Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Wanabodi.

Hili ni bandiko la swali kuhusu Trend Reading. Wanaohamia CCM Wasibezwe, Wanaona Mbali, 2020 Majimbo Yote Kurejeshwa?, Jee Tunarejea Kuwa Nchi Chama Kimoja?

Politics is a game of hide and seek and a changing variables, hivyo kwa mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, wanasiasa walioko upinzani, wenye uwezo wa kuona mbali kwa kusoma trends, wameishasoma mazingira yaliyopo na hali halisi ya siasa za upinzani nchini na their chances kuelekea 2020, hivyo wameamua kufanya uamuzi sasa kwa kujiunga CCM!.

Hivyo kwa hali hii, kama kuna mtu yoyote anataka kuwa na future kwenye politics za Tanzania kuelekea 2020, then atajiunga CCM!. Uthibitisho ni matokeo ya uchaguzi huu wa madiwani jinsi CCM ilivyotetea kata zake zote, na kukomba kata zote zilizokuwa zinasikiliwa na upinzani kasoro moja.

Hivyo kwa wanasiasa wanauojua kutazama mbali kwa kusoma trends, then CCM ndio mpango mzima, kama wanataka future ya politics kama ajira kukamata ulaji, chama cha kujiunga nacho ni CCM.

Hapa nazungumzia ukweli halisi ambao unaweza kuwa ni ukweli mtamu kwa CCM na ukweli mchungu kwa wapinzani, bila kujalisha kama Tume yetu ya Uchaguzi ni tume huru, au la, na kama chaguzi zetu ni changuzi huru na za haki, hapa mimi nazungumzia matokeo, kilichotokea, kilichopo, ni CCM imeshinda, bila kujalisha imeshindaje au kwa mbinu gani, mshindi ni mshindi tuu, the winner takes it all, na mshindi ni mshindi halali kwa kanuni ya the end justify the means.

Wapinzani poleni, CCM hongereni kuturudisha nchi ya chama kimoja.

Jumatatu Njema.

Paskali
Tukiwa wakweli na tuoipenda nchi hii, 2020 wala haguna haja ya kufanya uchaguzi ODDs zote zimeshazihilisha hilo, CCM ikishamaliza mchakato wa ndani wa kura ya maoni na kupitisha wagombea wake wote nchi nzima(udiwani,majimbo,urasi) basi hao ndio tume (NEC)iwatangaze washindi na iwaapishe basi.
HAPA TUTAKUWA TUMEONYESHA UKOMAVU WA AKILI NA KUWEZA KUFANYA MAMBO YETU WENYEWE KAMA TAIFA BILA KUJALI DUNIA ITASEMAJE (after all ccm lazima itashinda 100%) hebu tuwe wazalendo uchaguzu mkuu 2020 uishie ccm kwenye kura ya maoni, tutasevu mabilion ya hela zinazoweza kutumika kuleta maendeleo ya kweli na siyo maigizo ya uchaguzi
 
Kaka pascal ni ngumu sana kwa CCM kurudisha majimbo yote

Hali ya CCM ni mbaya sana, na Pamoja na Jitihada za Mtukufu Rais kumbambana na Ufisadi, Rushwa nk, lakini nachelea kusema kuwa HAKUBALIKI, sio ndani wala nje ya CCM, kwa jitihada alizozifanya mtukufu raisi ule uchaguzi wa madiwani wala CCM wasingefanya kampeni, lakini matokeo yake nguvu kubwa sana imetumika
Kwa nini nasema ni Vigumu CCM kurudisha majinbo
1: Mtukufu Rais itambidi apambane sana na Hali yake, uoinzani kutoka chamani na nje, so hatakiwa na muda wa kuwaangalia watu wa chini kama aliokuwa nao sasa
2: uchaguzi wa Zanzibar, msimu uliopita Lowassa aliwababaisha sana ikafikia kipindi wakaisahau Zanzibar na hatimae Hamad akajitangaza Mshindi (Asante Jecha), so uchaguzi ujao CCM hawawezi kamwe kuisahau Zanzibar
3: Chadema sasa ina Wapenzi wa chama waliopo Royal kwa kiasi fulani, na tunalipima hilo kwa sababu pamoja na kuondoka kwa Zitto, Slaa nk, bado Chadema iliweza kujikusanyia Wabunge wengi zaidi, na Madiwani wengi mpaka kupelekea kushika baadhi ya Halmashauri kwenye miji mikubwa
Hata kama CDM wafuasi wengi,kwani wanaotangaza matokeo ni wafuasi wa CDM? CDM Kura watapata nyingi tena Za kutosha kushinda lkn suala la kutangazwa mshindi ni jingine hilo.Huenda 2020 Wakatangazwa washindi wengi wa CCM
 
