Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Nani alikudanganya Kuwa Hao wanaohamia CCM 2020 watapitishwa kwenye Kura za Maoni?? Kuna wafia Chama Wanawalia Timing Kinoma.
 
CCM haina sifa ya kulea vigeugeu, hicho wanachopewa in chambo. Jana walikuwa CCM tukawashobokea ,wengi wakiwa hawana uwezo lkn kwa kuwa walibebwa kwa musuli za wazee na chama kukawachagua, baadae wakahama bado tukawashobokea, wakiwa CCM waliwatusi na kuwabeza wapinzani, walipoenda upinzani wameitusi na kuibeza CCM ati sasa wanarudi CCM wanawabeza wapinzani.Hivi kweli wao ni nani tuendelee kuwashobokea? CCM INA watu makini 2020 wataula wa chuya, hizi ni mbinu za hali ya juu,wanatumika kama toilet paper.Wengi hatuna vyama tukienda kupiga kura tunaangalia candidates, quality ya candidates ni moja ya sababu zinazochangia wananchi kutojitikeza kupiga kura.Utadamka asubuhi kwenda kumpigia kura MTU unayemwamini na kumheshimu
 
The exodus inaendelea, this time Nimezisoma sababu zake, ana hoja za msingi, asibezwe na hoja zake zisipuuzwe, kuna vitu vikubwa, vibaya, vichafu amevieleza hapa kwa just mention, bila kuvitaja, lakini kama vitu hivi ni kweli, then, wabunge wanawake wa Chadema, ni mashujaa sana, ni wavumilivu sana na wastahimilivu sana kwa vitu wanavyofanyiwa na viongozi wao, huyu ameshindwa kuvumilia, uvumilivu umemshinda, japo amewastahi lakini amesema katika mabano na hapa ninamnukuu "iliniuma sana pale nilipokataa kuwaabudia viongozi wa chama kitaifa kwa namna itakayo tweza utu wangu" Jee unakujua huko kuabudiwa kunakotweza utu wa mwanamke?.
pia kama mtu mwenyewe ni huyu
View attachment 897540
Na eneo analotoka ni Babati, then kiukweli kabisa, huyu ni shujaa, kwa sababu vitu vingine, na mambo mengine, sisi wengine wenu wenye udhaifu nayo, hata ningekuwa mimi...

Kama tuhuma hii ni kweli, hii inamaana wabunge wengine wanawake wa Chadema, wanavumilia sana.

Hivyo naendelea kusisitiza

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike - JamiiForums

P.
 
Kusema kweli ametoa hoja za msingi tena kwa marefu na mapana, kwanini anahama chadema na kwenda ccm,
 
Unahalalisha haramu?.. Eti alieshinda kashinda tu and unashabikia ujangilii huu??
 
Unahalalisha haramu?.. Eti alieshinda kashinda tu and unashabikia ujangilii huu??
Kujiunga na chama chochote cha siasa ni hiyari, kujitoa pia ni hiyari na kujiunga na chama kingine chochote, pia ni hiyari.

Kwa watu wanaojua kusoma trends kuelekea 2020, CCM ndio mpango mzima.
P
 
Mkuu Nguruvi3, mimi bado ninaamini, kila anayehama ana sababu, hata kama sababu yenyewe ni ile rushwa tuu ya ahadi ya kusimamishwa tena, nayo ni sababu tosha. Hata kama ni fear of unknown kwa hatma ya upinzani 2020 ni sababu kama nilivyoeleza kwenye bandiko hili.

Ila pia kuna wahamiaji wengine ni very genuine, wakati wanahana wanaandika barua kwa vyama vyao na wanatoa sababu, nilishauri, hawa wasipuuzwe wana hoja za msingi.
CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike - JamiiForums
P
 
Wana sababu kabisa binfasi ambazo ni kuijiandalia hatima njema lakini itakuwa ni shughuli kwao..
Halafu Mbona hamuelezi Upinzani unaokufa ni upi ? wa agenda IPI ?

Madhalani hoja ya Ufisadi mbona haijafanyiwa kazi na wanaoongoza.?
Eleza Ufisadi uliofanyiwa kazi nami nitakuelewa .

Mtu aliyewahi kugombea hata ujumbe ;anayejua kura zinapatikanje; mpaka sasa haoni Ccm iliyosimama Kwa miaka mitano !
 
Ndugu yangu Paskali, umejadili hoja nzito lakini umeitendea haki. Umejadili kisayansi japo uandishi wako wa kuchanganya kishwahili na kiingereza huwa haunipi raha ila naona wewe unakupa wepesi. Nimekuwa msomaji mahiri wa hekaya zako na kwa hiyo mimi ni mfuatilaji mzuri wa kila unachokiandika. Kuna nyakati unaniudhi na kuna nyakati unanifurahisha. Maneno uliyoyatumia leo tena kwa lugha ya kiswahili yamenivutia sana haya " Ukweli mchungu" kwa wapinzani.

Nimeumia kwa kiwango kile kile cha uchungu wa shubiri, lakini nikawaonea huruma watanzania kwa sababu shubiri hii wataionja kwa zaidi ya miaka mingi ijayo.
Kama unakiona ninachoimanisha, niaze kwa kuwaomba nyinyi waandishi mahiri, anzeni kuielezea shubiri ijayo kwa watanzania hasa baada ya 2020.

Kipindi cha mwisho cha utawala wa Mhe. Kikwete nilikuwa naiona tanzania ilikuwa ikielekea Nigeria na Nigeria ikielekea Somalia. Sasa naiona Tanzania ikielekea Zimbabwe ya Mzee shujaa Robert Mugabe; vile vile naziona Nigeria na Zimbabwe zinaelekea Tanzania. Ubadilishanaji huu hauna tija kwa watanzania. Hivi wasomi hamlioni hili?
Pamoja na ukweli mchungu uliousema nitabaki upinzani na nitajitahidi kusema kwa nguvu zangu zote kuhusu "ukweli mchungu" utakaowakabiri watanzania wenzangu endapo hatutasimama na kuwatahadharisha.
 
Mkuu Mechard Rwizile, kwanza asante kwa kuwa msomaji wangu mzuri. Sisi waandishi kazi yetu ni kuona na kuandika tuu, kuna kitu nimekiandika kwenye bandiko hili kuhusu uchaguzi Mkuu wa 2020 ambacho kitatanguliwa na matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, matokeo ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa ndio utawafungua macho watu wengi na ndio sasa watalielewa bandiko langu hili linazungumzia nini kuhusu matokeo ya uchaguzi Mkuu wa 2020.
P
 
Naendelea tuu kusisitiza, hawa watu wanaohamia CCM, wasibezwe!, wanaona mbali!.
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…