Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

CUF ya Zanzibar hawana mbunge hata mmoja kule Zenji. Ipo au haipo?
 
Halafu is very unfortunate Mh. Rais haonyeshi kuumizwa na mabilioni yanayotumika kugharamia chaguzi za marudio.

Sijui inawezekanaje uchomwe sindano kalio moja uumie halafu ukichomwa kalio lingine isiume.

Historia itatoa hukumu sahihi siku inakuja.
 
Pascal..ni kweli usemalo.lakini upinzani wa Tanzania umekuwa Duni sana na wanachotakiwa kufanya ni kuubomoa mfumo wa uongozi wao na kuupika upya kila kitu huwa kina reform yake..sasa chama kimoja hakiwezi kuwa na mfumo mmoja kwa miaka 20..ccm ilikaribia kuangua endapo isingeshitukia hilo ..na ndiyo ilifanya mabadiliko makubwa ambayo yanaipa mafanikio ccm ya leo..
Wapinzani wetu walipofeli kuzitetea hoja zao hiyo nayo ni tatizo linalowafanya sasa wahahehahe.wasijue wanafuata msimamo upi.Ccm inazidi kujikaza na inazidi kukomaa .CCM ya 2010,2015 si CCM ya sasa..ndiyo maana kweli ninaungana na wewe kwamba upinzani unaelekea kufa na kufa huku kweli nchi inarudi kwenye chama kimoja.japokuwa vipo vyama vidogo ambavyo vitashawishiwa hata kwa kubebwa ili viwepo kuonyesha kuna upinzani tanzania..Lakini kufa kwa Chadema,NCCR,ACT na CUF utaipeleka CCM kuongoza kwa miaka mingi sana kabla hivi vyama havijajipanga upya.
 
Hata Julius Mtatiro asibezwe kujitoa CUF na kujiunga CCM, ameona mbali.

P.
Mtatiro akiwa Cuf (na haswa katika lile dubwana la ukawa) kabaniwa fursa nyingi tena bila huruma wala mafao mbadala.
Angeshakuwa mbunge siku nyingi kama sio zile ghilba katika kambi ya upinzani.
Wakati umefika ajaribu bahati yake kwingine
 

Ukweli wa bandiko hili, unaendelea kusimama, kuna vitu watu tunasema humu, hatueleweki, ila baada ya uchaguzi wa 2020, ndipo kuna watu watalielewa bandiko kama hili!.
Chadema poleni, CCM, hongereni!.
P.
 
Chaguzi ndogo zilizofanyika zimetosha kutoa picha ya uchaguzi mkuu 2020. Kwa mtazamo wangu kwa yanayoendelea na yanayofanyika itakuwa ngumu sana mbunge wa upinzani kutoboa 2020 kama hawatafanya mabadiriko yanayohitajika
Huu ni ukweli mchungu, hiki ndicho nilichokizungumza kwenye bandiko hili
P
 
Naendelea kusisitiza hawa wanaohama wasibezwe, kwanza ni haki yao, pili wanahoja za msingi, na tatu wameona mbali kuwa 2020, hakuna mpinzani atarudi bungeni, hivyo kuliko kusubiri 2020 upotee, wameamua bora wajihakikishie nafasi mapema, na kichocheo cha kuhama ni ile ile rushwa ya ahadi, ukihama, tutakusimamisha wewe.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums
P.
 
Aliyekuwa diwani wa kata ya Kabila wilayani Magu mkoa wa Mwanza, Ndugu Edward James Kihamba amejiuzulu udiwani na nafasi zote ndani ya chama na kujiunga na chama cha mapinduzi ccm.
Taifa ndipo lilipofikia.
Naendelea tuu kuusisitiza huu wito wangu kwenye bandiko hili, hawa watu wasibezwe!.

P.
 
Dah...[emoji13]
 
Mkuu, kwanza niseme kuwa tunarejeshwa na sio tunarejea chama kimoja. ni kweli 2020 utakuwa mgumu kwa upinzani na hili halitokani na uzembe wa upinzani bali great force kutoka mahaali na mtu fulani na sio hali.
Kitakachofanya upinzani ushindwe 2020 ni kuwa wapiga kura watakuwa wachache sana na wataipigia CCM.
sababu ni force kubwa ya sasa against opposition. kinachotoke sasa ni kama maskini na tajiri wanaoenda kumchumbia binti katika nyumba inayoshobokea utajiri na sio mapenzi ya dhati. katika hali kamaa hii tajiri atachukua mke maskini atabaki kukodoa macho!
hali ni mbaya sana pale wapiga kura wanaposema na kuamini kuwa hakuna haja ya kupiga kura kwa sababu mshindi anajulikana.ujue hao wengi ni wale wanaopigia upinzani.
Cha kufanya ni kupambana kuondoa hii false belief na kuhakikisha watu wengi watapiga kura. short of that upinzani unaweza kufa kabisa hadharani na kubaki tu ndani ya mawazo ya watu.
Watu wamekata tamaa na si kwamba kwa kukata tamaa basi wanaipende ccm na wakubwa zake. Noooo! Hii hali ya watu kukata tamaa ni kifo kwa demokrasia and it is very dangerous to the health of our nation!
Kurudi kwa madiwani na wabunge CCM is more a drama than a reality!
Kawaida walitakiwa warudi wanachama na sio viongozi! Kiuhalisia tulipaswa kusikia idadi ya wanachama kadhaa mahali fulani wamerudi CCM na sio viongozi wao
Wengine watasema mbona wa ccm wanaenda upinzani bila kjua kuwa aliyekuwemo ndani ndiye hutoroka na sio wa nje atoroke! Hapa kwetu ndani ni ccm na Opposition ni nje. wanaotoroka na kurudi ni walafi tu na tena ni ma opportunists kwani huangalia ni wapi wata survive bila kujali waliowachagua wanawaza nini!
Sorry for too many words.
 
Ameshabainisha wazi kabisa, ana sera zake ambazo zitafanya kazi wakati wa kipindi chake kwa lazima. Lakini awamu ya 6, sera hizo zinaweza kubadilishwa kwa matakwa wa kiongozi atakaekuwepo wakati huo. Kwa mfano kufuta uzazi wa mpango. Amesema wazi kuwa kipindi chake watu wazaliane tu kwa uwezo wao (mbegu si zipo kiunoni). Lakini akija mwingine si lazima kufuata.
Hali kadhalika katika mpango wa kutaka chama kimoja kitawale ndo nia na dhumuni lake kubwa hilo. Akija mwingine ktk awamu ya 6 aendelee na vyama vingi vyake kama atapenda.
Hii pia inampa nafasi ya kuongeza muda wake wa kuwa Rais zaidi ya 10yrs ili aendelee kutesa umma wa watanzania. Manake bunge litakuwa ccm na wabunge wake ndo waoga kama yule mnyama wa porini.
Hii miaka 8 tu iliyobaki kisheria ni mzigo kwetu. Tunaona kama dunia imeacha kuzunguka. Saa hazitembei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…