Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Hama hama inaendelea, leo ni Mbunge wa jimbo la Liwale(CUF) Zuberi Kuchauka atangaza kujiuzulu na kuhamia CCM.

Tusimlaumu kwa lolote kwa sababu ameona mbali, nawahurumia tuu Watanzania masikini wa kutupwa, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea ambao ni miongoni watakaogharimia uchaguzi huu wa marudio.

P.
CUF ya Zanzibar hawana mbunge hata mmoja kule Zenji. Ipo au haipo?
 
Hama hama inaendelea, leo ni Mbunge wa jimbo la Liwale(CUF) Zuberi Kuchauka atangaza kujiuzulu na kuhamia CCM.

Tusimlaumu kwa lolote kwa sababu ameona mbali, nawahurumia tuu Watanzania masikini wa kutupwa, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea ambao ni miongoni watakaogharimia uchaguzi huu wa marudio.

P.
Halafu is very unfortunate Mh. Rais haonyeshi kuumizwa na mabilioni yanayotumika kugharamia chaguzi za marudio.

Sijui inawezekanaje uchomwe sindano kalio moja uumie halafu ukichomwa kalio lingine isiume.

Historia itatoa hukumu sahihi siku inakuja.
 
Pascal..ni kweli usemalo.lakini upinzani wa Tanzania umekuwa Duni sana na wanachotakiwa kufanya ni kuubomoa mfumo wa uongozi wao na kuupika upya kila kitu huwa kina reform yake..sasa chama kimoja hakiwezi kuwa na mfumo mmoja kwa miaka 20..ccm ilikaribia kuangua endapo isingeshitukia hilo ..na ndiyo ilifanya mabadiliko makubwa ambayo yanaipa mafanikio ccm ya leo..
Wapinzani wetu walipofeli kuzitetea hoja zao hiyo nayo ni tatizo linalowafanya sasa wahahehahe.wasijue wanafuata msimamo upi.Ccm inazidi kujikaza na inazidi kukomaa .CCM ya 2010,2015 si CCM ya sasa..ndiyo maana kweli ninaungana na wewe kwamba upinzani unaelekea kufa na kufa huku kweli nchi inarudi kwenye chama kimoja.japokuwa vipo vyama vidogo ambavyo vitashawishiwa hata kwa kubebwa ili viwepo kuonyesha kuna upinzani tanzania..Lakini kufa kwa Chadema,NCCR,ACT na CUF utaipeleka CCM kuongoza kwa miaka mingi sana kabla hivi vyama havijajipanga upya.
 
Hata Julius Mtatiro asibezwe kujitoa CUF na kujiunga CCM, ameona mbali.

P.
Mtatiro akiwa Cuf (na haswa katika lile dubwana la ukawa) kabaniwa fursa nyingi tena bila huruma wala mafao mbadala.
Angeshakuwa mbunge siku nyingi kama sio zile ghilba katika kambi ya upinzani.
Wakati umefika ajaribu bahati yake kwingine
 
Wanabodi.

Hili ni bandiko la swali kuhusu Trend Reading. Wanaohamia CCM Wasibezwe, Wanaona Mbali, 2020 Majimbo Yote Kurejeshwa?, Jee Tunarejea Kuwa Nchi Chama Kimoja?

Trend reading sio utabiri, bali ni matumizi ya analitical na logical thinking kwa kila jambo lililofanyika huangalii tuu hilo jambo lililofanyika bali bali unaliangalia kwa kujiuliza the motive behind jambo hili kufanyika jinsi hiyo lilivyofanyika ni nini? na matokeo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu wa jambo hili ni nini?, ndipo unakuja na conclusion kama hii.

Jambo letu kwenye uzi huu ni ushindi wa CCM kwenye uchaguzi wa marudio wa madiwani kata 43.

Politics is a game of hide and seek and the changing variables, hivyo kwa mazingira ya sasa ya siasa za Tanzania ya Magufuli, wanasiasa karibu wote walioko upinzani, with very few exceptions, wenye uwezo wa kuona mbali kwa kusoma trends za kisiasa kwa kuangalia mwelekeo wa 2020, kwa matokeo haya, watakuwa wameishasoma mazingira yaliyopo na hali halisi ya siasa zetu za Tanzania na siasa za upinzani nchini katika kipindi hiki cha Tanzania ya Magufuli na their chances ya upinzani kushinda kata yoyote au jimbo lolote kuelekea 2020, hivyo, wenye kuona mbali, wameamua kufanya uamuz wa mapema kwa kuvihama vyama vyao sasa kwa kujiunga CCM!, ili ku secure their positions mapema badala ya kusubiri kifo hiyo 2020!

Hivyo kwa hali hii, kama kuna mtu yoyote anataka kuwa na future kwenye politics za Tanzania kuelekea 2020, then mtu huyo, atajiunga CCM now!. Uthibitisho ni matokeo ya uchaguzi huu wa madiwani wa kata 4 kwa jinsi CCM ilivyotetea kata zake zote, na kukomba kata zote zilizokuwa zinasikiliwa na upinzani kasoro moja.

