Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Nani alikudanganya Kuwa Hao wanaohamia CCM 2020 watapitishwa kwenye Kura za Maoni?? Kuna wafia Chama Wanawalia Timing Kinoma.
 
CCM haina sifa ya kulea vigeugeu, hicho wanachopewa in chambo. Jana walikuwa CCM tukawashobokea ,wengi wakiwa hawana uwezo lkn kwa kuwa walibebwa kwa musuli za wazee na chama kukawachagua, baadae wakahama bado tukawashobokea, wakiwa CCM waliwatusi na kuwabeza wapinzani, walipoenda upinzani wameitusi na kuibeza CCM ati sasa wanarudi CCM wanawabeza wapinzani.Hivi kweli wao ni nani tuendelee kuwashobokea? CCM INA watu makini 2020 wataula wa chuya, hizi ni mbinu za hali ya juu,wanatumika kama toilet paper.Wengi hatuna vyama tukienda kupiga kura tunaangalia candidates, quality ya candidates ni moja ya sababu zinazochangia wananchi kutojitikeza kupiga kura.Utadamka asubuhi kwenda kumpigia kura MTU unayemwamini na kumheshimu
 
The exodus inaendelea, this time
Mbunge wa Babati Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Manyara na Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Kanda ya Kaskazini Pauline Gekul amejivua uanachama wa Chadema, na kujiuzulu nafasi zote za uongozi alizokuwa nazo usiku huu na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM).
_
Gekul ametaja sababu mbili za kufanya maamuzi hayo. Ya kwanza ni chama kuwabebesha wabunge mzigo shughuli za ujenzi wa chama. Anasema kwenye chaguzi ndogo zote zilizofanyika Manyara alitoa fedha zake mfukoni kugharamia, na chama kilileta laki tano tu, licha ya kwamba kinapokea ruzuku ya zaidi ya milioni 300 kwa mwezi. Pili amesema ni kupigwa majungu na viongozi wenzie wa Chadema.!
Nimezisoma sababu zake, ana hoja za msingi, asibezwe na hoja zake zisipuuzwe, kuna vitu vikubwa, vibaya, vichafu amevieleza hapa kwa just mention, bila kuvitaja, lakini kama vitu hivi ni kweli, then, wabunge wanawake wa Chadema, ni mashujaa sana, ni wavumilivu sana na wastahimilivu sana kwa vitu wanavyofanyiwa na viongozi wao, huyu ameshindwa kuvumilia, uvumilivu umemshinda, japo amewastahi lakini amesema katika mabano na hapa ninamnukuu "iliniuma sana pale nilipokataa kuwaabudia viongozi wa chama kitaifa kwa namna itakayo tweza utu wangu" Jee unakujua huko kuabudiwa kunakotweza utu wa mwanamke?.
pia kama mtu mwenyewe ni huyu
View attachment 897540
Na eneo analotoka ni Babati, then kiukweli kabisa, huyu ni shujaa, kwa sababu vitu vingine, na mambo mengine, sisi wengine wenu wenye udhaifu nayo, hata ningekuwa mimi...

Kama tuhuma hii ni kweli, hii inamaana wabunge wengine wanawake wa Chadema, wanavumilia sana.

Hivyo naendelea kusisitiza

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike - JamiiForums

P.
 
The exodus inaendelea, this time Nimezisoma sababu zake, ana hoja za msingi, asibezwe na hoja zake zisipuuzwe, kuna vitu vikubwa, vibaya, vichafu amevieleza hapa kwa just mention, bila kuvitaja, lakini kama vitu hivi ni kweli, then, wabunge wanawake wa Chadema, ni mashujaa sana, ni wavumilivu sana na wastahimilivu sana kwa vitu wanavyofanyiwa na viongozi wao, huyu ameshindwa kuvumilia, uvumilivu umemshinda, japo amewastahi lakini amesema katika mabano na hapa ninamnukuu "iliniuma sana pale nilipokataa kuwaabudia viongozi wa chama kitaifa kwa namna itakayo tweza utu wangu" Jee unakujua huko kuabudiwa kunakotweza utu wa mwanamke?.
pia kama mtu mwenyewe ni huyu
View attachment 897540
Na eneo analotoka ni Babati, then kiukweli kabisa, huyu ni shujaa, kwa sababu vitu vingine, na mambo mengine, sisi wengine wenu wenye udhaifu nayo, hata ningekuwa mimi...

