Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Wakibadilisha maoni ya wajumbe wanaunda double-upinzani ndani ya chama na ule wa chadema sasa...hapo polisi watapata tabu sana....Nadhani na chadema unawafahamu wakipita sehemu hawakosi wafuasi ndio maana mkuu hawapendi hawa jamaa.
 
Yalikuwa ni mawazo mfu,ndio yaliyowafanya wateme big gii kwa karanga za kuonjeshwa.
Mwaka huu upinzani utapata majimbo mengi sana, kumbuka polisi hawatoshi kuwasaidia majimbo yote
 


Nafikiri sasa utakuwa umeelewa tulivyokuwa tunasema msitete kila kitu. Hakuna tume huru Tanzania ambayo ni shirikishi. Kushabikia hivi vitu vitatupeleka pabaya hasa baadae.
 
Ndg yangu ktk uzi wako huu umejitahidi sana kupindapinda lakini dhumuni lako ni ku-support au kufurahia ujio wa chama kimoja na kujipigia debe asa mungu anaweza kuingiza huruma si lazima maendeleo yaletwe na chama kimoja kama mfano wako wa china zipo nchi nyingi za vyama vingi zimeendelea lakini utambue maendeleo ya vitu hayana tija bila maendeleo ya watu nchi zote zilizoendele kwanza zilianza na maendeleo ya watu hata hivyo miaka mitano iliopita ilikuwa ni utawala wa chama kimoja ebu tupe maendeleo ya watu yaliopatikana kwa hoja hiyo bado hujatushawishi.
Pia umegusia ushindi wa uchaguzi kwa chama chenu hayo yanafahamika rejea chaguzi ndogo na serekali za mitaa usemi wa wahenga unaweza kumvuta mbuzi kwa kipindi kirefu lakini akiamua kukaa chini ni ama umuuwe au umbebe hatatoka hapo kwa miguu yake
Ni kweli unavyo hisi uchaguzi huu inawezekana tukarudi kwenye chama kimoja lakini inawezekana pia ikawa ni mwisho wa kuwa na chama kimoja fahamu maendeleo hayalazimishwi huja yenyewe kama yalivyo ktk nchi tulizopa nazo uhuru
 
Haya hakubalik [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hao watu waadilifu na wazalendo ili kulitumikia taifa option Ni kugombea kupitia CCM tu,? Vyama vingine vipi? Au umekariri ya mfumo wa chama kimoja
Mkuu Mliberali, trends za 2020 kwa huku bara, zinaelekeza ni CCM only and only CCM!.
Hata vigogo wa upinzani ikiwemo ile mibuyu, inapigwa chini!.
P
 
Bandiko hili ni angalizo nililitoa kitambo, kuwa wanaohamia CCM wasibezwe!. Makamanda waliokuwa Chadema na kuhamia CCM sasa ndio wanakwenda kuwa mwiba kwa upinzani
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…