Wanabodi.
Hili ni bandiko la swali kuhusu Trend Reading.
Wanaohamia CCM Wasibezwe, Wanaona Mbali, 2020 Majimbo Yote Kurejeshwa?, Jee Tunarejea Kuwa Nchi Chama Kimoja?
Trend reading sio utabiri, bali ni matumizi ya analitical na logical thinking kwa kila jambo lililofanyika huangalii tuu jambo lililofanyika bali unajiuliza the motive behind jambo hili kufanyika jinsi hiyo lilivyofanyika na matokeo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu wa Jambo hili. Jambo letu kwenye uzi huu ni ushindi wa CCM kwenye uchaguzi wa marudio wa madiwani kata 43.
Politics is a game of hide and seek and a changing variables, hivyo kwa mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, wanasiasa walioko upinzani, wenye uwezo wa kuona mbali kwa kusoma trends, wameishasoma mazingira yaliyopo na hali halisi ya siasa za upinzani nchini na their chances kuelekea 2020, hivyo wameamua kufanya uamuzi sasa kwa kujiunga CCM!.
Hivyo kwa hali hii, kama kuna mtu yoyote anataka kuwa na future kwenye politics za Tanzania kuelekea 2020, then atajiunga CCM!. Uthibitisho ni matokeo ya uchaguzi huu wa madiwani jinsi CCM ilivyotetea kata zake zote, na kukomba kata zote zilizokuwa zinasikiliwa na upinzani kasoro moja.
Hivyo kwa wanasiasa wanauojua kutazama mbali kwa kusoma trends, then CCM ndio mpango mzima, kama wanataka future ya politics kama ajira kukamata ulaji, chama cha kujiunga nacho ni CCM.
Hapa nazungumzia ukweli halisi ambao unaweza kuwa ni ukweli mtamu kwa CCM na ukweli mchungu kwa wapinzani, bila kujalisha kama Tume yetu ya Uchaguzi ni tume huru, au la, na kama chaguzi zetu ni changuzi huru na za haki, hapa mimi nazungumzia matokeo, kilichotokea, kilichopo, ni CCM imeshinda, bila kujalisha imeshindaje au kwa mbinu gani, mshindi ni mshindi tuu, the winner takes it all, na mshindi ni mshindi halali kwa kanuni ya the end justify the means.
Wapinzani poleni, CCM hongereni kuturudisha nchi ya chama kimoja.
Jumatatu Njema.
Paskali
Rejea
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...
Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha ...
Jee Magufuli Anaimarisha CCM Au Anaua Upinzani?. Tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?. Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?
Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!.
CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za ...
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible .
Ukiangalia kwa undani, wamehama/wanahama kwa ajili ya mslahi yao binafsi au wameshinikizwa. Hawana msaada wowote kwa wanachi wailo wachagua hata kwenye vyama walivyo hamia