Kama tuhuma hii ni kweli, hii inamaana wabunge wengine wanawake wa Chadema, wanavumilia sana.

Hivyo naendelea kusisitiza

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike - JamiiForums

P.
Kusema kweli ametoa hoja za msingi tena kwa marefu na mapana, kwanini anahama chadema na kwenda ccm,
 
Wanabodi.

Hili ni bandiko la swali kuhusu Trend Reading. Wanaohamia CCM Wasibezwe, Wanaona Mbali, 2020 Majimbo Yote Kurejeshwa?, Jee Tunarejea Kuwa Nchi Chama Kimoja?

Trend reading sio utabiri, bali ni matumizi ya analitical na logical thinking kwa kila jambo lililofanyika huangalii tuu hilo jambo lililofanyika bali bali unaliangalia kwa kujiuliza the motive behind jambo hili kufanyika jinsi hiyo lilivyofanyika ni nini? na matokeo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu wa jambo hili ni nini?, ndipo unakuja na conclusion kama hii.

Jambo letu kwenye uzi huu ni ushindi wa CCM kwenye uchaguzi wa marudio wa madiwani kata 43.

Politics is a game of hide and seek and the changing variables, hivyo kwa mazingira ya sasa ya siasa za Tanzania ya Magufuli, wanasiasa karibu wote walioko upinzani, with very few exceptions, wenye uwezo wa kuona mbali kwa kusoma trends za kisiasa kwa kuangalia mwelekeo wa 2020, kwa matokeo haya, watakuwa wameishasoma mazingira yaliyopo na hali halisi ya siasa zetu za Tanzania na siasa za upinzani nchini katika kipindi hiki cha Tanzania ya Magufuli na their chances ya upinzani kushinda kata yoyote au jimbo lolote kuelekea 2020, hivyo, wenye kuona mbali, wameamua kufanya uamuz wa mapema kwa kuvihama vyama vyao sasa kwa kujiunga CCM!, ili ku secure their positions mapema badala ya kusubiri kifo hiyo 2020!

Hivyo kwa hali hii, kama kuna mtu yoyote anataka kuwa na future kwenye politics za Tanzania kuelekea 2020, then mtu huyo, atajiunga CCM now!. Uthibitisho ni matokeo ya uchaguzi huu wa madiwani wa kata 4 kwa jinsi CCM ilivyotetea kata zake zote, na kukomba kata zote zilizokuwa zinasikiliwa na upinzani kasoro moja.

Hivyo kwa wanasiasa wanauojua kutazama mbali kwa kusoma trends, then siasa za Tanzania kwa sasa, CCM ndio mpango mzima!, kama kuna mwanasiasa yoyote, au wowote, wanataka future ya politics kama ajira yao ya kudumu na kukamata ulaji, kujitafunia keki ya taifa, chama cha kujiunga nacho ni CCM!.

Hapa nazungumzia ukweli halisi wa kitu kilichopo, ambao unaweza kuwa ni ukweli mtamu kwa CCM na ukweli mchungu kwa wapinzani, bila kujalisha kama Tume yetu ya Uchaguzi ni tume huru, au la, na kama chaguzi zetu ni changuzi huru na za haki, hapa mimi nazungumzia matokeo ya mwisho tuu, ya kitu kilichotokea, ambacho ndicho kilichopo, ni CCM imeshinda!, bila kujalisha imeshindaje au imeshinda kwa mbinu gani, ziwe ni mbinu halali au haramu, CCM imeshinda kihalali kwa kufanya siasa safi, au kiharamu kwa kubebwa na wasimamizi wa uchaguzi, au upinzani umeshindwa kihalali kutokana na udhaifu wa kukosekana upinzani imara, ama upinzani umechezewa faulo za waziwazi, hapa mimi nazungumzia matokeo ya mwisho ya mshindi ni nani.

