Umasikini, majukumu ya kifamilia,ukosefu wa ajira na watu kulinda masilahi yao waliyoyapata kabla ya kujitoa CCM na kujiunga upinzani, kwangu mimi ndizo hasa sababu kubwwa za wanasiasa kuhama upinzani na kujiunga CCM.
kuna wanaohama kwa kuahidiwa vyeo,matumaini ya kupata vyeo,kutafuta ajira,kutafuta fursa za kupitishwa na CCM kugombea katika uchaguzi mkuu wa baadae mwaka huu,n.k.
Lakini pia wapo wanaoamua kwenda CCM kutokana na sisi kama nchi kutokuwa na tume huru ya uchaguzi hivyo kugombea kupitia upinzani kwa sasa ni kama kupoteza muda kwani teyari kuna mtu anatuhumiwa kuwatisha watakaotangaza wapinzani washindi na tumeona yaliyotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni.
Ni wazi,CCM hii ingekuwa inafanya vizuri,basi hata wananchi wa kawaida tungewaona kwa mamia au maelefu wakijiunga CCM jambo ambalo halipo na CCM kwa kujua ukweli huu,ndio maana swala la tume huru wanalipinga.
Swali ni je,wanasiasa hawa wanaokimbilia CCM kwa masilahi yao binafsi wakikosa wanachokitarajia huko CCM,wataendelea kubaki huko na kuwa waaminifu?
Tukumbuke teyari kuna ambao walihamia huko na kupewa vyeo na wengine wanaendelea kuhamia huku kuna wana-CCM ambao nao wanasubiri uteuzi,n.k.
Swali ni je,itawezekana kuwaridhisha wote hawa?
Kwa mfano,watakaotoswa baada ya uchaguzi mkuu,wataendelea kubaki CCM?
Na wakibaki,hawatakuwa na vinyongo?
Je,political migration hii si hatari kwa CCM katika siku zijazo?
Je,huku sio kutengeneza "time bomb"?
Kuhama huku kunaisadia CCM kujiimarisha kisiasa au kuna fanya wananchi wapuuze siasa na wanasiasa wakiwemo wanasiasa wa CCM na chama chao chote kwa ujumla?
Time will tell.