Mku Paskali unasahau Siasa ni Itikadi na kama zilivyo itikadi ni imani kamili kama zilivyo imani zingine. Ukiniambia mtu anahamusha Itikadi kwa ajili ya maslahi ya muda mfupi na kwa wachache huo unaliona hili liko sawa kweli. Wakati huo kumbuka mtu yuko pale kwa maslahi yake huwa yana ukomo wakati kinyang'anyiri kinakaribia hata hili vuguvugu unaloliona ni juu ya muda husika. Mtu mwenye njaa sio wa kuaminika ktk mambo endelevu
Ukiangalia wanasiasa wengi ni kuwa wanatumikia matumbo yao.Kwa Hali tulipofikia sitashangaa kuona Mnyika,Lema,Selasini,Mdee wamesepa kwenda ugambani
 
I was expecting thread ya ku-CONDEMN what has been done by CCM kwenye Uchaguzi wa jana..

Ushindi wao wala sio sign ya kwamba wanafanya siasa zao vema na kwamba uchaguzi wa 2020 wanakwenda kushinda majimbo yote na kuturudisha kwenye zama za chama kimoja, absolutely NO..

Fanya uchaguzi shinda FAIRLY there is no problem..

Lakini aina ya Uchaguzi wa jana sio wa kuusifia na kusema kwamba CCM wanakwenda kushinda kwa kishindo 2020...

Watu hawa wanafanya rafu zote kuhalalisha ushindi sio wa kuwasifia hata kidogo.
Paskali hajasifia ushindi wa Jana Ila kaona kuwa kwa Hali tuliyo nayo ni kama by any means lazima CCM washinde iwe kihalali au isiwe kihalali.Ila watashinda
 
Tye tye tye
Kwa ushauri mzuri kwao ni Mugabe wa Bongo aondoke kwenye Uenyekiti
kuwa mwenyekiti wa chama cha upinzani sio Utemi
Awape nafasi wengine
na chama kiwe na Wakosoaji
kiwe na hoja hai.
Pia wakumbuke Sio watanzania wote wapo Jf au Fb na Insta

CCM hoyeeeeee
Mugabe wetu hawezi ondoka kwenye tanuri la kuoka pesa!
Yeye na ruzuku, ruzuku na yeye.

Matokeo haya hayampi shida mfanyabiashara huyo.
 
Hata kama CDM wafuasi wengi,kwani wanaotangaza matokeo ni wafuasi wa CDM? CDM Kura watapata nyingi tena Za kutosha kushinda lkn suala la kutangazwa mshindi ni jingine hilo.Huenda 2020 Wakatangazwa washindi wengi wa CCM
Wakienda wao ni sawa lakini wafuasi wao bado wabaitikadi yao ukichanganya na madhila wanayoyapitia mambo kwao ni magumu
 
Vipi Sanduku la Kura limeamua kwa hiyari hilo ndiyo swali ulipaswa kuuliza..

Nguvu iliyotumika hakika inaonyesha jinsi jamaa wasivyo na uhakika wa kushinda kupitia sanduku la Kura...

Wanataka kuaminisha Wananchi eti wanakubalika lakini sivyo...

Weledi wameliona hilo...

Acheni Sanduku la Kura liamue matokeo...

Siyo hizi bla bla .....!!!
 