Aliyetangazwa mshindi ndiye aliyeshinda, na mshindi ni mshindi tuu, the winner takes it all, the looser standing small, aliyeshinda kashinda, ndiye mshindi na ni mshindi halali kwa mujibu wa kanuni ya "the end justify the means".

Wapinzani poleni sana!, CCM hongereni sana kwa ushindi huu, na hongereni kubwa in advance kwa chaguzi nyingine ndogo zitakazo fuatia, na hongera kubwa zaidi in advance ni hongera ya uchaguzi wa 2020 kwa Tanzania kuendelea kuitwa ni nchi ya vyama vingi jina tuu, lakini actually ni CCM hongera sana kuturudisha kuwa ni nchi ya chama kimoja cha siasa, CCM.

Jumatatu Njema.

Paskali
Rejea
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...

Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha ...

Jee Magufuli Anaimarisha CCM Au Anaua Upinzani?. Tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?.

Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!.

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za ...

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...
Unahalalisha haramu?.. Eti alieshinda kashinda tu and unashabikia ujangilii huu??
 
Unahalalisha haramu?.. Eti alieshinda kashinda tu and unashabikia ujangilii huu??
Kujiunga na chama chochote cha siasa ni hiyari, kujitoa pia ni hiyari na kujiunga na chama kingine chochote, pia ni hiyari.

Kwa watu wanaojua kusoma trends kuelekea 2020, CCM ndio mpango mzima.
P
 
Nashangaa watu wanaona hili ni jipya! Mbona siku nyingi tumeieleza hii 'biashara'

Wanaohama hawana sababu, wana visingizio tu.

Mtolea siku zote hakuona tatizo ndani ya chama chake, eti ameliona baada ya Deadline ya CCM ya tarehe 15 November! Bado watu wanaamini matatizo ndani ya vyama ndiyo sababu

Yeye haku-photocopy ile barua 'standard' yenye neno ''Kujiuzuru' iliyotumiwa na kila mmoja

Manunuzi yana namna zake , Pascal Mayalla umeamini sasa!

JokaKuu
Mkuu Nguruvi3, mimi bado ninaamini, kila anayehama ana sababu, hata kama sababu yenyewe ni ile rushwa tuu ya ahadi ya kusimamishwa tena, nayo ni sababu tosha. Hata kama ni fear of unknown kwa hatma ya upinzani 2020 ni sababu kama nilivyoeleza kwenye bandiko hili.

Ila pia kuna wahamiaji wengine ni very genuine, wakati wanahana wanaandika barua kwa vyama vyao na wanatoa sababu, nilishauri, hawa wasipuuzwe wana hoja za msingi.
CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike - JamiiForums
P
 
Wana sababu kabisa binfasi ambazo ni kuijiandalia hatima njema lakini itakuwa ni shughuli kwao..
Halafu Mbona hamuelezi Upinzani unaokufa ni upi ? wa agenda IPI ?

Madhalani hoja ya Ufisadi mbona haijafanyiwa kazi na wanaoongoza.?
Eleza Ufisadi uliofanyiwa kazi nami nitakuelewa .

Mtu aliyewahi kugombea hata ujumbe ;anayejua kura zinapatikanje; mpaka sasa haoni Ccm iliyosimama Kwa miaka mitano !
 
Wanabodi.

Hili ni bandiko la swali kuhusu Trend Reading. Wanaohamia CCM Wasibezwe, Wanaona Mbali, 2020 Majimbo Yote Kurejeshwa?, Jee Tunarejea Kuwa Nchi Chama Kimoja?

Trend reading sio utabiri, bali ni matumizi ya analitical na logical thinking kwa kila jambo lililofanyika huangalii tuu hilo jambo lililofanyika bali bali unaliangalia kwa kujiuliza the motive behind jambo hili kufanyika jinsi hiyo lilivyofanyika ni nini? na matokeo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu wa jambo hili ni nini?, ndipo unakuja na conclusion kama hii.

Jambo letu kwenye uzi huu ni ushindi wa CCM kwenye uchaguzi wa marudio wa madiwani kata 43.

