Bado Hujasema
Member
- Dec 1, 2024
- 12
- 14
Mimi ni mkazi wa Mfaranyaki, Kata ya Tungi, Manispaa ya Morogoro, mtaani kwetu tumechoshwa na matukio ya watu kupata majanga ikiwemo kupoteza Maisha katika eneo hilo la Mto Ngerengere uliokatisha Kata ya Tungi na Kihonda.
Mto huo umekuwa ni kero na tishio kutokana na watu kupoteza maisha wanapofanya shughuli za uvuvi na vifo eneo hilo, hiyo inatokana na kina kilichoongezeka katika mashimo yaliyochimbwa katika ndani ya mto wakati wa ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR.
Nakumbuka Disemba 16, 2024, Mwanaume anayekadiriwa kuwa na Umri wa Miaka 27, ambaye jina lake halijafahamika mkazi wa mtaa huo alipoteza maisha baada ya kutumbukia ndani ya Mto huo wakati akifanya shughuli ya uvuvi.
Kipindi cha Mwaka 2024 tayari inadaiwa jumla ya watu wanne wamepoteza maisha wakati wakiendelea na shughuli za uvuvi katika mto hali ambayo inatishia usalama wa watu wa eneo hilo hasa wanaofanya shughuli za uvuvi na kujipatia kipato.
Hali hii inatufanya kuwa na hofu katika eneo hili, hao ni watu wazima tunakuwa na hofu, watoto pia wanaweza kupoteza maisha maana kuna wengine wanakuja kucheza kando ya mto huo.
Nashauri Serikali kupitia watu wa Bonde Wami/Ruvu kwa kushirikiana na Manispaa ya Morogoro kuweka tahadhari juu ya uwepo wa kina kirefu maeneo hayo au kutafuta njia mbadala kutokana na watu kuendelea kutochukua tahadhari wakati wa shughuli za uvuvi jambo linalohatarisha usalama wa watu hao.
Wakati huohuo, umakini unatakiwa kuongezeka kwa wote wanaofanya shughuli zao maeneo hayo watambue kuwa kina ni kirefu tofauti na hali inavyoonekana kwa juu.