Kuna wanaoona mbali na wanaongalia Ugali....uzi wako unazuungumzia wanaoangalia Ugali

Wanaoona mbali (kama Lissu) hutumia upeo wao kukemea mambo kama haya ya kuminya demokrasia,kutumia mabavu kutawala il-hali wananchi wamewachoka watawala

Waache waikimbie njaa kwani njaa ni kitu kibaya kuliko lkn wajue ya kwamba Tanzania ni moja ya taifa ambalo linahitaji kujikomboa kutoka kwa watawala wake wasio na roho ya huruma...
 
Wanabodi.

Hili ni bandiko la swali kuhusu Trend Reading. Wanaohamia CCM Wasibezwe, Wanaona Mbali, 2020 Majimbo Yote Kurejeshwa?, Jee Tunarejea Kuwa Nchi Chama Kimoja?

Trend reading sio utabiri, bali ni matumizi ya analitical na logical thinking kwa kila jambo lililofanyika huangalii tuu jambo lililofanyika bali unajiuliza the motive behind jambo hili kufanyika jinsi hiyo lilivyofanyika na matokeo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu wa Jambo hili. Jambo letu kwenye uzi huu ni ushindi wa CCM kwenye uchaguzi wa marudio wa madiwani kata 43.

Politics is a game of hide and seek and a changing variables, hivyo kwa mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, wanasiasa walioko upinzani, wenye uwezo wa kuona mbali kwa kusoma trends, wameishasoma mazingira yaliyopo na hali halisi ya siasa za upinzani nchini na their chances kuelekea 2020, hivyo wameamua kufanya uamuzi sasa kwa kujiunga CCM!.

Hivyo kwa hali hii, kama kuna mtu yoyote anataka kuwa na future kwenye politics za Tanzania kuelekea 2020, then atajiunga CCM!. Uthibitisho ni matokeo ya uchaguzi huu wa madiwani jinsi CCM ilivyotetea kata zake zote, na kukomba kata zote zilizokuwa zinasikiliwa na upinzani kasoro moja.

Hivyo kwa wanasiasa wanauojua kutazama mbali kwa kusoma trends, then CCM ndio mpango mzima, kama wanataka future ya politics kama ajira kukamata ulaji, chama cha kujiunga nacho ni CCM.

Hapa nazungumzia ukweli halisi ambao unaweza kuwa ni ukweli mtamu kwa CCM na ukweli mchungu kwa wapinzani, bila kujalisha kama Tume yetu ya Uchaguzi ni tume huru, au la, na kama chaguzi zetu ni changuzi huru na za haki, hapa mimi nazungumzia matokeo, kilichotokea, kilichopo, ni CCM imeshinda, bila kujalisha imeshindaje au kwa mbinu gani, mshindi ni mshindi tuu, the winner takes it all, na mshindi ni mshindi halali kwa kanuni ya the end justify the means.

Wapinzani poleni, CCM hongereni kuturudisha nchi ya chama kimoja.

Jumatatu Njema.

Paskali
Rejea
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...
Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha ...

Jee Magufuli Anaimarisha CCM Au Anaua Upinzani?. Tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?. Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!.

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za ...
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...

Kwa momentum ya kisiasa iliyokuwepo sidhani kama hata hao wapinzani walitegemea kitu tofauti sana. its pity baada ya mika ishirini kwenye siasa za mfumo wa vyama vingi jamii yote imeaminishwa kuwa aina hii ya siasa haina mchango kwenye maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Wenye akili wamebaini ugonjwa mkubwa wa chama kikuu cha upinzani ni wao kujigeuza kuwa chombo cha utakatishaji wa mafisadi.
Ukiwa mchafu, hamia chadema...you will be washed and become as white as snow! Sad

Pia ukiwa changu hamia Chadema like Wema did na akapokelewa kwa mbwembwe kibao.
 
Wenye akili wamebaini ugonjwa mkubwa wa chama kikuu cha upinzani ni wao kujigeuza kuwa chombo cha utakatishaji wa mafisadi.
Ukiwa mchafu, hamia chadema...you will be washed and become as white as snow! Sad
Wajinga na wapumbavu ndio wanaoaminj ccm imeshinda kjhalali. Ukiukwajj wa haki ulikuwa wahali ya juu sana bika hata kificho. Hata kama mkijhamijiaminisha umeshinda . Lakini nafsini zenu zinawasufa.
 
Back
Top Bottom