaa hata mabubu wa wakati wa Magufuli wanapata wapi uhalali, wakati walikalia kimya uovu wa wazi wa Magufuli?
Kikubwa alichofeli JPM ni kuzuia mikutano ya kisiasa baada ya uchaguzi. Lakini swala la wapingaji wa serikali kufanyiwa unyama tukisema ziwekwe list bampa to bampa awamu ya tano vs nne utashangaa.

Uzuri matukio yote yapo humu JF! Chuma kelele zilizidi sababu aligusa maslahi ya watu wazito ndani na nje ya nchi! Mwenzake JK hakugusa big fish!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwanini nyie walipa kodi muamue leo mbona utawala uliopita ulikuwa "worse" zaidi na hamkuamua? Ila pia mkubaliane kuwa na tunaomuunga mkono Rais samia tupo nae mpaka kieleweke.
Kuna Time Limitation ya Uamuzi wa Kufanya the Right Thing...

Anyway Binafsi Sijawahi kuwa Cheerleader wa Mtawala yoyote yule anapofanya vyema ni kazi yake akifanya ndivyo sivyo (in my humble opinion) sisiti kusema - Sina muda wa ku-practice Uchawa...
 
Sijasema Magufuli alikubali kukosolewa.

Nimesema naye alipingwa na kukosolewa na watu wengi tu.

Membe hakumpinga Magufuli?

Yule padri wa Kilutheri hakuwa anampinga Magufuli?

Magufuli naye alipingwa na wengi tu.
 
Tatizo ni CCM. Tatizo halikuwa Magufuli.

Na ndo maana hayo mambo ya unyama uliyoyataja yapo kwenye awamu zote.

Hata huyu Samia naye ni mvunja katiba tu.

Ni huyu huyu Samia naye alivunja katiba kwa kukataza mikutano ya kisiasa kwa kisingizio eti anataka kujenga uchumi kwanza.

Sasa mikutano imeruhusiwa. Ina maana uchumi ushajengeka?

Juzi hapa vijana walioandamana kupinga suala la DP World, wamepigwa virungu na kukamatwa.

Kosa lao ni lipi wakati katiba inaruhusu watu kuandamana kwa amani na kujieleza wajisikiavyo?

Samia naye atapingwa tu kama walivyopingwa wengine.

Hapendwi mtu hapa. Ni Tanzania, katiba, na utawala bora wa kisheria.

Kinyume na hapo, ni kumkoma nyani giladi tu.
 

Sio kuzuia tu mikutano ya kisiasa, bali ni kuua demokrasia nchini kwetu kwa ujumla wake, ikiwemo hata ndani ya chama chake cha mapinduzi. Kuua uhuru wa vyombo vya habari, kubwa kuliko yote ilikuwa ni kufubuza jumla mihimili yaani bunge na mahakama, na ameacha Mihimili hiyo ikiwa dhaifu mno, kiasi kwamba inatakiwa mabadiliko ya dhati kurejesha nguvu halisi ya mihimili hiyo.

Ni kweli Magufuli alikuta mifumo ikiwa na udhaifu, lakini yeye ndio aliweka bayana udhaifu wa mifumo hiyo, na akaonyesha wazi udhaifu wa mifumo yetu, na madaraka makubwa yasiyo na tija kwa rais. Kama ni kuweka hiyo bampa tu bampa ya mauaji ya watu awamu ya 4 vs 5 itakubidi urudi hadi ya kwanza.

Narudia tena, kama kilio cha madai ya katiba mpya, na kutazamwa upya kwa mipaka ya madaraka ya urais, basi kilio hicho kilionekana wazi wakati wa utawala wa Magufuli. Pale ndio kila mmoja alijua ni kwa kiwango gani madaraka ya cheo cha urais kwa mujibu wa katiba yetu ni ya hatari. Siku Magufuli alipokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi mchana kweupe huko Arusha, mbele ya CDF tena akiwa anatabasamu, huku jeshi likiwa limetengwa kabisa na siasa, ndio nilijua katiba yetu ni takataka.
 