Hivyo kwa wanasiasa wanauojua kutazama mbali kwa kusoma trends, then siasa za Tanzania kwa sasa, CCM ndio mpango mzima!, kama kuna mwanasiasa yoyote, au wowote, wanataka future ya politics kama ajira yao ya kudumu na kukamata ulaji, kujitafunia keki ya taifa, chama cha kujiunga nacho ni CCM!.

Hapa nazungumzia ukweli halisi wa kitu kilichopo, ambao unaweza kuwa ni ukweli mtamu kwa CCM na ukweli mchungu kwa wapinzani, bila kujalisha kama Tume yetu ya Uchaguzi ni tume huru, au la, na kama chaguzi zetu ni changuzi huru na za haki, hapa mimi nazungumzia matokeo ya mwisho tuu, ya kitu kilichotokea, ambacho ndicho kilichopo, ni CCM imeshinda!, bila kujalisha imeshindaje au imeshinda kwa mbinu gani, ziwe ni mbinu halali au haramu, CCM imeshinda kihalali kwa kufanya siasa safi, au kiharamu kwa kubebwa na wasimamizi wa uchaguzi, au upinzani umeshindwa kihalali kutokana na udhaifu wa kukosekana upinzani imara, ama upinzani umechezewa faulo za waziwazi, hapa mimi nazungumzia matokeo ya mwisho ya mshindi ni nani.

Aliyetangazwa mshindi ndiye aliyeshinda, na mshindi ni mshindi tuu, the winner takes it all, the looser standing small, aliyeshinda kashinda, ndiye mshindi na ni mshindi halali kwa mujibu wa kanuni ya "the end justify the means".

Wapinzani poleni sana!, CCM hongereni sana kwa ushindi huu, na hongereni kubwa in advance kwa chaguzi nyingine ndogo zitakazo fuatia, na hongera kubwa zaidi in advance ni hongera ya uchaguzi wa 2020 kwa Tanzania kuendelea kuitwa ni nchi ya vyama vingi jina tuu, lakini actually ni CCM hongera sana kuturudisha kuwa ni nchi ya chama kimoja cha siasa, CCM.

Jumatatu Njema.

Paskali
Rejea
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...
Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha ...

Jee Magufuli Anaimarisha CCM Au Anaua Upinzani?. Tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?. Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!.

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za ...
Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...

Ukweli wa bandiko hili, unaendelea kusimama, kuna vitu watu tunasema humu, hatueleweki, ila baada ya uchaguzi wa 2020, ndipo kuna watu watalielewa bandiko kama hili!.
Chadema poleni, CCM, hongereni!.
P.
 
Chaguzi ndogo zilizofanyika zimetosha kutoa picha ya uchaguzi mkuu 2020. Kwa mtazamo wangu kwa yanayoendelea na yanayofanyika itakuwa ngumu sana mbunge wa upinzani kutoboa 2020 kama hawatafanya mabadiriko yanayohitajika
Huu ni ukweli mchungu, hiki ndicho nilichokizungumza kwenye bandiko hili
P
 

Mbunge wa jimbo la Serengeti kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Marwa Ryoba Chacha amejivua uanachama wa chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) muda mfupi uliopita kwa kile alichodai kuunga mkono juhudi za Mhe. John Pombe Magufuli katika kuwaletea wananchi wa Tanzania maendeleo.

Amesema hajashurutishwa na yeyote kuchukua maamuzi haya.

Marwa amewasihi wana Serengeti kumchagua wanayeona anafaa, anayeunga mkono juhudi za Mhe. Rais Magufuli katika kuleta maendeleo.

Akitangaza kujivua uanachama amesema,

Mimi Marwa Ryoba Chacha, mbunge wa jimbo la Serengeti na mwanachama wa CHADEMA, leo tarehe 27/08/2018 nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushinikizwa na mtu yeyote kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi. Nawaomba wananchi wa Serengeti, mlinipa imani kubwa ya kuwatumikia lakini imefikia sehemu kupitia CHADEMA naona kama siwatendei haki.

Nimeamua nijivue uanachama na kujinga na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za maendeleo ambazo anazifanya Rais Magufuli. Niwaombe wananchi wa Serengeti, nafasi ipo kwenu chagueni mtu mnayemuona anawafaa kuwawakilisha ambaye ataungana na Rais Magufuli kuwaletea maendeleo.
Asanteni sana.


VIDEO:


Naendelea kusisitiza hawa wanaohama wasibezwe, kwanza ni haki yao, pili wanahoja za msingi, na tatu wameona mbali kuwa 2020, hakuna mpinzani atarudi bungeni, hivyo kuliko kusubiri 2020 upotee, wameamua bora wajihakikishie nafasi mapema, na kichocheo cha kuhama ni ile ile rushwa ya ahadi, ukihama, tutakusimamisha wewe.
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums
P.
 
