Wanaodaiwa kumteka mwanaharakati wa Tanzania wafikishwa mahakamani Nairobi

Wanaodaiwa kumteka mwanaharakati wa Tanzania wafikishwa mahakamani Nairobi

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Nairobi. Dereva raia wa Kenya, Nelson Wanjohi Kirika mkazi wa Kenya anayeishi nchini Afrika Kusini Edward Mwangi Mwai na Aziz Hama raia wa Tanzania, leo Machi 6 wamefikishwa mahakamani jijini Nairobi kwa tuhuma za kumteka nyara Mtanzania, Mshabaha Mshabaha Hamza na kumsababishia majeraha mabaya katika kaunti ya Machakos.

Taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wa X wa Manesty Kenya imesema, watuhumiwa hao walikana mashtaka hayo na kurejeshwa rumande.

"Ombi la dhamana na kesi itatajwa tarehe 9 Machi. Kenya haipaswi kamwe kuwa korido ya ukandamizaji wa kimataifa," imesema taarifa hiyo.

Amnesty ilisema katika taarifa ya Februari 24 kuwa Hamza, ambaye amekuwa uhamishoni nchini Kenya kwa takriban miaka minne, alikamatwa na kuingizwa kwenye gari Februari 21 na wanaume watatu.
Hamza alipambana na watekaji hao na akatupwa "akiwa amepoteza fahamu kutokana na madawa aliyopewa na kujeruhiwa" huko Lukenya katika kaunti ya Machakos.

Taarifa ya Amnesty ilisema Polisi walijitokeza mara moja na kukamata gari lililotumiwa na watekaji nyara hao.

Kwa mujibu wa Amnesty, washukiwa hao walikuwa wameahidiwa malipo ya kumpeleka Hamza kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania.
 
Wafuatilie mawasilaino yao , ikiwezekana kushirikiana na Watanzania ili hio chain ifahamike.
 
HAYA MAMBO YANATIA AIBU SERIKALI NA CHAMA CHAKE CHAKAVU CCM.
 
Back
Top Bottom