Politics is a game of hide and seek and the changing variables, hivyo kwa mazingira ya sasa ya siasa za Tanzania ya Magufuli, wanasiasa karibu wote walioko upinzani, with very few exceptions, wenye uwezo wa kuona mbali kwa kusoma trends za kisiasa kwa kuangalia mwelekeo wa 2020, kwa matokeo haya, watakuwa wameishasoma mazingira yaliyopo na hali halisi ya siasa zetu za Tanzania na siasa za upinzani nchini katika kipindi hiki cha Tanzania ya Magufuli na their chances ya upinzani kushinda kata yoyote au jimbo lolote kuelekea 2020, hivyo, wenye kuona mbali, wameamua kufanya uamuz wa mapema kwa kuvihama vyama vyao sasa kwa kujiunga CCM!, ili ku secure their positions mapema badala ya kusubiri kifo hiyo 2020!

Hivyo kwa hali hii, kama kuna mtu yoyote anataka kuwa na future kwenye politics za Tanzania kuelekea 2020, then mtu huyo, atajiunga CCM now!. Uthibitisho ni matokeo ya uchaguzi huu wa madiwani wa kata 4 kwa jinsi CCM ilivyotetea kata zake zote, na kukomba kata zote zilizokuwa zinasikiliwa na upinzani kasoro moja.

Hivyo kwa wanasiasa wanauojua kutazama mbali kwa kusoma trends, then siasa za Tanzania kwa sasa, CCM ndio mpango mzima!, kama kuna mwanasiasa yoyote, au wowote, wanataka future ya politics kama ajira yao ya kudumu na kukamata ulaji, kujitafunia keki ya taifa, chama cha kujiunga nacho ni CCM!.

Hapa nazungumzia ukweli halisi wa kitu kilichopo, ambao unaweza kuwa ni ukweli mtamu kwa CCM na ukweli mchungu kwa wapinzani, bila kujalisha kama Tume yetu ya Uchaguzi ni tume huru, au la, na kama chaguzi zetu ni changuzi huru na za haki, hapa mimi nazungumzia matokeo ya mwisho tuu, ya kitu kilichotokea, ambacho ndicho kilichopo, ni CCM imeshinda!, bila kujalisha imeshindaje au imeshinda kwa mbinu gani, ziwe ni mbinu halali au haramu, CCM imeshinda kihalali kwa kufanya siasa safi, au kiharamu kwa kubebwa na wasimamizi wa uchaguzi, au upinzani umeshindwa kihalali kutokana na udhaifu wa kukosekana upinzani imara, ama upinzani umechezewa faulo za waziwazi, hapa mimi nazungumzia matokeo ya mwisho ya mshindi ni nani.

Aliyetangazwa mshindi ndiye aliyeshinda, na mshindi ni mshindi tuu, the winner takes it all, the looser standing small, aliyeshinda kashinda, ndiye mshindi na ni mshindi halali kwa mujibu wa kanuni ya "the end justify the means".

Wapinzani poleni sana!, CCM hongereni sana kwa ushindi huu, na hongereni kubwa in advance kwa chaguzi nyingine ndogo zitakazo fuatia, na hongera kubwa zaidi in advance ni hongera ya uchaguzi wa 2020 kwa Tanzania kuendelea kuitwa ni nchi ya vyama vingi jina tuu, lakini actually ni CCM hongera sana kuturudisha kuwa ni nchi ya chama kimoja cha siasa, CCM.

Jumatatu Njema.

Paskali
Rejea
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...

Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha ...

Jee Magufuli Anaimarisha CCM Au Anaua Upinzani?. Tunaelekea Nchi ya Chama Kimoja?.

Nini Mustakabali wa Upinzani TZ?

Swali la Ukweli Mchungu: Je, 2020 Magufuli ana mpinzani au mshindani, au Ni Magufuli tu?!.

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za ...

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible ...
Ndugu yangu Paskali, umejadili hoja nzito lakini umeitendea haki. Umejadili kisayansi japo uandishi wako wa kuchanganya kishwahili na kiingereza huwa haunipi raha ila naona wewe unakupa wepesi. Nimekuwa msomaji mahiri wa hekaya zako na kwa hiyo mimi ni mfuatilaji mzuri wa kila unachokiandika. Kuna nyakati unaniudhi na kuna nyakati unanifurahisha. Maneno uliyoyatumia leo tena kwa lugha ya kiswahili yamenivutia sana haya " Ukweli mchungu" kwa wapinzani.