Aliyekuwa diwani wa kata ya Kabila wilayani Magu mkoa wa Mwanza, Ndugu Edward James Kihamba amejiuzulu udiwani na nafasi zote ndani ya chama na kujiunga na chama cha mapinduzi ccm.
Taifa ndipo lilipofikia.
Naendelea tuu kuusisitiza huu wito wangu kwenye bandiko hili, hawa watu wasibezwe!.

P.
 
Kaka pascal ni ngumu sana kwa CCM kurudisha majimbo yote

Hali ya CCM ni mbaya sana, na Pamoja na Jitihada za Mtukufu Rais kumbambana na Ufisadi, Rushwa nk, lakini nachelea kusema kuwa HAKUBALIKI, sio ndani wala nje ya CCM, kwa jitihada alizozifanya mtukufu raisi ule uchaguzi wa madiwani wala CCM wasingefanya kampeni, lakini matokeo yake nguvu kubwa sana imetumika
Kwa nini nasema ni Vigumu CCM kurudisha majinbo
1: Mtukufu Rais itambidi apambane sana na Hali yake, uoinzani kutoka chamani na nje, so hatakiwa na muda wa kuwaangalia watu wa chini kama aliokuwa nao sasa
2: uchaguzi wa Zanzibar, msimu uliopita Lowassa aliwababaisha sana ikafikia kipindi wakaisahau Zanzibar na hatimae Hamad akajitangaza Mshindi (Asante Jecha), so uchaguzi ujao CCM hawawezi kamwe kuisahau Zanzibar
3: Chadema sasa ina Wapenzi wa chama waliopo Royal kwa kiasi fulani, na tunalipima hilo kwa sababu pamoja na kuondoka kwa Zitto, Slaa nk, bado Chadema iliweza kujikusanyia Wabunge wengi zaidi, na Madiwani wengi mpaka kupelekea kushika baadhi ya Halmashauri kwenye miji mikubwa
Dah...[emoji13]
 
Mkuu, kwanza niseme kuwa tunarejeshwa na sio tunarejea chama kimoja. ni kweli 2020 utakuwa mgumu kwa upinzani na hili halitokani na uzembe wa upinzani bali great force kutoka mahaali na mtu fulani na sio hali.
Kitakachofanya upinzani ushindwe 2020 ni kuwa wapiga kura watakuwa wachache sana na wataipigia CCM.
sababu ni force kubwa ya sasa against opposition. kinachotoke sasa ni kama maskini na tajiri wanaoenda kumchumbia binti katika nyumba inayoshobokea utajiri na sio mapenzi ya dhati. katika hali kamaa hii tajiri atachukua mke maskini atabaki kukodoa macho!
hali ni mbaya sana pale wapiga kura wanaposema na kuamini kuwa hakuna haja ya kupiga kura kwa sababu mshindi anajulikana.ujue hao wengi ni wale wanaopigia upinzani.
Cha kufanya ni kupambana kuondoa hii false belief na kuhakikisha watu wengi watapiga kura. short of that upinzani unaweza kufa kabisa hadharani na kubaki tu ndani ya mawazo ya watu.
Watu wamekata tamaa na si kwamba kwa kukata tamaa basi wanaipende ccm na wakubwa zake. Noooo! Hii hali ya watu kukata tamaa ni kifo kwa demokrasia and it is very dangerous to the health of our nation!
Kurudi kwa madiwani na wabunge CCM is more a drama than a reality!
Kawaida walitakiwa warudi wanachama na sio viongozi! Kiuhalisia tulipaswa kusikia idadi ya wanachama kadhaa mahali fulani wamerudi CCM na sio viongozi wao
Wengine watasema mbona wa ccm wanaenda upinzani bila kjua kuwa aliyekuwemo ndani ndiye hutoroka na sio wa nje atoroke! Hapa kwetu ndani ni ccm na Opposition ni nje. wanaotoroka na kurudi ni walafi tu na tena ni ma opportunists kwani huangalia ni wapi wata survive bila kujali waliowachagua wanawaza nini!
Sorry for too many words.
 
Ameshabainisha wazi kabisa, ana sera zake ambazo zitafanya kazi wakati wa kipindi chake kwa lazima. Lakini awamu ya 6, sera hizo zinaweza kubadilishwa kwa matakwa wa kiongozi atakaekuwepo wakati huo. Kwa mfano kufuta uzazi wa mpango. Amesema wazi kuwa kipindi chake watu wazaliane tu kwa uwezo wao (mbegu si zipo kiunoni). Lakini akija mwingine si lazima kufuata.
Hali kadhalika katika mpango wa kutaka chama kimoja kitawale ndo nia na dhumuni lake kubwa hilo. Akija mwingine ktk awamu ya 6 aendelee na vyama vingi vyake kama atapenda.
Hii pia inampa nafasi ya kuongeza muda wake wa kuwa Rais zaidi ya 10yrs ili aendelee kutesa umma wa watanzania. Manake bunge litakuwa ccm na wabunge wake ndo waoga kama yule mnyama wa porini.
Hii miaka 8 tu iliyobaki kisheria ni mzigo kwetu. Tunaona kama dunia imeacha kuzunguka. Saa hazitembei
 
Back
Top Bottom