Hawa uliowataja ndio hao watu wachache sana waliothubutu kumkosoa Magufuli kwa gharama kubwa. Ila hawa watetezi wa Samia sasa,wanashangaa hata mabubu wa wakati wa Magufuli wanapata wapi uhalali, wakati walikalia kimya uovu wa wazi wa Magufuli?
Mr Tindo mbona kuna wakosoaji wa kipindi cha Magufuli nao kipindi hiki wamekuwa mabubu, The boss Jf,Faizafox, Zito kabwe,January, Nape, Kinana late Membe n.k hii inahashilia kwwmba watu wanapigania mambo binafsi.
 
Mkuu Tindo Pata chips dume na mirinda nyeusi hapo kwa mangi!! Umeyakweka vizuri sana. Naona Nyani anataka kutulisha uwongo hapa. Sina nyongeza.

Ila tuendelee kukosoa hadi Mama Samia asikie kuhusu vifungu vya HOVYO vya mkataba wa Bandari
 
Mfano mtu anakomaa anasema heti bomba la mafuta pia walisaini IGa ,nikamuuliza bomba la mafuta sisi tumewekeza nini ,kwanza bomba la mafuta mbona hakuna mfanano na bandari, ndio maana Uganda alikua anaweza kuamua kupitisha popote Kenya au Tanzania
Watu kama nape na ndo huwa wanfananisha mambo yasio na mfanano hata kidogo
 
Sijasema Magufuli alikubali kukosolewa.

Nimesema naye alipingwa na kukosolewa na watu wengi tu.

Membe hakumpinga Magufuli?

Yule padri wa Kilutheri hakuwa anampinga Magufuli?

Magufuli naye alipingwa na wengi tu.

✔️
 
Magufuli alikuwa ni kichaa mwenye rungu. Ukimkosoa tu hasa kwenye Face Book utatafutwa mpaka wakukamate. Wakikukamata huku kuna watu hadharani itaishia kufunguliwa mashtaka ya kutakatisha fedha kama Eric Kabendera au Tito Magoti.

Wakikukamata bila mtu kukuona watakuua na kukuweka kwenye viroba kisha kukutupa baharini.

Hata mama Samia akiuza bandari najua ni suala la muda, akitoka madarakani tunairudisha fasta na tunaanza kupambana huko ICSD kama Djibouti. Lakini yule kichaa aliyekuwa anaua, aiua akina Ben Saanane au Azory huwezi kuwarudishia uhai tena
 
Aisee 🤔
 
1. Dr.Slaa alipinga lini?
2. Prof.Shivji alipinga lini?
3. Polepole alipinga lini?
4. Kadinali Pengo alipinga lini?.

N.k............... walipinga lini?.
 
Tatizo ni CCM sio Magufuli! Ndio maana hilo dude lina survive kila awamu maana linatupa Rais na kujenga upinzani wenyewe. Ndio maana nimesema walipo change awamu 5 kuwa 6 wengi walifurahi utafikiri chama kipya kimeingia! Sasa wote wanamgeuka baada ya kugundua ni mvinyo ile ile kwenye Kiriba?
 
Wewe Nyani ndiyo mwongo kwa kuwa una uwezo wa kula mahindi mabichi na kunya.

Waliompinga Magufuli hadharani walikipata cha moto. Kuna waliouliwa kama Ben Sanane, Azory na wale wa kwenye viroba baharini.

Kuna waliopigwa risasi na kujeruhiwa kama Tundu Lissu. Kuna waliohojiwa uraia kama Askofu Niiwemugizi na kuna walifunguliwa mashataka ya kutakatisha fedha kama Tito Magoti na Eric Kabedera.

Sisi wa humu JF tulimkosoa kwa fake ID kwa hisani ya Maxence Melo na tunajuwa ilimcost sana huyu protector wetu. Waliomkosoa Facebook walikuwa wanasakwa na kuuawa au kushtakiwa kwa sheria mbaya.
 
Sijasema Magufuli alikubali kukosolewa.

Nimesema naye alipingwa na kukosolewa na watu wengi tu.

Membe hakumpinga Magufuli?

Yule padri wa Kilutheri hakuwa anampinga Magufuli?

Magufuli naye alipingwa na wengi tu.
Zitto Alienda mbali hadi hadi tukanyimwa mkopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…