Nimeumia kwa kiwango kile kile cha uchungu wa shubiri, lakini nikawaonea huruma watanzania kwa sababu shubiri hii wataionja kwa zaidi ya miaka mingi ijayo.
Kama unakiona ninachoimanisha, niaze kwa kuwaomba nyinyi waandishi mahiri, anzeni kuielezea shubiri ijayo kwa watanzania hasa baada ya 2020.

Kipindi cha mwisho cha utawala wa Mhe. Kikwete nilikuwa naiona tanzania ilikuwa ikielekea Nigeria na Nigeria ikielekea Somalia. Sasa naiona Tanzania ikielekea Zimbabwe ya Mzee shujaa Robert Mugabe; vile vile naziona Nigeria na Zimbabwe zinaelekea Tanzania. Ubadilishanaji huu hauna tija kwa watanzania. Hivi wasomi hamlioni hili?
Pamoja na ukweli mchungu uliousema nitabaki upinzani na nitajitahidi kusema kwa nguvu zangu zote kuhusu "ukweli mchungu" utakaowakabiri watanzania wenzangu endapo hatutasimama na kuwatahadharisha.
 
Ndugu yangu Paskali, umejadili hoja nzito lakini umeitendea haki. Nimekuwa msomaji mahiri wa hekaya zako na kwa hiyo mimi ni mfuatilaji mzuri wa kila unachokiandika. Kuna nyakati unaniudhi na kuna nyakati unanifurahisha. Maneno uliyoyatumia leo tena kwa lugha ya kiswahili yamenivutia sana haya " Ukweli mchungu" kwa wapinzani.

Nimeumia kwa kiwango kile kile cha uchungu wa shubiri, lakini nikawaonea huruma watanzania kwa sababu shubiri hii wataionja kwa zaidi ya miaka mingi ijayo.
Kama unakiona ninachoimanisha, niaze kwa kuwaomba nyinyi waandishi mahiri, anzeni kuielezea shubiri ijayo kwa watanzania hasa baada ya 2020.

Pamoja na ukweli mchungu uliousema nitabaki upinzani na nitajitahidi kusema kwa nguvu zangu zote kuhusu "ukweli mchungu" utakaowakabiri watanzania wenzangu endapo hatutasimama na kuwatahadharisha.
Mkuu Mechard Rwizile, kwanza asante kwa kuwa msomaji wangu mzuri. Sisi waandishi kazi yetu ni kuona na kuandika tuu, kuna kitu nimekiandika kwenye bandiko hili kuhusu uchaguzi Mkuu wa 2020 ambacho kitatanguliwa na matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, matokeo ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa ndio utawafungua macho watu wengi na ndio sasa watalielewa bandiko langu hili linazungumzia nini kuhusu matokeo ya uchaguzi Mkuu wa 2020.
P
 
Meya wa Jiji la Arusha (Chadema), kalisti lazaro leo Novemba 19, 2019 amekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi

Amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupitia wakati mgumu kutoka kwa uongozi wa chama chake ikiwamo kupokea barua za onyo mara kwa mara ambazo zilimtaka kutokutoa ushirikiano kwa viongozi wa Serikali ambao anatakiwa kufanya nao kazi ngazi ya Mkoa na Wilaya na kutompongeza hadharani Rais Dk. John Magufuli.

Kalisti Lazaro amenena kwamba,
"Nimekuwa nikifanya kazi katika mazingira magumu nakutana na changamoto, nimeshletewa barua nyingi za onyo kwa sababu ya kumsifia Rais, lakini pia siwezi kukaa chama ambacho kimejitoa kwenye Uchaguzi, leo Arusha inaenda kuwa ya CCM sababu wenzetu wamejitoa."

"Nitaendelea kuwa Mwanasiasa kwa sababu niwaombe wananchi wa Kata yangu, nitaendelea kuwatumikia kwa nafasi nyingine ambayo chama changu itaamua mimi nirudi"

View attachment 1266800

Pia soma

Naendelea tuu kusisitiza, hawa watu wanaohamia CCM, wasibezwe!, wanaona mbali!.
P.
 
Back
Top Bottom